Is Harmonize a yesterday news?

Is Harmonize a yesterday news?

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Dizain kama mambo yanakua magumu kwa kijana wetu, ngoma mbili nje ya management yake ya zamani, Uno na Kushoto Kulia, ya kwanza ilikua pushed sana media tour Afrika ya Mashariki, interview kali pale Clouds na Efm hadi wakamuandalia open concert, atleast ikapata views milioni ndani ya siku mbili tena audio.

Hii ya pili mapokezi yake yanasuasua; media kama zimemtosa hivi, amebaki peke yake na matokeo yake ndo kama haya hapa chini.

Screenshot_20191123-171244.png


By the way, nalia na hii management yake mpya; naona wanashindwa kuendeleza kipaji cha huyu Mwamba wa Kusini, lawama zote nazitupa kwa Jembe ni Jembe unamuangusha kijana wetu, msanii pekee anaepeperusha bendera ya nchi yetu ya Jamhuri ya watu wa Kusini na majimbo yake mawili Lindi na Mtwara.

Wenyewe tunamtegemea, msitake kutuhujumu na huku kwenye sanaa kama mlivyofanya kwenye gas, Dangote Cement, korosho na mbaazi.
 
Lazima kuwa na jicho la kibiashara, ngoma aliotoa sahivi si nzuri kushinda UNO!!,

Niliisikiliza ile beat wanayosema kaiba, inafanana kidogo na UNO, ila kama ile beat angepewa Harmonize angeimba kushinda kina King Kaka!

Harmonize anatakiwa atulie na aje katika namna fulani nzuri bila kutifuana na watu bali kazi zenye kubamba, mashabiki tupo.
 
Numbisa, Wewe ndio maana ukawa na ng'onda!
Mashabiki ndio wanamtengenezea stunts Mmkonde na si WCB.

Diamond hajawahi kumzungumzia vibaya Harmonize tena huwa anajaribu kufanya kama hakuna lolote limetokea vilevile Harmonize, hadi huwa nahisi kuna mchezo unachezeka behind ni eidha wanamuunguza Alikiba au wanatengeneza balance ya media zao.

Kibongobongo mtu hawezi kuwekeza kwao from the scratch uwe mkubwa kama mbuyu eti ndo ujifanye kuachana naye na bado akuchekee haiwezekani wale wana jambo.
Harmo akiulizwa swali la WCB lazima alitolee maelezo kuna interview kafanya na NBS Uganda hajui lugha ya malkia ila alilazimika tu kujaribu ila Simba akiulizwa atajibu once alafu kujichekesha kwingi imeisha hiyooo
 
Watu wamemzoea konde akiwa wcb so wanatengemea katoka basi afanya makubwa kuliko akiwa wcb na wengine hawaamini kama konde anaweza kufanya mziki bila wcb.

Ikumbukwee kipindi diamond anatoka kwa papa misifa na Bob junior. Alitoa ngoma ya moyo wangu .. wengi walisema ndomwisho wake Bora arudi .. kwa Bob junior na alivyo toa mawazo ndo kabisa wengi walimponda ila baada ya wiki mbili ilikuwa hit .. na mpaka Leo yupo juu so kondee .

Niwakumpa mda tuu .. namtabiria atafika mbali nakupeperusha bendera vema kamaanavyo fanya diamond simbaa
 
Back
Top Bottom