Is it fair?

Is it fair?

Ambassador

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2008
Posts
933
Reaction score
75
Mshikaji wangu mmoja anayeishi Dar ana rafiki yake wa kike wa siku nyingi anayeishi mkoani. Siku chache zilizopita alimuomba amtumie nauli aje Dar kutembea. Jamaa hakufanya ajizi akamtumia kilo 1 ghafla.

Huyo dada alifika Dar Jumatatu ya wiki iliyopita kama alivyoahidi na kupokelewa na ndugu zake, akimuahidi mshikaji kwamba wangeonana kesho yake. Tatizo tangu afike amekuwa busy sana na ndugu zake kiasi amekosa muda kabisa wa kuonana na mshikaji, zaidi ya kuwasiliana nae kwenye simu na kumpa ahadi moto moto.

Jamaa kachoka na ahadi za uongo na ameamua kuwa mpole mpaka huyo dada atakapopata muda wa kumtafuta na kuwa nae, kama sio kurudi mkoani bila kuonana nae. Hivi huyu shemeji yetu anamtendea haki kweli mshikaji?
 
jamaa yako mpaka hapo ni kwamba anachunwa........mpe pole
 
Yani hiyo sio fair kabisa, Huyo Demu atakuwa na psychological problems, yana anatumia mgongo wa jamaa kumaliza shida zake!!!
 
mhhhhh kwanini huyu jamaa asimfuatilie mwenyewe.....
jamaa aende kwao ili huyu dada amueleze ni nini kulikoni...
ili ajue cha kufanya maana naona hii ni kupotezeana muda tu.... kwa kweli.
 
Mshikaji wangu mmoja anayeishi Dar ana rafiki yake wa kike wa siku nyingi anayeishi mkoani. Siku chache zilizopita alimuomba amtumie nauli aje Dar kutembea. Jamaa hakufanya ajizi akamtumia kilo 1 ghafla.

Huyo dada alifika Dar Jumatatu ya wiki iliyopita kama alivyoahidi na kupokelewa na ndugu zake, akimuahidi mshikaji kwamba wangeonana kesho yake. Tatizo tangu afike amekuwa busy sana na ndugu zake kiasi amekosa muda kabisa wa kuonana na mshikaji, zaidi ya kuwasiliana nae kwenye simu na kumpa ahadi moto moto.

Jamaa kachoka na ahadi za uongo na ameamua kuwa mpole mpaka huyo dada atakapopata muda wa kumtafuta na kuwa nae, kama sio kurudi mkoani bila kuonana nae. Hivi huyu shemeji yetu anamtendea haki kweli mshikaji?

it is fare but not fair!!!!!!!!!
 
kwani ka maindi iyo laki au anataka kingamuzi chake,ka vip akifate maeneo kilichopo.......... urreeeee mkiibiwa mnakuwa wakali kama pilipli
 
safi sana nampa big up huyo dada, na wengine wenye tabia kama hizo wakome;
1. wanawake wamekwisha Dar mpaka aagize? Im sure jamaa sio inocent
2. Kama jamaa ni inocent kwanini anaogopa kuwa face ndugu wa dem
3. Jamaa hatambuliki kwa ndugu afanye juhudi atambulike.
4. Kuna jamaa katoa dau kubwa
 
Duh!! Mpe pole huyo jamaa but amwache ila ampe condition kuwa
kama kweli amekuja kwa ajili yake aende kwa jamaa la sivyo ndoa imekufa
coz angejua kaja kwa ndugu kwann wasimtumie nauli wao??!!
Hawa mademu taaaabu kwelikweli!!!
 
Kwani huyu jamaa na huyo demu wake wako kwenye mkataba gani (ndoa, wachumba au marafiki tu?) Kama ni marafiki tu basi inabidi akubaliane na hali halisi. Maana demu kafika kwa ndg zake na labda amejaribu kutafuta mbinu za kuwatoka ili aende kwa jamaa zinashindikana. Jamaa kama anampenda kweli demu basi aende akajitambulishe kwao ili wakati mwingine iwe rahisi kuaga toka kwa ndg kuwa anakwenda kwa mchumba; bila hivyo mambo yatakuwa ni hivyo siku zote wengine watoto wa mageti.
 
Mwambie asubiri kumpa nauli ya kurudi tena mkoani kupenda ni kazi
 
The fare was fair kabisa maana aliombwa akakubali kutuma na hakuomba guarantee yoyote.
 
Hao ndio akina dada pia wake zetu watarajiwa/wake zetu (kwa waliooa). Mpe pole na mwambie akae kimya aone huyu dada atafanya nini, maana akimfuatafuata sana anaweza akaja kwa kukwepa usumbufu, amwache atimize lengo lake then baaday ya kuona mwisho wake afanye uamuzi
 
Asife moyo brazamen, kama huo mtego haukushika atege mwengineee!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom