Ndugu, naomba kujulishwa na wale ambao wana utaalamu na mambo ya barabarani haswa hapa kwetu bongo. Mara nyingi ukiwa unasafiri inatokea madereva wanapeana ishara, mfano kwa kuwashiana taa full au kwa mkono kwa maana ya kujulishana hali ya barabara mbeleni kama uwepo wa wazee wa torch na vitu kama hivyo. Swali langu ni kama hizi alama ni uniform. Au kwa maneno mengine, ni kwamba unajuaje kuwa alama hii ni ya tahadhari fulani? Naamini swali langu linaeleweka.