Irrigation

Wapo wakulima wanaolima nyanya,tikiti na maharage kwa mkoa wa pwani ila tunachokushauri ni vyema ukafanya kwanza vipimo vya udongo katika shamba lako ili kuweza kufahamu ni mazao gani unaweza ukazalisha vizuri katika shamba lako,hili huweza kufahamika tu baada ya kupata majibu ya virutubisho vilivyopo katika udongo wako. Kumwagilia kwa njia ya sprinkler inawezekana kabisa ila lazima uwe na kisima chenye maji ya kutosha kwani umwagiliaji kwa kutumia sprinkler huhitaji maji mengi sana.
 
Mkuu kuna hiki kiporo niliuliza mwezi june uliahidi kutoa mchanganuo wa gharama kwa miti ya matunda kama parachichi.
Space yangu ni 7m*7m jumla miti 80 kwa acre, chanzo cha maji mto usiokauka hapo hapo shambani, shamba lina mteremko maji yanashuka kirahisi yakishafika kwenye tank.
Ninachohitaji ni mchanganuo wa acre 1 na 10 ( tank la lita 5000 linaweza kuhudumia miti mingapi?)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
utatusamehe boss,soon nitakurudia na mchanganuo mkuu
 

Tukiendelea na ujenzi wa greenhouse ya chuma mjini Moshi KILIMANJARO,greenhouse hii ni ya upana wa mita 8 na urefu wa mita 15,Tunazijenga kwa kuzingatia utaalamu kuanzia structure nzima, Crop support system, Drip irrigation System, Stand ya tank pamoja na tank la lita 1000.

Vijana wakiandaa zege kwa ajili ya kujengea greenhouse, ratio nzuri ya cement, kokoto na mchanga ni kitu tunachokizingatia sana ila kuhakikisha greenhouse tunayoijenga inakuwa imara ili kumuwezesha mkulima kuweza kuitumia katika uzalishaji kwa muda mrefu.

Ujenzi ukiendea, Wapi greenhouse ijengwe?, itatakiwa iwe katika uelekeo upi? Ijengwe kwa height gani? Vyote vinazingatia baadhi ya vitu ambavyo vyote ni vya kiutaalamu na vinakuwa tofauti sehemu moja na nyingine.


Greenhouse ikiwa imeshafunikwa, hapa huwa tunatumia special greenhose plastic cover ambazo zinakuwa na sifa tofauti tofauti kulingana na greenhouse itatumika kuzalisha nini na process nzima ya uzalishaji,zipo plastic cover ambazo zina ruhusu ultra violet rays kutoka kwenye mwanga wa jua kupita na zipo zinazo block ultraviolet rays kutoka kwenye mwanga wa jua kuingia ndani ya greenhouse.Tunapopanda mimea ndani ya greenhouse ambayo hutegemea baadhi ya wadudu kama nyuki kusaidia katika uchavushaji basi kutumia greenhouse cover ambazo zinaruhusu uv rays ni muhimu kwani uv rays husaidia wadudu hawa katika ku navigate.Kama unapanda mimea ambayo haihitaji wadudu hawa katika uchavushaji basi kutumia plastic covers ambazo zina zuia uv rays ni jambo la muhimu kwani husaidia kuzuia wadudu kama whiteflies,thrips,aphids na wadudu wengine.
Mbali greenhouse plastic covers kwa pembeni greenhouse hufunikwa na Insect net maalum kwa kuzuia wadudu na pia kusaidia katika mzunguko wa hewa ndani ya greenhouse.

Muonekano wa ndani ya greenhouse kabla ya kufunga system ya umwagiliaji kwa njia ya matone (drip irrigation
system)

Nursery ya kisasa kabisa ikiwa inaendelea kutengenezwa kwa ajili ya kupandia miche itakayopandwa ndani greenhouse tunayoendelea kuitengeneza.Ili kuhakikisha ubora wa miche tunatumia seedling tray pamoja na udongo maalum kwa ajili ya kupandia(pithmoss) miche katika shughuli nzima ya kupanda mbegu.

Greenhouse ikiwa imekamilika tayari kwa mkulima kuendelea na maandalizi mengine kutokana na zao analotaka kupanda ndani ya greenhouse.


Tunatarajia fufanya uzalishaji wa hoho za rangi katika greenhouse hii ambapo uzalishaji wake utakuwa 100% ORGANICALLY.

KWA UJENZI WA GREENHOUSE, UFUNGAJI WA MFUMO WA UMWAGILIAJI KWA NJIA YA MATONE(DRIP IRRIGATION SYSTEM) PAMOJA NA MAHITAJI YA VIFAA KAMA SEEDLING TRAYS,UDONGO WA KUPANDIA (PITHMOSS) ,DRIPLINES,CONNECTORS PAMOJA NA USHAURI USISITE KUWASILIANA NA WAHANDISI WETU WA KILIMO NA UMWAGILIAJI KUPITIA 0752022108 / 0654357571. AGRILA FARMING COMPANY LTD,Where Farming Meets Technology.
 
Project hii imefanyika bagamoyo,Tanzania.Tumeanza kuanzia maandalizi ya awali ya shamba, usimamiaji wa upigaji wa matuta,uandaaji wa miundombinu ya ufungaji wa mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone(drip irrigation system) pamoja na ufungaji wa mfumo huu tayari kwa kilimo cha kisasa cha nyanya.Kwa ufungaji wa mfumo huu usisite kuwasiliana nasi kupitia +255752022108 / +255654357571.
 

Attachments

  • bagamoyo.mp4
    37.3 MB
Mkuu kilimo cha pilipili iko kinafaa maeneo gani hasa


Sent using Jamii Forums mobile app
Kilimo cha pilipili kinafaa eneo lolote kikubwa tunashauri kuanza kwa kufanya vipimo vya udongo kujua aina ya udongo katika shamba unalotaka kuanza kilimo chako cha pilipili lakini hapo kwenye picha pilipili hio ililimwa chekereni moshi kilimanjaro.
 
Kwa sasa kuna kipimo maalum cha kujua kama kuna maji ardhini
(Shambani,nyumbani nk),wingi wake na ni ya chumvi au la kabla hujachimba.Kwa muhitaji mawasiliano ni 0744572145.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUKIWA KATIKA UJENZI WA GREENHOUSE 16M KWA 45M KATIKA WILAYA YA HAI MKOANI KILIMANJARO KWA UZALISHAJI WA KISASA WA MICHE.



Maandalizi ya chuma(galvanized) tayari kwa kuanza kuzisimamisha ili kupata strength ya kutosha kuhimili vikwazo kama upepo


Tukiendelea na maandalizi ya zege kwa ajili ya kusimamisha chuma, uchanganyaji huusisha ratio maalum ili kuzipa chuma strength ya kutosha.


Chuma zikiwa tayari zimesimama tayari kwa kuendelea na hatua zingine zinazofuata


Arc zikiwa zimewekwa vizuri katika chuma zilizosimamishwa tayari kuendelea na hatua muhumu inayofuata ya kufunika greenhouse kwa greenhouse polycover.

Zoezi la ufunikaji wa greenhouse kwa kutumia greenhouse polycover ukiendelea,hatua hii huhitaji watu wengikidogo.


Greenhouse ikiwa katika hatua ya mwisho kabisa ili kuhakikisha neti inafukiwa vizuri ili kuhakikisha wadudu hawapiti kuelekea ndani.

Greenhouse ikiwa imeshakamilika kwa 100% tayari kwa uzalishaji wa miche mbalimbali kama vile nyanya,matango,hoho n.k.

Kwa ujenzi wa greenhouse za kisasa kabisa kampuni yetu ya AGRILA FARMING CO LTD inauzoefu wa kufanya greenhouse yako kuwa imara na kujengwa kwa kuzingatia utaalamu.Wasiliana na Mhandisi wetu Eng. Joseph O mlang'a kwa simu nambari +255752022108.
 
Greenhouse za mfumo huu ukijenga sehemu zenye joto zinakua na ufanisi kweli kama hazina vent juu au kwenye mikoa yenye joto kali kama dar na pwani mnajenga greenhouse za mtindo gani

Mtu akiwa na skeleton yake na amejenga mwenyewe mnaweza kumuuzia vifaa kama polycover na insect net?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aina za greenhouse zinatofautiana kutoka sehemu moja kwenda nyingine,greenhouse tunazojenga maeneo kama Dar es salaam mbali na kwamba lazima ziwe na vent, height yake huongezeka kidogo kuhakikisha tunapata mzunguko wa hewa wa kutosha kupunguza joto linaloweza kuathiri mazao ndani.Kuhusu materials zote pia tunazo poly cover (clear na Yellow), profifes,zigzags, selfdrilling screws, anti-insect net vyote vipo.
 
Sawa mkuu kwa maelezo mazuri,je mna jenga pia za miti?

Na kwa nini greenhouse nyingi huwa zinaachwa yani watu wana fail baada ya kuzijenga au hazina faida?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu kwa maelezo mazuri,je mna jenga pia za miti?
Tunajenga pia za miti kutokana na size unayotaka.

Na kwa nini greenhouse nyingi huwa zinaachwa yani watu wana fail baada ya kuzijenga au hazina faida?

Swali zuri. Unajua mkuu kilimo biashara ni biashara kama biashara zingine, kujenga greenhouse tu haitoshi kufanya mkulima kupata mafanikio katika biashara yake ya kilimo.Kuna mambo mengine mengi ambayo mkulima ni lazima ayafahamu ili aweze kupata mafanikio katika greenhouse yake na ndio maana mbali na kwamba wapo wakulima wanaotelekeza greenhouse zao wapo wakulima wengine ambao kila mwaka wanaongeza greenhouse katika mashamba yao ili kukuza miradi yao ya kilimo.Ni lazima mkulima awe na uzoefu wa kutosha hasa katika upande wa masoko,utaalamu na spirit pia ya ujasiriamali kwani unapojenga greenhouse yako na hukanyagi kabisa shambani ni rahisi kudangwanywa na vijana wa shambani kwenye mambo mengi,mwisho wa siku mkulima akipata hasara utathubutu kusema ni greenhouse imemkwamisha? Mfano mkulima ambaye tulikuwa tunamjengea hapo juu yeye anazalisha miche,yeye alikuwa ana greehouse aliyokuwa anazalishia miche ila orders zimekuwa nyingi ameamua kuongeza greenhouse nyingine.Je mkulima kama huyu unategemea kuna siku ataitelekeza greenhouse yake?.Tunarudi pale pale greenhouse peke yake haitoshi kumfanya mkulima anufaike na kilimo.
 
Faida kuu tatu za udongo maalum wa kupandia miche uitwao Peat Moss

PEAT MOSS NI NINI?

Peat moss ni udongo maalumu unaotumika kwa ajili ya kuandaa miche hasa kwenye upande wa miche ya mboga mboga na matunda kama vile nyanya,hoho,papai n.k Udongo huu huzalishwa katika nchi za ulaya kama vile Norway,Finland na husambazwa duniani kote ili utumike katika shughuli za uoteshaji wa miche kwani umetengenezwa kuwa na sifa zote maalum zinazohitajika katika uotaji wa mbegu ukilinganisha na udongo huu wa kawaida tunaoutumia kupandia mazao yetu mashambani.Peat moss huenda sambamba na matumizi ya seedling trays,tray maalumu ambazo hutumika kupandia mbegu na kukuzia miche kitaluni.


Fig 1 Udongo wa peat moss unaotumika kupandi mbegu kwa maandalizi ya miche

Fig 2 Miche iliyotayari ikiwa imepandwa ndani ya tray kwa kutumia Udongo wa Peat moss
KWANINI WAKULIMA WENGI HUPENDELEA KUTUMIA UDONGO WA PEAT MOSS?

Wakulima wengi hapa nchini kwetu wameanza kupenda kuzalisha miche kwa kutumia udongo huu maalum wa peat moss kwasababu mbegu za kisasa za hybrid huuzwa ghali kidogo ukilinganisha na hizi mbegu za kawaida za OPV na mara nyingi mbegu hizi huuzwa kwa punje na gharama ya punje za zao kama nyanya hufikia mpaka 150/= Tsh kwa punje moja hasa kwa mbegu za hybrid za ndani ya greenhouse.

Mkulima anapoamua kulima kwa kutumia punje hizi ni lazima ahakikishe punje hizi zinaota zote ili kuepusha hasara anayoweza kuipata pindi punje hizi za mbegu zisipo ota kama zinavyotakiwa kutokana na matatizo mbali mbali yanayosababishwa na Udongo.Udongo wetu huu wa kawaida unaweza kutumika lakini kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo magonjwa,rotuba na sifa mbali mbali za udongo si mbegu zote zinaweza zikaota kama inavyotakiwa kitu ambacho kinaweza kuleta hasara kubwa sana kwa mkulima.Ili kuweza kutatua changamoto hii wakulima wamekuwa wakipenda kutumia udongo huu kwani umetengenezwa ukiwa na sifa zote muhimu zinazotakiwa kwa uotaji na ukuaji wa mbegu.


Fig.3 Udongo wa peatmoss ukiwa katika package ya Kilo 50

FAIDA KUU TATU ZIPATIKANAZO PINDI MKULIMA ANAPO TUMIA UDONGO MAALUM WA KUPANDIA WA PEAT MOSS

(i)Udongo wa peatmoss unauwezo mkubwa wa kuhifadhi maji pamoja na hewa ya kutosha.


Moja ya sifa kuu ya udongo huu maalum wa peatmoss ni uwezo wake mkubwa wa kutunza maji na hewa ya kutosha kwa shuguli mbalimbali za mmea ikiwemo utengenezaji wa chakula.Udongo huu huweza kuhifadhi maji mara 20 ya uzito wake wenyewe na kuyaachia maji haya pindi yanapohitajika na mmea.Udongo huu pia huhifadhi hewa ya kutosha kwani hewa ya oxygen huhitajika sana na mmea hasa kwenye mizizi ili mmea kukua vizuri.

ii)Udongo huu hauna magonjwa wala magugu

Udongo huu maalum huwa hauna kabisa magojwa yeyote yanatoambatana na udongo ambayo huweza kuleta changamoto katika germination ya mbegu pamoja na ukuaji wa miche pindi iwapo kitaluni.Tunapotumia udongo wetu huu wa kawaida changamoto kubwa tunayokuwa nayo ni kutokua na uhakika juu ya afya ya udongo kwani udongo unapokuwa na vimelea vya magojwa mbegu kuota huwa ni ngumu.Udongo huu unapotumika husaidia pia kupunguza uwepo wa magugu ambayo hushindania mbolea na miche pindi tunapotumia udongo wa kawaida wa kupandia.

(iii)Udongo huu hauhitaji kuchanganywa na kitu chochote pindi unapotumika

Pindi Udongo wa peatmoss unapotumika kupandia miche,hauhitaji kuchanganywa na kitu chochote wala mbolea yeyote kwani umetengenezwa ukiwa na kila sifa zote zinazohitajika kwa uotaji wa mbegu pamoja na ukuaji wa mche.Hauhitaji kuchangwanywa na chochote mbali ya dawa zinazotumika kupiga miche pindi miche inapokua.Kilo moja ya udongo huu hutosha kujaza Tray Mbili wakati wa kupanda.

Kwa mahitaji ya udongo huu wa kupandia wa PEAT MOSS usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba +255752022108 | 0654357571.Tunauza 3500/= Tsh kwa kilo na pia upo kwa package ya kilo 50 ambao tuna uuza 1,70,000/=Tsh. SEEDLING TRAYS pia tunazo zenye idadi ya matundu tofauti tofauti kwa gharama ya 5000/=Tsh kwa tray. KARIBU KWA SWALI LOLOTE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…