Akiwa katika Kituo Cha kupigia kura Kata ya Gangilonga Mh. Serukumba amewataka Wananchi kujitokeza kupiga kura Ili kuwapata viongozi watakowaletea maendeleo kuanzia ngazi ya Mtaa, Kitongoji na Kijiji.
Aidha amesema kuwa baadhi ya mawakala wa vyama vya upinzani ambao fomu zao hazikugongwa muhuri wa moto, imeshatatuliwa na wanaendelea na zoezi la uchaguzi katika vituo vya kupigia kura hapa Mkoani Iringa.
Hata hivyo amesema kuwa usalama katika maeneo yote umeimarishwa huku akisisitiza kuwa atakayefanya vurugu katika uchaguzi huo atachukuliwa hatua za kisheria.