LGE2024 Iringa: RC Serukamba ashiriki zoezi la kupiga kura, asema changamoto ya wakala wa CHADEMA yatatuliwa

LGE2024 Iringa: RC Serukamba ashiriki zoezi la kupiga kura, asema changamoto ya wakala wa CHADEMA yatatuliwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Peter Serukamba ameshiriki zoezi la kupiga kura Kuchagua viongozi wa serikali za Mitaa Leo Nov 27 2024.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Akiwa katika Kituo Cha kupigia kura Kata ya Gangilonga Mh. Serukumba amewataka Wananchi kujitokeza kupiga kura Ili kuwapata viongozi watakowaletea maendeleo kuanzia ngazi ya Mtaa, Kitongoji na Kijiji.

Soma Pia: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

Aidha amesema kuwa baadhi ya mawakala wa vyama vya upinzani ambao fomu zao hazikugongwa muhuri wa moto, imeshatatuliwa na wanaendelea na zoezi la uchaguzi katika vituo vya kupigia kura hapa Mkoani Iringa.

Hata hivyo amesema kuwa usalama katika maeneo yote umeimarishwa huku akisisitiza kuwa atakayefanya vurugu katika uchaguzi huo atachukuliwa hatua za kisheria.
 
Back
Top Bottom