Reinhard1941
New Member
- Aug 30, 2010
- 2
- 0
Kuna ndugu yetu naye ni mjerumani hupo humu ndani ya JF, anaitwa Kipala, nakushauri uwasiliane naye.Wapendwa,
mimi ni Mjerumani. Najitahidi kujifunza Kiswahili.
Swali langu: Je, kuna neno katika lugha ya Kiswahili linalotumiwa kuonyesha kwamba wanaarusi wawili walifunga ndoa yao, kama neno la "couple" katika lugha ya Kingereza?
Kuna neno tofauti kwa ndoa ya Kikristo ya mtu mmoja na mke mmoja? Au ni neno lilelile kwa ndoa za wake wengi za Waislamu?
Au neno la ndoa au arusi zinaruhusu ndoa za wake wa kila namba?
Poleni, jamani,
Jibuni tafadhali.
reinhard1941
karibu katika lugha yetu hii adhimu ya kiswahili!,
vema; kuhusu couple marriage kwa kiswahili ni "mitara" kwa maana ya ndoa ya mwanamme na wanawake zaidi ya wawili.lakini
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971; "Ndoa ni muunganiko wa hiari baina ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kuishi muda wote wa maisha yote" hapa hawajataja kuwa mwanaume na wanawake. japo hata kama ni zaidi ya mke mmoja sheria inasema ni lazima muunganiko huo uwe wa hiari kwa maana ya kuwa wote wawili waridhiane kuwa pamoja.
Na kuhusu neno ndoa kama linamaanisha wake wengi au mmoja sina hakika na hilo
labda kama kuna mtu mwingine mwenye uelewa tofauti atusaidie.

Nashukuru, huenda pengine ni mitala, labda tunaweza kurejea katika kamusi ya kiswahili sanifu kama ni neno lipi ni sahihi.Kwanza niseme kwamba kwa uelewa wangu neno sahihi ni "mitala" na sio "mitara" kumaanisha neno la kiingereza "poligyny" yaani ndoa ya mume 1 na wake zaidi ya 1. Kwa hiyo ndoa ya kiislamu ya mke zaidi ya mmoja inaitwa "ndoa ya mitala". Sheria ya Tanzania haitambui ndoa za mitala zinazowahusisha mke 1 na wanaume wengi, yaani "poliandry" kwa kiingereza. Hizi ni utamaduni wa India!

Kuhusu neno "couple" sidhani kama kuna kiswahili chake cha tofauti na "wapenzi wawili" au kwa kifupi "wapenzi". Unaweza pia kutumia neno "wanandoa" kama tayari wamekwisha oana hasa kwa kuwa muuliza swali amesisitiza kuwa "wanaharusi wawaili walifunga ndoa" akimaanisha kuwa ni watu waliooana tayari.

Neno "ndoa" kwa sheria za Tanzania lina maanisha ya mke mmoja au wengi. Hii ni kwa kuwa sheria hiyo ya 1971 inaruhusu ndoa za aina 3. i.e. ndoa ya mume 1, mke 1 au mume 1, wake wengi. Hizi ni za kiristu (mke 1), za kiislamu (wake wengi) na za kimila (wake wengi). Tena inatumia maneno "potentially poligamous" inapozungumzia ndoa za kiislamu na za kimila.

Endelea kujifunza.

Asante
Ni MITALA, ila wengi ukosea na kuandika MITARA.

Nashukuru, huenda pengine ni mitala, labda tunaweza kurejea katika kamusi ya kiswahili sanifu kama ni neno lipi ni sahihi.
Nashukuru, huenda uko sahihi lakini nilirejea katika kamusi ya kiswahili na limeandikwa mitara, tusaidiane kama lipi ni sahihi au yote yanatumika
inawezekana akawa ni mjerumani kweli kwani nao kiingereza si lugha ya pili?Aisee mtoa mada ninao wasiwasi juu yako; Kwanza, umejiunga 30 Agosti 2010 na hapa ndipo ume-post kwa mara ya kwanza, ni muda mrefu sana umepita; Pili kichwa cha mada yako kinasomeka 'Is there a Swahili world for a marriage of two people - like couple in English?'
Pale pekundu ndipo nilipoona shaka kama wewe ni Mjerumani kweli! Neno lililotumika hapo pekundu liko mbali mno na lengo la mada yako! Anyway subiri majibu zaidi ya Wana JF.
Jamani, tukumbuke pia kwamba neno "couple" halimaanishi watu waliooana pekee, bali linamaanisha pia watu wanaopendana na kuishi pamoja. Kwa maana kwamba, siyo lazima kuwepo na ndoa; ya kanisani, msikitini au ile ya msajili.