Ishara za mwili kupungukiwa maji

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2011
Posts
3,211
Reaction score
993

IJUWE KIU


Unasubiri KIU ndipo unywe maji? Na je kiu ni?:



NAMNA MPYA YA KUITAMBUA KIU:


Ikiwa 'mdomo uliokauka au kiu' siyo kiashiria kikuu cha mwili kuhitaji maji, ni vipi hasa viashiria vya mwanzo na sahihi vya mwili kupungukiwa maji?.


kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj na maoni ya kisayansi, kuna mafungu ya aina mbili tofauti ya hisia, yanayotoa ishara ya kiu ya eneo moja au mwili mzima.


Mafungu haya yanajumuisha; Maono ya jumla ya kimawazo na zile ishara kubwa zaidi za dharura za sehemu moja au za jumla za kupungukiwa maji.


Ishara za kimawazo zinajumuisha baadhi ya viashiria vifuatavyo ambavyo vimepewa majina kama 'matatizo ya kisaikolojia'. Ishara za mwanzo za mwili kuanza kupungukiwa maji:




  • Kujisikia umechoka (uchovu): Sababu maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu.

  • Hasira bila sababu: maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu cha ubongo, mwili unapopungukiwa maji, ubongo unakosa nguvu kushughurika na hali mpya, mawazo na vitendo. Hasira inatokea kuwa ndiyo namna ya ubongo kujibu hali mpya zinazohitaji majibu, "Siwezi kufanya jambo hili”, sababu hauna nguvu za kutosha.

  • Woga na aibu: dr.Batmanghelidj amepata barua ya ushuhuda toka kwa mtu aliyekuwa akisumbuliwa na woga na aibu (agoraphobic) aliyejitibu kwa tiba ya maji.

  • Kujisikia umetengwa na usiyemkamilifu - huwezi kutimiza yale uyatakayo.

  • Kujisikia unaonewa.

  • Kichwa kizito uamkapo asubuhi: hakuna nguvu za kutosha kufungua mifumo ya mishipa ya fahamu.

  • Kukosa mantiki au sababu za maana unapoongea au kujibu na kukosa uvumilivu.

  • Kukosa usikivu na ufuatiriaji hasa kwa watoto na vijana; 'Uwezo wa akili wa mwanafunzi unapungua wakati kiasi cha maji mwilini kinakuwa chini ya wastani, kushuka kwa asilimia 2 tu ya uzito wa mwili sababu ya upungufu wa maji, kunapelekea matatizo ya usikivu na ufuatiriaji na uwezo mdogo wa kumbukumbu miongoni mwa wanafunzi'.

  • Kukosa usingizi mororo na kuota ndoto za kuogofya (nightmares).
  • Pumzi fupi, hatua za mwanzo za pumu, inashauriwa pia kunywa maji kabla ya michezo au mazoezi.

  • Utegemezi kwa vinywaji vya viwandani na vilevi (conditional reflex).
  • Kukata tamaa na hasira, ubongo hauna nguvu za kutosha kushughurika na matatizo mapya na unataka kuachana na mada (wacha lipite bwana, liwalo na liwe), ndiyo maana wahenga walipomwona mtu ana hasira, watampa glasi ya maji hata kiasi kidogo cha chumvi.


Utakuwa umegunduwa sasa ni kiasi gani mwili wako umejihangaisha wenyewe kwa kujibana katika matumizi ya maji kiasi cha kukusababishia moja au yote kati ya matatizo yaliyorodheshwa hapo juu ambayo yangeondoka tu kirahisi kwa wewe kuamua kunywa maji kwa mtindo wa kutosubiri kiu ili kunywa maji au kusubiri kuona ishara za kupungukiwa maji.



Kabla upungufu wa maji (dehydration) haujakudhuru kufikia hatua ya umaututi, Mwili utazitoa moja kati ya ishara hizi za pili kubwa na za dharura (emergency calls) za uhitaji wa maji mwilini zifuatazo; vidonda vya tumbo, tumbo kunyonga, kiungulia, mafuta yaliyozidi, kansa ya utumbo mdogo, kukinaishwa na chakula, na ernia.


Ishara zingine ni; Kansa, kisukari, kifua kikuu (TB), shinikizo la damu (BP), mfadhaiko (stress), matatizo ya moyo na kuzimia, magonjwa ya tumbo, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya Ini, pumu (Asthima), mzio (Allergy), chunusi, homa, kupunguwa nguvu na kinga ya mwili, matatizo ya kina mama, magonjwa mengine ni pamoja na homa ya uti wa mgongo, kansa ya kizazi, kikohozi, kuharisha, kikundu, nyongo, matatizo ya tumbo, kupungua uzito, upungufu wa damu (anaemia), vichomi, utipwatipwa na uzito kupita kiasi, kuzeeka mapema, na ishara nyingine nyingi.
 
Ahsante! Tafiti zinaonyesha Waafrika (hususani Wanawake) hawanywi maji, Wanaume hunywa maji mengi zaidi ya Wanawake kutokana na aina ya kazi wanazofanya. Inashauriwa kunywa, si chini ya glasi nane (lita mbili) za maji kila siku, kwani ndio kiasi mwili unachohitaji kila siku. Kunywa bia, soda, juisi n.k si mbadala wa maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…