Kwanza kabisa kuna drip za mboga mboga na drip za miti kama matunda,tofauti yake ni kwanmba hizi za mboga mboga zinakuwa na emitter tayari na zinakuwa na flow rate ndogo(mostly1.5l/h ,2l/h),hizi drip za miti zenyewe zinakuwa hazina emitter,emitter unaweka mwenyewe kulingana na spacing yako ya miti na flow rate unayohitaji(mostly 4l/h-8l/h) kwahiyo kwenye drip za miti inahusisha BLIND PIPE na BUTTON DRIPPER,
Mfano hapo una shamba la ekari moja lenye miti 75 hapo umetoa spacing ya mti na mti ni 8.9m lakini hujatoa spacing ya ya mstari mmoja wa mti na mwingine,lakini kimahesabu hapo spacing ya mstari mmoja na mwingine itakuwa 4000/(8.9*75)=6m,Chukua mfano hiyo ekari yako moja ina upana wa mita 50 na urefu wa mita 80 size ya blind pipe utakayo hitaji itakuwa (50/6)*80=667m na idadi ya button dripper itakuwa sawa na idadi ya miti yako ambayo ni 75. Baada ya hapo utahitaji vifaa vingine sasa kama connectors,Filter,control valves,air valves,punching tool,na mashine zingine za kazi.
Kwenye eneo kama lina slope au lipo flat kikubwa kinacho tofautisha kwenye ufungaji wa drip irrigation ni kwamba kwenye eneo lenye slope kali ni vyema kumwagilia kwa kutumia blocks ili kusaidia maji kufika eneo lote la shamba maana bila kufanya hivyo maji hukimbilia upande wa chini kwenye slope na mimea iliyo pandwa upande wa chini ndiyo hupata maji vizuri kulinganisha na ile iliyo pandwa upande wa juu,idadi ya blocks inategemeana na ukali wa slope yenyewe.Kwa upande wa shamba lililo flat hapa haihitajiki sana kugawa shamba katika block unaweza kumwagilia shamba zima(ekari moja) kwa mara moja provided tank lipo juu umbali gani ili kuweza kutoa pressure ya maji ya kutosha.Kwa ushauri,vifaa na kufungiwa mifumo hii ya umwagiliaji usisite kuwasiliana nasi kupitia,
+255752022108
ENG.Joseph O Mlang'a
Bsc. Agricultural Engineering
Sokoine University Of Agriculture