Irrigation

Kwa ekari moja unaweza kutumia tank la lita 5000, Kwenye umwagiliaji wa tikiti,Mwanzoni baada ya kuotesha ni lazima kumwagilia maji ya kutosha(mizizi ishike vizuri ardhini) ila baada ya kama wiki tatu una weza kupunguza maji,

Kumwagilia hatuwezi kusema umwagilie baada ya siku ngapi maana inategemea na aina ya udongo,kikubwa ni kupima kama maji yameingia vya kutosha,kwa tikiti ni vyema maji kuingia ardhini kama inchi nne na hii unaweza kupima kwa kutumia kidole.

kama unyevu haujafika ichi nne ardhini unamwagilia.siku kama 10-12 kabla ya kuvuna una stop kumwagilia ili kusaidia sukari kukaa vizuri ili kupata ladha nzuri ya tikiti.
 
bei ya soral pump kwa kilimo cha umwagliaji inaweza fka shngap?
Bei inategemea na mahitaji ya size ya shamba ambalo pump itatumika kwa umwagiliaji,pia inategemea na unataka pump ya kumwagilia kwa kutumia system gani,drip au sprinkler.
 
Kwa Maswali na ushauri please tuyalete hapa,Kufungiwa mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone(DRIP IRRIGATION SYSTEM) kwa ajili ya mboga mboga,parachichi,papai nk please wasiliana nasi kupitia +255752022108.
 
Asante ila embu nielimishe uzuri zaidi pls. Una maanisha kwa ekari nane lazima niwe na simtanks 10? Sasa mbona same tank inamwagia ekari 2 kwa pressure nzuri tu?

Natarajia kutumia system ya drip irrigation
Kuna wataalamu wengi wenye mawazo tofauti. Tatizo ninalo liona kwako ni urefu wa mnara wako. Pia hujasema maji yako una yashusha na pipe ya ukubwa gani pia shamba umeligawaje. Na una tumia system gani ya umwagiliaji.
Naweza kukupa ushauri uka tumia hilo tank kumwagilia eneo lako lote. Nipigie 0754281399
 
Asante ila embu nielimishe uzuri zaidi pls. Una maanisha kwa ekari nane lazima niwe na simtanks 10? Sasa mbona same tank inamwagia ekari 2 kwa pressure nzuri tu?

Natarajia kutumia system ya drip irrigation
Kuna wataalamu wengi wenye mawazo tofauti. Tatizo ninalo liona kwako ni urefu wa mnara wako. Pia hujasema maji yako una yashusha na pipe ya ukubwa gani pia shamba umeligawaje. Na una tumia system gani ya umwagiliaji.
Naweza kukupa ushauri uka tumia hilo tank kumwagilia eneo lako lote. Nipigie 0754281399 Text kwenye hiyo namba
 
NYANGI IRRIGATION DEPARTMENT-NID MAKALA. FAHAMU ZAIDI KILIMO CHA UMWAGILIAJI.
Umwagiliaji ni mtindo wa kilimo wa kupeleka maji kwa mimea shambani pasipo mvua ya kutosha.

Hutumiwa katika maeneo yabisi au wakati mvua ni kidogo. Katika nchi baridi unatumiwa pia kwa kusudi la kulinda mazao dhidi ya jalidi.

Ni kilimo ambacho kinasaidia sana, kwa mfano nchi ya Misri tangu zamani inategemea mto Naili katika shughuli zake za umwagiliaji wa mazao.

Chanzo cha maji
Umwagiliaji hutumia maji kutoka vyanzo mbalimbali:

maji hutolewa kutoka mtoni au ziwani
mwendo wa mto huzuiliwa kwa lambo na maji kutolewa katika ziwa ya lambo
pampu yavuta maji kutoka kisima
Mbinu za umwagiliaji
Kuna mbinu nyingi za kumwagilia mazao. Tangu kale watu walichimba mifereji wa kupeleka maji mashambani. Mashamba yazungukwa kwa ukuta mdogo wa udongo na eneo la shamba lajazwa maji. Kujazwa kwa shamba kunarudiwa hadi mazao (kwa mfano ngano) yamekua. Mazao mengine kama mpunga hukuzwa mara nyingi ndani ya maji yanayofunika shamba kwa miezi kadhaa. Mtindo huu unaendelea kutumiwa hasa katika nchi nyingi za Asia na sehemu kubwa ya mchele duniani inapatikana kwa njia hii.

Mitambo kama pampu imewezesha wakulima kuachana na mifereji na kazi ya kugawa maji. Vinyunyizo vinamwaga maji kwa mashamba. Kuna mashine kubwa zenye matairi zinazozunguka kwenye ncha na kumwagilia duara. Nyingine zinazungushwa kwa nguvu ya maji na kutupa maji hadi umbali wa mita 500.

Katika nchi zenye uhaba wa maji kuna mbinu mpya ya umwagiliaji wa matone; mabomba au mipira yenye matundu madogo yanapelekwa shambani. Mimea inapandwa karibu na tundu la mpira. Wakati wa usiku pasipo joto kali maji yanatoka tone kwa tone kwenye bomba au mpira, hivyo yanafika moja kwa moja kwenye mizizi. Mbinu hii inatumia maji kidogo kulingana na umwagiliaji wa kawaida. Nchi ya Israeli imetangulia kulima mashamba makubwa upande wa kusini kwa njia hii, pamoja na kuwa na ukame sana.

Matatizo
Umwagiliaji huongeza mavuno kiasi kikubwa. Lakini kuongezeka kwa umwagiliaji duniani kumeleta matatizo mengi.

Matumizi ya maji yanazidi akiba yake; mito imekauka kwa sababu watu wengi mno wamechukua maji mle. Mfano mbaya sana ni ziwa Aral iligeuzwa kuwa jangwa kwa sababu maji ya mito yake yametumiwa kwa miradi mikubwa ya pamba katika mazingira ya joto kali tena kwa teknolojia isiyofaa kama mifereji iliyo wazi
Maji mengi yanapotea hasa pale ambako maji hupitishwa kwenye mifereji au na kujaza shamba kumwagiliwa kwa vinyunyizo. Sehemu kubwa inapotea kwa njia ya uvukizaji kuliko kulisha zao.
Pampu zimesababisha kushuka kwa uwiano wa maji chini ya ardhi. Hi ni hofu kubwa kwa umwagiliaji katika jangwa Sahara unaotumia akiba ya maji iliyojengwa na mvua wa milenia nyingi lakini inayopungua haraka tangu kuanzishwa kwa miradi ya umwagiliaji kwa pampu kubwa zinazovuta maji ya chini.
uharibifu wa mashamba ka kuongeza kiwango cha chumvi ardhini; katika mazingira ya joto uvukizaji wa maji unapeleka chumvi iliyoko ardhini juu; maji yavukiza lakini chumvi inabaki. Kuna mifano mingi ambako mashamba yameshaharibika kutokana na kuongezeka kwa chumvi. Maeneo yaliyolisha watu tangu kale yamekuwa jangwa kabisa.
Matatizo haya yote yanaonyesha ya kwamba haitoshi kumwagilia mashamba tu na kufurahia mazao mazuri kwa sababu matatizo yataongezeka baada ya miaka kadhaa. Kwa hiyo ni lazima kuangalia vema mbinu za uimwagiliaji inayolingana na mazingira na kutumia maji kidogo kama vile umwagiliaji wa matone. 0719549848(watsup), head office Dar. Husisahau kufollow page yetu ya Facebook na YouTube channel yetu kwa kuandika NYANGI IRRIGATION. Karibu
 

Tukiendelea na ufungaji wa mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone (drip irrigation system)-MERERANI jijini arusha kwa kilimo cha kisasa cha nyanya

System ikiwa tayari tayari kwa kuanza kazi ya umwagiliaji katika eneo la ekari mbili jijini Arusha.
Tukiendelea na upandaji wa nyanya zilizo andaliwa kitaalamu kabisa kwa kutumia tray na mbegu za kisasa za nyanya za hybrid.


Mche wa nyanya tulio uotesha ukiendelea kupata maji kwa mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone (drip irrigation system.


Nyanya zikiwa katika stage ya maua huku zikiendelea kusimawiwa na wataalamu wetu toka AGRILA FARMING COMPANY LTD, kampuni tuliyofunga mfumo huu wa umwagiliaji kwa njia ya matone unaomwagilia shamba hili.

KWA UFUNGAJI WA MFUMO HUU WA UMWAGILIAJI KWA NJIA YA MATONE PAMOJA NA MAHITAJI YA VIFAA KAMA DRIPLINES,CONNECTORS PAMOJA NA USHAURI USISITE KUWASILIANA NA WAHANDISI WETU WA KILIMO NA UMWAGILIAJI KUPITIA 0752022108 / 0654357571. AGRILA FARMING COMPANY LTD,ARUSHA,TANZANIA.
 
Je unaweza tumia mfumo gani wenye gharama nafuu kwa umwagiliaji wa maharage. NB maji yanatokana na kisima cha kumchimba.

Natanguliza shukurani
Hope tumeelewana boss,Kwa maswali,ushauri,vifaa na ufungaji wa mfumo huu wa umwagiliaji usisite kuwasiliana nasi kupitia +255752022108.
 
Je unaweza tumia mfumo gani wenye gharama nafuu kwa umwagiliaji wa maharage. NB maji yanatokana na kisima cha kumchimba.

Natanguliza shukurani
Swali zuri.Wengi wanaofanya kilimo cha umwagiliaji kwa zao la maharage wanamwagilia kwa njia ya FURROW IRRIGATION yaani umwagiliaji kwa njia ya mifereji,changamoto kubwa ya umwagiliaji kwa kutumia mifereji inakuja kwenye wingi wa maji, JE UNA MAJI MENGI YA KUTOSHA?kumwagilia kwa mifereji kunapoteza maji mengi sana,Pili changamoto nyingine ni maambukizi ya magonjwa ya udongo toka sehemu moja ya shamba kwenda sehemu nyingine ya shamba na baadhi ya magojwa hayo yakisha athiri mmea huwa hayana dawa kabisa (dawa yake ni kung'oa miche iliyoathirika).Mfumo tunaoweza kukushauri na wenye gharama nafuu kwa kilimo cha kisasa cha maharage ni drip irrigation system (umwagiliaji kwa njia ya matone),mfumo huu husaidia sana kwani hutumia maji kidogo sana ukilinganisha na mifumo mingine ya umwagiliaji.Maji humwagiliwa tu pale yanapohitajika(kwenye mmea pekee).Maji humwagiliwa ya kutosha na mmea hukua vizuri na huwa na mazao bora sana,Mfumo huu utakusaidia pia kuokoa muda na mimea kupata muda kwa wakati kwani kwa kutumia mifereji vijana wa shambani wanaweza kukuambia wamemwagilia lakini hawajafanya hivyo yote ni kutokana na ugumu wa shughuli nzima ya umwagiliaji kwa njia ya mifereji.sisi kama wataalamu tunakushauri kumwagilia kwa kutumia drip irrigation system (umwagiliaji kwa njia ya matone.
 
Mkuu kwa kuwa umejitolea kutuelimisha naomba usichoke na maswali.

Je gharama za mfumo wa Drop inaweza kuwa sh. ngapi kufungia kwenye heka moja.
 
Mkuu kwa kuwa umejitolea kutuelimisha naomba usichoke na maswali.

Je gharama za mfumo wa Drop inaweza kuwa sh. ngapi kufungia kwenye heka moja.
 
Mkuu kwa kuwa umejitolea kutuelimisha naomba usichoke na maswali.

Je gharama za mfumo wa Drop inaweza kuwa sh. ngapi kufungia kwenye heka moja.
Kuuliza maswali usiwe na shaka mkuu we uliza tuu na kama kuna wengine wenye maswali tungependa kuyajibu hapa.
Kuhusu gharama za kufunga kwa acre moja inategemeana na baadhi ya vitu kama unataka kufunga single line au double line,chanzo cha maji kipo umbali gani toka shambani na vitu vingine vidogo vidogo,wapo wataalamu wanao chaji gharama kubwa na wapo wanaochaji gharama kidogo sana lakini yote hii ni kutokana na ubora wa material wanazo zitumia katika mfumo,wanaochaji bei za chini sana unakuta wanatumia vifaa vya hovyo ambavyo mkulima anaweza akatumia miezi miwili mitatu vinaanza kupasuka na kuharibika.Kwa sisi tunatumia vifaa vyote vina ubora wa hali ya juu,FITTINGS zetu zote tunatumia za HIGH PRESSURE na bomba zetu zote ni CLASS B vinavyodumu muda mrefu hasa kama mfumo ukitunzwa vizuri, Kwa kutumia vifaa hivi gharama zetu kwa acre moja hufikia wastani wa 2,500,000/=Tshs (kwa single line) japo inaweza kupungua kidogo kutokana na shamba lilivyo.Karibu kama una swali lingine mkuu.
 
Na mm sijabaki nyuma
Mtaalamu naomba unifafanulie ikiwa nina shamba la Hekari 15 na nahitaji kulilima lote kwa mfumo wa umwagiliaji je kisima kimoja kitamudu kutoa maji ya kutosha kumwagilia shamba lote?
Pia ni vitu gani vya muhimu vya kuZingatia kabla cjachimba kisima?

Je eneo la pwani kama chalinze linafaa kilima cha nyanya na matikiti? Au pengine na maharage?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko hivi mkuu,unaweza ukamwagilia shamba lote la acre 15 kwa kutumia kisima kimoja kama utachagua kumwagilia kwa mfumo wa matone (drip irrigation system) kikubwa ni kuhakikisha kisima kinakuwa na maji ya kutosha.Unapomwagilia kwa kutumia drip maji yanayotumika ni kidogo sana kwani maji huenda pale tu yanapotakiwa kwenda(kwenye mmea).Kabla ya kuchimba kisima kwa shughuli za umwagiliaji ni vyema wakakutembelea wataalamu watakao kupa maelekezo ya yapi kisima kingependekezwa kuchimbwa sio tu kwa ajili ya kupata maji ya kutosha bali kupunguza gharama za kufungiwa mfumo wako wa umwagiliaji. Kwa ushauri wa wapi kisima kichimbwe unaweza ukawasiliana nasi tukakutembelea shambani.
 
Asante sana kwa majibu na ufafanuzi mzuri
Ila swali la 3 hujanijibu
Je eneo hilo naweza lima nyanya matikiti au maharage?
Pia endapo nitataka kumwagilia kwa njia ya sprinkler kwa kutumia chanzo cha maji ya kisima je inawezekana?


Sent using Jamii Forums mobile app
 


Tukiendelea na maandalizi ya mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya Matone (drip irrigation system)-CHEKERENI mjini Moshi Kilimanjaro maalum kwa kilimo cha PILIPILI.



Size ya bomba tunazotumia inategemeana na size ya shamba linalofungwa mfumo huu ila kikubwa tunatumia bomba zenye ubora ili zidumu kwa muda mrefu.



Wataalamu wetu wakiendelea na maandalizi ya mfumo kwa kilimo cha pili pili katika shamba la ekari tatu chekereni.mjini.moshi.



Shamba likiwa tayari kwa uoteshaji wa PILI PILI kwa kutumia mbegu za kisasa za pilipili za hybrid.



Pili pili zikiwa zimeshakuwa zikisubiri kukomaa kidogo zianze kuvunwa tayari kwa kupelekwa sokoni.



Pilipili zenyewe zikiwa bado mbichi shambani chekereni Moshi kilimanjaro



PILIPILI zikiwa tayari zimeshavunwa zinaendelea na kuandaliwa vizuri ili ziweze kupelekwa sokoni jijini Arusha.

KWA UFUNGAJI WA MFUMO HUU WA UMWAGILIAJI KWA NJIA YA MATONE PAMOJA NA MAHITAJI YA VIFAA KAMA DRIPLINES,CONNECTORS PAMOJA NA USHAURI JUU YA KILIMO USISITE KUWASILIANA NA WAHANDISI WETU WA KILIMO NA UMWAGILIAJI KUPITIA 0752022108 / 0654357571. AGRILA FARMING COMPANY LTD,ARUSHA,TANZANIA.
 

Attachments

  • mtaro copy.jpg
    192.2 KB · Views: 7
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…