Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,912
- 12,904
Hello jamiiforums
Hakuna ambaye hajawahi kupokea ugeni,hakuna ambaye hajawahi kuwa mgeni wa mtu,safari zipo iwe kikazi misiba ,sherehe au kuamua kutembelea ndugu zako hususani mwishoni mwa mwaka.
Unaweza ukawa na shughuli fulani mkoani,ama utoke mkoani uje Jiji hili la Dar es salaam,ukawaambia ndugu zako kuwa utakuwa hapo Kwa siku au wiki kadhaa wakaamua kukushauri kuliko ukae lodge na upoteze pesa Bora ukae kwao ,hapo ndipo ishu ya ugeni inapoanzia.
Leo tuangalie mambo ya kuzingatia unapokuwa ugenini ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa mapema
Hii itawasaidia wenyeji kukuandalia mazingira mazuri ya chumba cha kulala pamoja na settings zingine.kama mtakuwa wawili mke na mume nayo ni vizuri mkasema wazi mko wangapi hii itampa mwenyeji wako kupangilia budgets zake .
Uwapo ugenini sasa hata kama ni Kwa Kaka,dada au mjomba,chukua tahadhari hizi
1.Jiongeze
Hata kama wana uwezo kukuzidi wewe usiangalie hilo badala yake ,toa mchango wa pesa,hata kama huyo Shemeji atakataa, utasikia shemu kuwa na amani hapa ni kwako,wewe si mpita njia,usikubali maneno hayo,toa sababu stahiki ,atapokea tu.
2.Punguza kuwa huru sana
Hata kama joto la Dar linakusumbua ,jikaze acha kuvua shati hata ,au kuvaa nguo zisizo na maadili ukiulizwa eti joto linakusumbua.
3.Muda wa chakula kuwa makini
Familia zetu za Kiswahili zina hila sana, unaweza kusema shemu au aunty ananipenda kumbe unachorwa tu,muda wa chakula ni vyema Kula Kwa kiasi hata kama una uwezo wa Kula kilo nzima peke yako.
4.Ukiombwa usaidie kazi hakikisha unaiweza
Siyo unakurupuka kutengeneza vitu vya umeme ikiwa huna utaalamu navyo utapigwa shot uaibike,nilishawahi kuchezea dishi la watu (yale ya zamani ya wavu) nikajikuta nimepoteza Chanel zote hata zilizokuwa zinaonesha.pia usisaidie homework ikiwa huna uhakika kuwa muwazi kitu fulani huwezi
5.Punguza ulafi uwapo ugenini
Muuza ice cream kapita ,mama anaamua kuwanunulia wanaye,kisha anakujaribu shemu na wewe chukua,mara na wewe na ndevu zako unachukua mnaanza kufyonza wote wewe ,Shemeji yako ,khaaaaa!
6.Usije kukubali ukafuliwa nguo zako.
Huyo aunty yako au Shemeji yako anaweza kuwa na roho nzuri tu, washing machine si ipo? akataka akufulie nguo zako,usikubali badala yake omba vitendea kazi ufue mwenyewe.itajenga taswira nzuri hata Kwa Kaka au uncle wako.
7.Usipende kukaa kwenye TV ya wenyewe muda mrefu.
Mechi za UEFA zinachezwa usiku wa saa tano na wewe umeng'ang'ania lazima Barcelona yako uione hutaki kusimuliwa ,huu ni ujinga vitu vingine vikupite ,si lazima haswa uwapo ugenini. Lazima uwe na kamba mguuni.
8.Acha kuleta marafiki na washikaji zako hapo ulipokaribishwa
Mmeonana na wana unasmua kuwaonesha ulipofikia nao walivyokosa nishai wanakula kisha mnaitawala sebule ya wenyeji Kwa kukumbushana stori zenu za miaka mingi huku mkiongea Kwa nguvu,kucheka na kugonga mikono. Siyo vizuri.
9.Punguza tamaa uwapo ugenini,
Siyo kuona kitu kizuri iwe simu,jiko , friji,Gari limepaki tu haliendeshwi na vingine vingi halafu unaropoka hiki mniuzie,tena unaonesha kumaanisha kabisa uuziwe.hata kama unaona kimekaa tu hakina kazi wewe jishikilie vunga kuna watu hawana hulka za kuuza vitu (Mimi mwenyewe smartphone ya Kwanza kuitumia ipo kabatini tu japo haiwaki
10.Punguza kuleta vyakula binafsi ambavyo hutaki familia ya pale wale
Yaani umenunua kidali cha kuku umekifunga kwenye kipercel na kupitiliza hadi chumbani ukalie huko,hata kama ukigundua wenye nyumba siyo shida zao,lakini siyo utaratibu mzuri kula na maliza huko huko mtaani
11.Punguza kunywa pombe na sigara.
Hata kama una addition na vitu hivi jaribu kupunguza ukiwa ugenini hata kama na wao ni walevi kupindukia lakini wewe jitahidi kuwa timamu muda wote ikiwezekana usinywe tu maana yake pombe haionjwi.
12.Usilete demu au mwanamke mahali ulipo
Hata Kwa kuibia,au wenyewe wakakupa hiyo ruhusa lakini wewe usifanye hivyo,jitahidi kumaliza shida zako huko huko na kama mmesafiri wewe na mkeo mko hapo ugenini,punguzeni kuwa chumbani muda wote ikiwa wenyeji wapo sebuleni yaani masaa manne tena mchana mko tu room mwenyeji anashindwa kujua mnaumwa au la.pia Kwa wanawake wenye makelele kwenye tendo jitahidi kuugua kimya kimya
13.Mabadiliko yeyote kiafya kwenye mwili wako wataarifu wenyeji haraka sana
Hii itakusaidia Sana,kila sehemu ina milipuko yake ya magonjwa.unapokaa kimya kisa aibu,watanichukuliaje,unazidi kujiweka katika hatari.
14.Usikosoe sana, toa ushauri ukiombwa.
Hata kama sebule haina muonekano au mpangilio mzuri we kaa kimya,usafiri wanaotumia siyo mzuri piga kimya ,TV yao ya chogo wakati unajua wanamudu kununua flat TV we kaa kimya .
15. Siku za kukaa hapo zikiisha aga huku ukiwashukuru wenyeji wako, hata kama kuna maudhi yalijitokeza wewe shukuru na uwakaribishe kwako hata Kwa kuzuga,ikiwa umepiga mshindo waweza kuwabariki kidogo wenyeji wako hata kama unajua wanajiweza.
Chukua yanayokufaa ,ongezea yanayotakiwa
Jumamosi njema .