FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,789
- 5,401
Heeeee
Hivi hukupata kusikia jinsi yule mganga wa jadi aliyekuwa akiitwa...sijui LIMBE naninani huko, alivyomchukua mtoto bomba NORA ,yule mwIGIZAJI wa runinga?
Mbona pia kuna rafiki yangu humu jamvini anajiita NG'WANA MADASO. ana mchumba bomba mbaya!...lol!
Thank you very much my dear,ur welcomenimekuelewa
hahaha yaani leo klorokwini kanichekesha kila post nayopita inaniacha hoi PJ
Huku Dar mbona mtu wa kawaida tu na ofisi zake zipo Magomeni watu tunamchukulia kama mganga njaa tu.
mi sisemi kitu. I am watching!
Thank you very much my dear,ur welcome
pole labda umemshitukia wewe usiyeumwa. Ila waoumwa anawafaa.
iveni mi amu wochingi yu mai dia.
pj tuwasiliane bwana tuko hapa watoto wa mujini wanaita A Tau wote tuanzishe kaclabu cheti na sisi kama kile chawote na zero p
I think its high time we went for the altenative medication, maana madawa haya ya madukani yana side effects nyingi mno ambazo, kwa bahati mbaya hatuzijui.
Isaac ndodi, japo mi si wakala wake anakuelekeza jinsi ya kutumia hivi vitu vya asilia, na more interesting hakupi yeye, anakwambia ukavinunue popote...so unajitibu kwa kitu ulicho na uhakika nacho...
I see it as a revolutional treatment!
Naona wengi wamemshambulia sana huyu Dr. Isac Ndodi. Binafsi sijapata huduma za tiba zake ila naamini kuna watu ambao wao binafsi au ndugu na marafiki/majirani wamehudumiwa na huyu binadamu. Ningependa wajitokeze hadharani watoe shuhuda ili tuone matokeo makubwa ya hizi dawa.
Ninamsikiliza sana katika kipindi chake Star TV, ninamkubali kwa vipindi vyake hasa kuhusu vyakula tunavyokula na madhara ya baadhi yake na nini tufanye tuachane na magonjwa ya kujitakia. Yote yale anayosema ni sawa kabisa theoretically, practically ni kwa kutumia dawa zake, ambazo tunataka shuhuda hapa.
Tusipende kushambulia kwa lugha kali bila kufanya uchambuzi wa kina. Hebu imagine dawa za kichina zilivyotapakaa na hujui wala mtengenezaji na wala kama kampuni hizo ziko duniani lakini bado tunanunua wakati kule kwao hawazitumii. Ni lini basi tutakubali kuwa huwa pia Tanzania kuna vipaji na wavumbuzi na hao basi wanatakiwa wasaidiwe au kuenziwa ili tuwe na patent rights zetu???
Kuna rafiki yangu mjukuu wake alikuwa anasumbuliwa na malaria sana na alipata dawa kwa Dr. Ndodi magomeni(dose ni a bit expensive) na alipona kabisa na walishasahau kama mtoto alikuwa ni msumbufu. Walikiuwa hawakosi hospital kwa dawa na drips za malaria. Let us praise our traditions, traditional medicine kama zitakuwa administered inavyotakiwa ni the best.
Afya yako utailinda kwa aina ya chakula unachokula na wala hutahitaji kumtembelea Dr. Ndodi. Imagine wala nyama za kuchoma sinia na bia, ndizi rost on top, chips, kuku broilers na mifupa unatafuna wakati dawa zote za makuzi yake huwa kwenye mifupa, you name all food related toxic in our bodies!!!
Bottom line afadhali Ndodi amepokelewa kwa vifijo A town kuliko mapokezi ya kifisadi Monduli na Shinyanga jimbo la cheupe ambaye mikataba yake mibovu ime-undermine huduma za serikali hasa kwa huduma za jamii(imagine shule hazina huduma na hospital hazina madawa na vitendea kazi na mishahara mibovu). Hayo madola yange top up mishahara na huduma. All the best comrade Ndodi.
Guyz..acheni kuponda vitu msivyokuwa na uhakika navyo, jamaa kauliza swali zuri afahamishwe kuhusu Dk. Ndodi, lakini hapa naona watu wanajibu lakini kwa hisia tu bila kujua ukweli, chuki binafsi. Mimi sijatumia dawa zake, ila wapo watu wengi wametumia dawa zake na zimewatibu na wanashuhudia hilo, dawa zake nyingi anatumia mchanganyiko wa matunda mbalimbali. Huo umaarufu unaouona na kwa sababu amekubalika sio kwa sababu ya kujua kuongea bali kwa tiba zake mbadala ambazo zimeponya wengi. Yeye haombei watu kama wengine wanavopotosha humu ndani, wala hafanyi miujiza kama wengine wanavosema, yeye ni dokta tu wa kawaida sema pia ni mchungaji wa makanisa ya kisabato, lakini safari zake hizo sio za huduma ya kichungaji. Hope wanaotaka kujua wameanza kupata mwanga, kwa wale wenye data zaidi watujuze zaidi.
Guyz..acheni kuponda vitu msivyokuwa na uhakika navyo, jamaa kauliza swali zuri afahamishwe kuhusu Dk. Ndodi, lakini hapa naona watu wanajibu lakini kwa hisia tu bila kujua ukweli, chuki binafsi. Mimi sijatumia dawa zake, ila wapo watu wengi wametumia dawa zake na zimewatibu na wanashuhudia hilo, dawa zake nyingi anatumia mchanganyiko wa matunda mbalimbali. Huo umaarufu unaouona na kwa sababu amekubalika sio kwa sababu ya kujua kuongea bali kwa tiba zake mbadala ambazo zimeponya wengi. Yeye haombei watu kama wengine wanavopotosha humu ndani, wala hafanyi miujiza kama wengine wanavosema, yeye ni dokta tu wa kawaida sema pia ni mchungaji wa makanisa ya kisabato, lakini safari zake hizo sio za huduma ya kichungaji. Hope wanaotaka kujua wameanza kupata mwanga, kwa wale wenye data zaidi watujuze zaidi.
isak ndodi ninamfahamu sana, sijawi kupata tiba kotoka kwake. huyu bana ni muumini wa kanisa la sabato. mimi si msabato bali kama kuna walio wasabato ndani ya JF wanaweza wakaeleza yeye ( ndodi) ni nani. nilimfahamu ndodi huko songea, anachokifanya ndodi si jambo geni kwani hakusomea popote na siyo daktari kwa kuwa na degree ya medicine au daktari kama wale wanaoagua bagamoyo. nijuavyo mimi ndani ya kanisa la sabato wanautaratibu wa kuta elimu juu ya tiba asilia kwa kutumia mimea kutibu au kujenga afya ya mwili. kanisa la sabato lina vitabu vinavyoeleza aina ya mmea , magonjwa yanayoweza kuponywa kwa mmea huo, na hata namna ya kuandaa dawa na dozi yake kwa ugonjwa husika. hivyo vitabu vipo. isak alikuwa akifudisha vipindi vya dini (sabato) pale songea ktk shule za sekondari.wakati huo alikuwa anafundisha bible na si haya ya tiba mubadala. nadhani hapo ndiyo alijifunza kuongea mbele ya watu. lakini anachokifanya sasa ni kutangaza vile vitabu vya tiba vya kisabato, ukienda kwake atakupatia hicho kitabu utasoma na wewe utaamua wapi kwa kwenda kupata hiyo aina ya mmea / tunda/mbegu a u hata majani kwaajili ya tiba. kama aina ya ugonjwa huijui isak hawezi kukusaidia na atakwambia hana cha kufanya nawe. yeye hafanyi diagnosis( hafanyi kutambua unaumwa nini) , ukijua unaumwa nini , anaweza kukuongoza kwenye tiba. ninauhakika kama kanisa la sabato litamgundua akifanya diagnosis watamfungia mara moja. faida yake ipo kwenye kutoa huo ushauri wa tiba, na pia anauza hivyo vitabu ambavyo vinatoa mwongozo wa tiba. hata ukienda baadhi ya maduka ya vitabu, utakuta hivyo vitabu vya tiba, na mtunzi siyo isak, ni watu wengine kabisa, yeye amefahamu kupitia kusoma hivyo vitabu. kwa lugha nyingine unaweza kwenda kwa isak na ukanunua kitabu chako ukajisomea namna ya kulinda afya yako.
umaarufu wa isak hautokani na uelewa mdogo wa watanzania bali unatokana na watu kujali afya zao. mtu akisema isak anazungumza juu ya machungwa na akadai mbona sote tunajua juu ya machungwa, tukumbuke hata tunapokwenda hosptali tunakuwa hatujui tunaumwa nini, hapo tunaambiwa chanzo cha ugonjwa na tiba , ambavyo utakuta ni vya kawaida kabisa. tuwaache wanaoumwa wahoji uwezo wa isak, lakini sisi wenye afya hatumhitaji isak mpaka tutakapo umwa