Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kuna baadhi ya watu huwa wanakubalika sana, kwenye mitaa wanayoishi; kutokana na kujichanganya kwao au kushiriki kwenye matukio ya hapa na pale yanayohusu mitaa waliopo.
Ila kuna wengine, wanajulikana kama vipanga; hawajulikani kama mtaani wapo ama hawapo; kutokana na kila mmoja kuishi kivyake vyake; hakuna kusemeshana au kushiriki tukio lolote linalohusu mtaa. Mtu akiingia kwake, anafunga geti lake na hataki mawasiliano na mtu wa nje hata jirani.
Kwa uoefu wa hapa na pale; nimekuja kugundua, maisha ya kijamii (kijamaa) yana umuhimu sana, hasa maeneo tulipojenga makazi (nyumba) zetu za kuishi.
Sehemu ulipojenga nyumba yako na kuishi, ni muhimu kupafanya pawe na furaha, na ili furaha iwe kubwa zaidi itakulazimu kuishi kijamaa.
Na waliofanikisha hili, watakuja na ushuhuda wa namna wanavyofurahia maisha ya hapo mtaani.
Majirani ndio wanakuwa ndugu zako wa karibu.
Inawezekana miaka yote huwa unatamani, uchanganyikane na jamii ya mtaani kwako, ila unakosa pa kuanzia.
Unaweza kubuni namna ya kuwakutanisha pamoja, mfano; kwenye matukio ya mwisho wa mwaka; unaweza ukawashawishi watoe mchango kidogo ili msherehekee kwa pamoja, kwa kuchinja mifugo n.k Na katika makutano yenu, mkaazimia baadhi ya vitu vitakavyokuwa na faida maishani mwenu.
Naamini; wote mtafurahia hiyo kukutana kwenu, na mtajiuliza siku zote mlikuwa wapi kufanya tukio la namna hiyo?