Mdau hapa naona haiko sawa.
Watu tunahistoria ya kusomeshwa na wazazi wetu kupitia SACCOS kwa mokopo na marejesho ya fedha kidogo kodogo za mama zetu wakaanga vitumbua.
Tumesoma shule za private kwa kuwa ni serikali hii haikutaka kutupangia shule zake kwa kuwa ufaulu wetu ulikuwa ni wa kiwango cha chini.
Hali imeeendelea hivyo hadi katika ngazi za diploma, na hii yote ni katika kutafuta sifa linganishi za kutuwezesha kufika huko kwenye vyuo vikuu, na Mungu amesaidia hili.
Sasaserikali ikifikiria sisi kupitia njia mbadala kuwa tuna uwezo inakosea kwani nayo pia ni sababu ya sisi kusomeshwa shule na vyuo hivyo, na si kwamba wazazi wana pesa la hasha; wamekopa sana ktk SACCOS hizi hadi wamepoteza sifa za kukopesheka tena kwa kuwa madeni walionayo ni makubwa mno.
Kwa wale waliopewa wakadisco, bado pia wana haki ya kupata tena siku wakimaliza masomo wakafaulu basi watarejesha madeni.
Ni ukiritimba wa serikari na watu wachache iliowakabidhi hatamu za kuvisimamia vyombo hivi vya fedha.