Is this one Kenyan?

Is this one Kenyan?

REDEEMER.

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
8,925
Reaction score
14,890
Screenshot_2018-12-26-07-43-34.png

๐Ÿ˜” What a naked pain truth ๐Ÿ˜„
 
mkenya gani asiyejua spelling za kibera eti kibras...mswahili tu huyo anaunga unga tu mitandaoni!
 
Nimejua sio Mkenya na kuna kasoro pale aliposifia mabasi ya mwendo kasi, jameni hayo mabasi yanawatesa Watanzania kupita maelezo, mimi nimeyatumia na kukumbana na kero wanazopitia watu kule, kuna wengi wanaomba bora daladala ziruhusiwe kurudi.
Yaani unalisubiri kwenye stendi hadi kilio, na likija limejaa mpaka milango imebana, kuna hata siku nililipia ila ikabidi nitoke nje ya jengo la stendi na kutafuta usafiri wa aina nyingine.
 
Yaani unalisubiri kwenye stendi hadi kilio, na likija limejaa mpaka milango imebana, kuna hata siku nililipia ila ikabidi nitoke nje ya jengo la stendi na kutafuta usafiri mwingine.
isitoshe pia jamaa wanasimama ndani ya hayo mabasi na kunukishana makwapa balaa
 
Hahahahaha, huu ndio usafiri wa kisasa duniani kote wanasimama, hakuna usafiri wa mijini duniani ambapo watu hawasimamishi, iwe metro, light train ama mabasi, miji yote mikubwa iliyoendelea, kama umefika Paris, Tokyo, NY, London au Cape Town.

Kuhusu matatizo ya kuchelewa na kujaza sana, hiyo ni miongoni mwa changamoto zinazotokana na uchache wa idadi ya mabasi na uzembe wa kampuni la UDART lililopewa kandarasi ya kusafirisha watu, kama ambavyo Fast jet ameshindwa kutoa Huduma na amefutiwa kibali na baadhi yenu mnalalamika eti serikali inaogopa ushindani, hata UDART siku zake zinahesabika.

Pamoja na changamoto hizo, bado BRT is the best civilized means of public transport in the world not only in Africa, mtanzania anayelalamika ni out of frustration, lakini hakuna anayetaka kusikia kadhia ya daladala/matatu, usafiri usiofuata sheria wa standards, kila mtu anafanya atakavyo, poleni sana majirani kwa kuteseka na usafiri wa matatu, tunajua mnatamani sana BRT, ipo siku mtapata msijali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejua sio Mkenya na kuna kasoro pale aliposifia mabasi ya mwendo kasi, jameni hayo mabasi yanawatesa Watanzania kupita maelezo, mimi nimeyatumia na kukumbana na kero wanazopitia watu kule, kuna wengi wanaomba bora daladala ziruhusiwe kurudi.
Yaani unalisubiri kwenye stendi hadi kilio, na likija limejaa mpaka milango imebana, kuna hata siku nililipia ila ikabidi nitoke nje ya jengo la stendi na kutafuta usafiri wa aina nyingine.
Endelea Kusoma Magazeti na Jf ukiota umepanda BRT
Hahaha
 
Nimejua sio Mkenya na kuna kasoro pale aliposifia mabasi ya mwendo kasi, jameni hayo mabasi yanawatesa Watanzania kupita maelezo, mimi nimeyatumia na kukumbana na kero wanazopitia watu kule, kuna wengi wanaomba bora daladala ziruhusiwe kurudi.
Yaani unalisubiri kwenye stendi hadi kilio, na likija limejaa mpaka milango imebana, kuna hata siku nililipia ila ikabidi nitoke nje ya jengo la stendi na kutafuta usafiri wa aina nyingine.

Ulikuwa unaelekea wapi???
 
huo ni uongo. nipo Dar tangu last wikend, sijaona kitu unachoongea.
 
Umekwenda kipindi cha Xmas wakati mji umefulia, nenda Jan kati wakati watu wamerejea mishe.
Tena naweza nikakuelekeza wapi uanzie maana Dar napajua sana kuzidi wengi wenu humu.
Nikirudi nitapiga mapicha na kuyaleta humu muone watu wanavyoteseka kisa ukosefu wa mabasi ya kutosha.
Wanajazana stendi, likija inakua vuta nikuvute, halafu milango lazima ifunge, hivyo inabidi msukumane humo ndani muachie nafasi mlangoni, midereva yenyewe imenuna kwa uchovu na ukosefu wa hela, hauwezi kumuuliza kitu.
Madubwasha ya kusoma tiketi ili ikuachie uingie au kutoka stendi haifanyi kazi siku hizi, kuna jamaa wamewekwa hapo kazi yao kukagua hizo tiketi, jamaa wenyewe wachovu huwa hata hawashughulki, unapita tu.
Yaani awali wakati hayo mabasi yanaanza, yalikua nafuu hata kuzidi taxi, nilikua natoka hotelini na kufika mjini ndani ya muda mfupi, lakini kama ilivyo kwa Mswahili, huwa mtihani sana kutunza na kudumisha chema.
 
Ni kweli kuna changamoto za uendeshaji huu mradi. Serikali imejenga miundombinu na kukabidhi mradi kwa mkandarasi ili kuendesha(PPP), tayari serikali imeshampa Warning mkandarasi ambaye ni UDART ajirejebishe kabla ya rungu alilopigwa Fastjet alijatua kichwani mwake, lakini pamoja na hayo yote bado BRT ni bora kuliko daladala, bado unafika mapema, usalama ni mzuri, hakuna wizi ndani, magari wanayotumia ni mazuri, mzungungo wa hewa ndani ni mzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom