Iron and steel industries Tanzania vs Kenya

Iron and steel industries Tanzania vs Kenya

Mkurugenzi Mkuu wa Kiluwa Steel Group, Bw. Mohammed Kiluwa alimweleza Waziri Mkuu kuwa anatarajia kuanza uzalishaji Januari, mwakani na kwamba ataajiri wafanyakazi wapatao 200.
“Tunataraji kuanza uzalishaji Janruari, mwakani na uzalishaji utakuwa tani 2,000 kwa siku.
k1.JPG

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mitambo ya kiwanda cha chuma cha Kiluwa Steel Group kilichopo Mlandizi Pwani Novemba 19,2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

k2.JPG

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi wa reli inayounganisha reli ya kati na kiwanda cha Kiluwa Steel Group cha Mlandizi Pwani Novemba 19, 2016 . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Bw. Masanja Kadogosa amesema shirika hilo limetumia sh. milioni 863 kukamilisha ujenzi wa reli ya km.5 kutoka njia panda hadi kwenye kiwanda hicho ambapo kati ya hizo km.1.5 zimo ndani ya kiwanda.

Amesema hadi sasa wameshaweka njia nne za reli, moja ikiwa ni mahsusi kwa ajili ya kubeba makaa ya mawe. “Tulilazimika pia kujenga culvert katika eneo moja kwa sababu pailikuwa na shimo kubwa. Tumetumia fedha kidogo kwa sababu tumetumia mafundi wetu badala ya wakandarasi,” ameongeza.
 
Ngoja walete picha za SA na US waseme ni Turkana [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom