Ishara za viungo vyangu

Ishara za viungo vyangu

clearmind

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
813
Reaction score
1,913
Wanajamii wa jukwaa hili, naombeni wenye utaalam mnipe muongozo katika hili. Mwaka juzi mwezi wa sita nilikuwa niki-experience kitu cha tofauti sana. Ilikuwa inatokea tu automatically ninakunja vidole viwili yaani dole gumba na kidole kinachofuatia baada ya dole gumba halafu vinabaki vidole vitatu vimesimama.

Tukio hili lilikuwa linatokea mara kwa mara kwa mikono yote miwili hadi siku ambayo mdogo wangu alifariki tukio hilo likakoma. Imekuwa sasa ni kawaida. Kila panapokuwepo na tukio lolote la kupoteza, ninakuwa na dalili hizi mapema. Ikishatokea, ni lazima nitapitia kwenye tukio lolote la kupoteza.

Jambo jingine ni mwili wote, kuna wakati usingizi unakuja ghafla na hudumu ndani ya dakika moja au mbili. Ikitokea hivi, safari yangu yoyote ile hugairishwa. Nini kipo nyuma ya dalili hizi? Msaada na maono yako ni muhimu sana. Natanguliza shukrani.
 
Pole sana ushajichunguza alama ama signal za mwili wako?
Sijakuelewa hapa mkuu. Ila mara nyingi hizi hutokea tu automatically. Yaani naweza kuwa hata kwenye mazungumzo, nashtukia tu nimekunja vidole bila hata kujua. Ikitokea hivyo basi najawa na hofu sana.
 
Sijakuelewa hapa mkuu. Ila mara nyingi hizi hutokea tu automatically. Yaani naweza kuwa hata kwenye mazungumzo, nashtukia tu nimekunja vidole bila hata kujua. Ikitokea hivyo basi najawa na hofu sana.
Namana mwili wa binadam hua unishara mfano mm ukiwasha mwili ubavu w kulia najua kuna tatizo litatokea,ukiwa mkono was kushoto pesa Zita nitoka balaa ivyo muhim kujua signal kama izo itakusaidia.
 
Back
Top Bottom