Isaac Ndodi: Umaarufu Gani Huu?

Tatizo ni umaarufu wake ama traffic jam ya muda?

Vyote viwili ni tatizo!
Umaarufu wake unakusanya washangiliaji wake wengi, ambapo wanavuruga utaratibu na mienendo ya magari.
Kama hujafika Ars, naapenda nikufahamishe kwamba barabara kuu za hapa hazizidi 4, kwahiyo hakuna pa kukimbilia.
Hope you are happy with my answer!
Karibu.
 
Hizo zote ni ishara za jamii iliyokata tamaa

Yawezekana kweli?Hawa watu wamekataje tamaa, wakati ni watu na mausafiri yao, masuti ya kifisadi na vitambi vya hatari ndo waliokusanyiika uwanja wa ndege kumsubiri huyu mtu?!Ni watu na maofisi yao ambapo ndo matajiri wa hapa mjini ati!Ebu niwekeni sawa hapa!
 
Niliona kipindi chake star Tv janakinarushwa live kutoka arusha.nadhani atarusha live mpaka semina iishe.
Hayo mengine kama ni tapeli wa kiganga ,au kama ni mwijilisti wa uongo mie sijui kwa vile sina ushahidi na sina haki ya kumhukumu.

Mbarikiwe na Bwana!
 
Guyz..acheni kuponda vitu msivyokuwa na uhakika navyo, jamaa kauliza swali zuri afahamishwe kuhusu Dk. Ndodi, lakini hapa naona watu wanajibu lakini kwa hisia tu bila kujua ukweli, chuki binafsi. Mimi sijatumia dawa zake, ila wapo watu wengi wametumia dawa zake na zimewatibu na wanashuhudia hilo, dawa zake nyingi anatumia mchanganyiko wa matunda mbalimbali. Huo umaarufu unaouona na kwa sababu amekubalika sio kwa sababu ya kujua kuongea bali kwa tiba zake mbadala ambazo zimeponya wengi. Yeye haombei watu kama wengine wanavopotosha humu ndani, wala hafanyi miujiza kama wengine wanavosema, yeye ni dokta tu wa kawaida sema pia ni mchungaji wa makanisa ya kisabato, lakini safari zake hizo sio za huduma ya kichungaji. Hope wanaotaka kujua wameanza kupata mwanga, kwa wale wenye data zaidi watujuze zaidi.
 
sio rahisi kujua ukweli, kwa sababu ya imani yako, siku zote FAITH ikiwa kubwa basi THINKING inakuwa ZERO,
KAKOBE ANAKWAMBIA WANAWAKE WASIJIPAMBE NA MAMBO YA DHAHABU NA MAWIGI NI MAMBO YA KIJINI HIVYO WENYE DHAHABU WAZISALIMISHE KANISANI, NA KWELI WENYE IMANI ZAO WALIFANYA HIVYO, KWA UPANDE WA PILI LWAKATALE ANAKWAMBIA ANAHUBIRI INJILI YA KITAJIRI ANAKWAMBIA KAMA UNAWIGI AU DHAHABU WE VAA TU SASA BIBLIA NI MOJA NA KWA SABABU WATU WANAIMANI BAC THINKING HAKUNA,
KABOBE ANAVUNA KWA MASIKINI, LWAKATALE ANACHANJA KWA MATAJIRI
 
Lakini kituko, mi nimetazama na nimesikiliza sana maongezi yake, anatumia vitu vya kawaida kama machungwa, kitunguu swaumu etc, shida inakuja wapi kama watu wanapona kweli?
 
Lakini kituko, mi nimetazama na nimesikiliza sana maongezi yake, anatumia vitu vya kawaida kama machungwa, kitunguu swaumu etc, shida inakuja wapi kama watu wanapona kweli?

Lakini wote tunajua machungwa ni dawa na pia ni tunda ,kitunguu ni kiungo na pia ni dawa si bora yeye anatibu kwa kutumia njia mbadala
 
Lakini kituko, mi nimetazama na nimesikiliza sana maongezi yake, anatumia vitu vya kawaida kama machungwa, kitunguu swaumu etc, shida inakuja wapi kama watu wanapona kweli?
hata mimi ni mtaalam sana wa haya madawa ya machungwa,vitunguu na kazalika kazalika, lakini usini pm kwa sasa, nipo likizo, nikimaliza likizo nitawataarifu.
 
Lakini wote tunajua machungwa ni dawa na pia ni tunda ,kitunguu ni kiungo na pia ni dawa si bora yeye anatibu kwa kutumia njia mbadala

I think its high time we went for the altenative medication, maana madawa haya ya madukani yana side effects nyingi mno ambazo, kwa bahati mbaya hatuzijui.

Isaac ndodi, japo mi si wakala wake anakuelekeza jinsi ya kutumia hivi vitu vya asilia, na more interesting hakupi yeye, anakwambia ukavinunue popote...so unajitibu kwa kitu ulicho na uhakika nacho...
I see it as a revolutional treatment!
 
hata mimi ni mtaalam sana wa haya madawa ya machungwa,vitunguu na kazalika kazalika, lakini usini pm kwa sasa, nipo likizo, nikimaliza likizo nitawataarifu.

KLOROKWINI..
nASIKITIKA kwamba jina lako ni dawa iliyopitwa na wakati.!lol
Lakini jina lako ni mfano halisi wa effects za dawa za kisasa, ambapo zinafikia wakati zinaekspaya, unlike tiba asilia...
Wewe rafiki yangu bora ujiite MZIZIMKAVU orijino!...huh!
 
Wajameni, tujifunze kuwa tuna appreciate pale mtu anapotoa huduma zenye faida kwa jamii, kama wewe unaona huyu ndugu hana msaada kwako hilo ni juu yako lakini kwa baadhi ni msaada mkubwa
 
Kwa hiyo unaona mchango wake katika taifa ulivo mkubwa? Wangapi wanafundisha watanzania elimu kama hiyo ili waepuke hatari ya sumu?.Kwa hiyo ana haki ya kuwa celeb na kuwavuta watu wengi na hayo mapokezi anastahili,Sababu amefanya kitu kinachoonekana kwenye jamii,Mtu anayempinga ni bora atupe na ushahidi wa kukosoa kile anafanya sio maneno ya fitina na wivu.
Mitanzania bwana,ndivyo tulivyo.!
 
Wajameni, tujifunze kuwa tuna appreciate pale mtu anapotoa huduma zenye faida kwa jamii, kama wewe unaona huyu ndugu hana msaada kwako hilo ni juu yako lakini kwa baadhi ni msaada mkubwa

Hongera kwa kuwa na mawazo ya kimaendeleo,tukiwa na watu kumi kama wewe Tanzania tutaendelea
 
Huku Dar mbona mtu wa kawaida tu na ofisi zake zipo Magomeni watu tunamchukulia kama mganga njaa tu.
 
Wewe ndio unanifurahisha kweli. Hivi wewe unavyodhani imani ni mpaka iwe ya kikristo au kiislamu? Kwa taarifa yako hata wewe hapo unaishi kwa imani ila sijui imani gani.Na naweza kusema wewe ndio una ziro thinking kwa vile hata hujitambui kama unaishi kwa imani.
Hivi unadhani hao wanasayansi wakubwa akina Newton kama wasingekuwa na imani na sayansi yao wangegundua? au hao waliogundua ndege?
Pole sana. Ndio maana hata nchi imeweka kipaumbele kuheshimu imani za wengine.
Kaa na imani yako na uwaache wenzio waamini imani zao ilimradi hazivunji taratibu za nchi.
Kama watu wanaona wanapona wakienda kwa Ndodi waache,aftaloo huwezi kuwasaidia kwenye magonjwa yao.
 
deh deh deh, hili jina nimelipia haki miliki, nikijiita jina la kiswahili kama mzizimkavu nitakosa mchumba katika hili dunia la ubaguzi, tukirudi kwenye mada, jamaa akihitaji tenda ya kupelekewa machungwa nijulishe nina shamba la urisi la michungwa.
 
nimekuelewa
 
Heeeee

Hivi hukupata kusikia jinsi yule mganga wa jadi aliyekuwa akiitwa...sijui LIMBE naninani huko, alivyomchukua mtoto bomba NORA ,yule mwIGIZAJI wa runinga?

Mbona pia kuna rafiki yangu humu jamvini anajiita NG'WANA MADASO. ana mchumba bomba mbaya!...lol!
 
hata mie sasa itabidi nianze kufatilia kwa kina matibabu yake ..
kuna madawa ya tunakunywa baada ya muda yanapigwa marufuku eti hayana TBS ni lini chungwa lako mwenyewe uambiwe halina TBS
 
Jamani waacheni kina Ndodi, Kakobe, Lwakatale et al wagange njaa, mnataka kujifanya hamjui kwamba hata huko RC, Lutheran, Moravian, et al wanaganga njaa????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…