Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Uchaguzi wa Urais Zanzibar uko njiani unakuja.
Historia ya uchaguzi visiwani inazidi kupambika na kuwa ya kugusa hisia ya kila mwanafunzi wa somo la historia ya siasa za Zanzibar na Afrika.
Dkt. Hussein Mwinyi mtoto wa Rais Ali Hassan Mwinyi ni mgombea wa pili kuchukua fomu za kugombea urais wa Zanzibar kutoka koo zilizotoa rais wa Zanzibar.
Ali Karume, baba yake Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa rais wa Zanzibar (1964 - 1972)na mwanae Amani Abeid Karume akawa rais pia (2000 - 2010)na hivi sasa mdogo wake Amani Karume, Ali Karume kachukua fomu anataka kugombea urais.
Nini sifa ya kuwa rais wa Zanzibar?
Yawezekana kuwa moja ya kigezo ni kuwa baba alikuwa rais?
Katika hali kama ile iliyopelekea Amani Karume kuwa rais, wagombea wengine ambao baba zao hawakukalia kiti cha urais wa Zanzibar wana nafasi na tegemeo gani la kuweza kuchaguliwa kugombea?
Tuje katika fikra ndani ya bongo za watoto wa marais wanaotaka na wao kama baba zao wawe marais.
Wanaijua kwa uhakika wake nguvu ya wananchi wa Zanzibar wapiga kura pale wanapokuwa peke yao ndani ya kizimba kupiga kura?
Haiyumkiniki kuwa hawajui na hawahitaji kuingia maktaba kusoma historia ya chaguzi za Zanzibar baada ya vyama vingi.
Rejea za wao kuzisoma wanazo ndani ya familia zao achilia mbali kuwa wao wenyewe siku zote wamekuwa sehemu ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Wagombea hawa watoto wa marais waliopita wanajua kinachowakabili.
Hivi inawezekana kuwa hawa watoto wa marais ikiwa watapitishwa kugombea watakuja na mbinu mpya ya kuteka nyoyo za Wazanzibari ili washinde uchaguzi kwa amani na salama?
Kuwa mtoto wa rais anaegombea urais wa Zanzibar ni mtaji kwao au ni kubebeshwa gunia zito la misumari yenye ncha kali mchana wa jua kali?
Maswali kama haya na "plot," mfano wa hizi ndizo Irving Wallace alizokuwa akitumia kuandika vitabu vilivyouzwa nakala milioni na kitabu kutengenezwa senema za kusisimua.