Is a big loan worth it??

Neno nalo

Member
Joined
Jun 10, 2013
Posts
67
Reaction score
54
Za muda huu watafutaji wenzangu. Mimi nina mambo machache naomba kujuzwa na kusaidiwa kupanua upeo.

Kwa muda sasa nimekuwa na biashara yangu kichwani na kuiandalia business plan. I see myself soaring heights nayo na kabisa naona its an opportunity, ukiachia mbali kuwa ni hobby pia. Utata uko kwenye wimbo wa taifa, Mtaji.

Napenda kuuliza, Je mkopo mkubwa ni wazo jema kuisimamisha biashara yako vema kuliko kudunduliza miaka na bado usiweze timiza ndoto kwa wakati pangwa?

Kwanini Watanzania wengi ni waoga wa mikopo mikubwa? Je ni riba au hofu ya kutumia mkopo hovyo?

Nimesoma makala nyingi za waliofanikiwa na kupiga hatua kubwa kibiashara na wengi wao walifikia kukopa, mbona waliweza fanikiwa? Je niogope kuprocess mkopo mkubwa? Naomba kujuzwa the risks.

Nimechoka kudunduliza na hali naona wazi nahitaji mtaji mpana na biashara yangu itanilipa sana tu ilimradi nimesimama wima na kujipanga sawia.

Kumradhi kwa kuchanganya lugha.

Karibuni kwa msaada wa mawazo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…