Katika hali isiyotarajiwa aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam kupitia Chadema Mstahiki Isaya Mwita amebwagwa vibaya sana katika Uchagizi wa Chama hicho Wilayani Kigamboni. Meya huyo anashutumiwa na Wanachadema kwamba alikitelekeza chama hicho tangu aliposhika umeya. Matokeo ya Uchaguzi huo uliofanyika jumamosi tarehe 27/7/2024 yanaonyesha kama ofuatavyo:
Nafasi ya Mwenyekiti, Kamanda Mbaraka Mtitu ameshinda kwa Kura 42 dhidi ya Isaya Mwita (Meya Mstaafu wa Jiji la Dar) aliyepata kura 28.
Nafasi ya Katibu wa Chama Wilaya, Musa Bwashari amepata kura 65 za ndio dhidi ya 7 za hapana.
Nafasi ya Mweka hazina, Kamanda Mohamed Kitenge amepata Kura za ndio 41 dhidi ya kura 31 za Hapana
Nafasi ya Mwenezi Wilaya Kamanda Hamis Ngapunga amepata kura 44 dhidi ya Kamanda Hasan Juma aliyepata kura 27.
Nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Yericko Nyerere ameshinda kwakupata kura 51 dhidi ya Sultan Ibrahim aliyepata kura 19.
Wapiga kura walikuwa 72
Msimamizi wa Uchaguzi alikuwa ni Katibu wa Kanda Mh. Jerry Kerenge