Isaac Ndodi.

Wana tofauti.
Mganga wa Kienyeji anafanya Traditional Medicine hii husomei ila unaweza kuoteshwa, kurithiswha nk
Mganga wa tiba mbadala anafanya Alternative medicine hii lazima usomee mfano Chinise medicine, Indian medicine, homeopathy, Ayuved etc

Ndodi sijui amesomea wapi?
 
Ndondi ni mganga wa kienyeji kama walivyo waganga wengine.
 
Jamani mwenye CV ya huyu bwana naomba anisaidie kuibandika hapa JF.
Nasikia ni Daktari, sijui kasomea wapi na amebobea kwenye tiba ya magonjwa yepi?

Huyu jamaa udaktari wake ni kama wa akina JK,Marehemu Remmy Ongala,Prof J nk...hajasoma popote ni ujanja ujanja tu..alianza kazi ya uijilisti kwenye kanisa la Wasabato kule Songea...na alikuwa ni mahiri kufundisha masomo ya afya kama yanavyofundishwa kwenye kanisa la wasabato..baadae akaamia DSM alipoinuka kuwa maarufu sana...mpaka sasa anafanya kazi kama muijilisti katika kanisa la wasabato Kurasini DSM....
 
Akili kumkichwa. Ni tapeli flani anayetumia udhaifu wa nafsi zetu kujitajirisha.
Nakubaliana nawe. Ndodi ni msheenzi na tapeli mkubwa. Anajineemesha kwa fedha za wagonjwa pasipo huruma. Dawa za ndodi huuzwa hadi Sh milioni mbili na wagonjwa wengi tu hawajapona. Utapeli wake upo mdomoni. Mwanaume gani wa kawaida anayeongea kama cherehani!!!!!!!
 
Kwani mganga wa jadi lazima awe mshirikina? Mimi nikigundua mti fulani (pengine unatumika kwenye nchi zingine kutengeneza dawa za kisasa) una uwezo wa kutibu maradhi fulani, je ni vipi utanihusisha na ushirikina? Ukisema Ndodi ni tapeli kwa kuwa una uhakika dawa zake haziponeshi ni sawa lakini si kumuhusisha na ushirikina kwa kuwa tu ni mganga wa jadi. Kuhusu CV yake, nimewahi kumsikia akisema amesoma Marekani katika chuo cha kisabato kinachotoa elimu ya tiba mbadala.
 

dah, sijui amewezaje kupenya na kuziteka kabisa akili za wanawake wengi wa Tz?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…