Ishi kwa Amani Moyoni mwako kwa kuanza na kuwasamehe waliokukosea

Ishi kwa Amani Moyoni mwako kwa kuanza na kuwasamehe waliokukosea

Princep

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2016
Posts
584
Reaction score
839
Dunia nzima hakuna ambaye ni mkamilifu asilimia 100% kwa maana hiyo kila mtu kwa nafasi yake anafanya makosa kwa bahati mbaya au kukusudia

Hivyo usitake kuwa mkamilifu kwa kuwa haiwezekani hata Kidogo

Kwa maana hiyo mtu yeyote ambaye anajitambua anajua kwamba kila mtu anayekutana nae kwenye maisha ana sifa kubwa mbili:

1. Uimara/Ubora wake (Their Strengths)

Hajazaliwa kwa bahati mbaya kwa kuwa ndani umebeba hadhina ya vipawa kwa maana una uwezo wa kipekee, ubora wa mtu ndio humfanya kuongeza thamani ya maisha yake kwa maana thamani yako

2. Madhaifu yake (Their Weakness)

Hupaswi kuwa na dharau na kuwasema wengine vibaya kisa tu ana madhaifu fulani Hata wewe una madhaifu yako kwa maana hiyo wewe unapaswa kuwa mtu wa kuchukuliana na watu wengine

Je unataka kuwa na Amani ya moyo na mwenye furaha?

Najua umesema ndio hahahaha!

Usijali kabisa ili uwe na amani wa moyo wako na mwenye furaha

Basi unapaswa kuwa mtu ambaye unasamehe watu wengine pasipo kujali:

1. Amekukosea kwa bahati mbaya

2. Amekukosea kwa makusudi

Wewe samehe sababu ukisamehe watu wengine inakusaidia kuondoa chuki, kisasi pamoja na kinyongo moyoni

Unaposamahe watu wengine ni faida kwako na kwa watu wengine....

..... kwa sababu utakuwa na Amani ya moyo huku una mahusiano mazuri na watu wengine

Je, wewe una tabia ya kusamehe watu wengine?

Kuwa mtu wa kusamehe watu wengine

Usiwe na dhana kwamba ukisamehe watu wengine wewe ni dhaifu sio kweli

Kwa maana kusamehe watu wengine ni ishara kuwa umepevuka na unajitambua wewe ni nani

Chukua nafasi hii leo kusamehe watu wengine kwenye maisha yako ili kuachilia mzigo mzito ndani ya moyo wako

Samehe kisha endelea na maisha yako

Ukisamehe Sio kwamba ni lazima uendelee ukaribu na watu wengine kwa sababu unasamehe kwa ustawi wako

Samehe walikukosa kama unataka kuwa na Amani na furaha ndani ya moyo wako

Samehe ili Mungu wa Mbinguni pia akusamehe makosa yako

Samehe kama unataka kuishi na watu wengine vizuri sehemu ambayo upo

Kutoa msamaha kwa walio kukosea pasipo kujali wamekuomba au laasha!

Je umesamehe wote walio kukosea?
 
Kuna Jamaa alimpiga Jamaa fulan wamakamo na Jiwe kwenye uti wa mgongo, Jamaa akapalalaizi kuanzia kiunon kushuka miguun yaan hawezi tembea, hawez lolote lile !!


Matokeo ya tukio hilo

Watoto wa Mzee wakafukuzwa Shule

Mke akazalishwa na Boss wake


Mzee umasikin ukamvaa kwelikweli.



Hii inamaana gan??? Kuna Ubaya MTU anaweza kukutenda, ukaathiri Familia na kizazi, nahata wewe mwenyewe mpaka Kufa..


Ubaya wa aina hiyo kwann uuache ??yaan uusamehe kirahisi rahis??


MTU lazima avune alichopanda na awajibike kwacho.


Ndio sababu, Hata wana Israel walikua Mungu anawambia, Nendeni mkauume wahiti, waamori, muwauwe wao na wake zao, na Watoto, na mifugo yao yaaan kuteketeza.



Sio kwamba nawashauri muwe wa Visasi, kama huwez tulia, ila kama unaweza, nawewe hakikisha ADUI YAKO umempitisha mazingira ya ajabu na mateso kwelikweli.


Mambo mengine ni ya kidunia tu hapa , suluhisho lake pia ni Hapa hapa Duniani.



Nyie hamjiulizi kwann Waisrael daily wanawapa kichapo wapalestina???
 
Ni Sawa lakini Maandiko Matakatifu yanasema; mtu alikikukosea ;

1. Muonye

Akitubu


2. Msamehe


Asipotubu muitie wazee 2-3

Akigoma mkatae.

Kwa hiyo kumsamehe mtu Kuna mchakato.

Halafu mtu umsishinike kuomba msamaha anatakiwa mkosaji aelezwe ukubwa wa kosa , hasara na madhara alosababisha kwa yeye kumkosea mwenzie au wenzie.

Kisha kwa kujitambua kwake au kwa uungwana wake ndipo atapaswa kuomba msamaha.

Msamaha wa shinikizo wala huwa hausaidii.
 
Ili msamaha uweze kuleta maana mkosaji anapaswa ;

1: kukiri kosa au makosa

2. Aoneshe kujutia kufanya makosa

3. Awe na utayari wa kugeuka kwa kuomba toba/msamaha.

4. Aoneshe kutorudia kufanya kosa.
 
Kwa baadhi ya makosa mkosa inabidi awajibike kwanza kwa kufanya compasations for losses or damages alozosababisha there after akiomba msamaha ndipo asamehewe.

Tusitake kulea ujinga kwa watu kukosea wenzao makusudi wakijua kuwa watasamehewa bure au kirahisi.
 
Unafahamu ukimsaheme mtu kijumla bila kusemezana nae ni rahis sana mtu huyo akarudia kukujeruhi moyo wako.

Katika kuzungumza na kuonyana kila mtu atajifunza na kufahamu mambo mengine na kuepuka kukwazana tena.
 
Katika kuzungumza wewe ulokosewa unaweza ukagundua kumbe kosa halikuwa kiasi kikubwa ulochukulia au kuambiwa.

Utafahamu ukweli na vitu vingi sana kupitia mazungumzo.

Tatizo watu hawataki kuulizana wala kuzungumza juu ya mambo.

Wanawekeana mabifu na visasi tu.
 
Kusamehe ni tiba moja nzuri japo ni ngumu sanaaaaa...niamini, I used to be very revengeful..Kuna matukio yalitokea kuanzia August 4, 2021 (Manne) na yote yaliniumiza to the extent..lazwa mpaka hospt..wakicheck pressure iko juu vibaya sana...nikaamua kufanya ibada na kuomba Mungu anipe moyo wa kusamehe..Dude, Msamaha ni muhimu sana..Nilikua siwezi potezea jambo in short nilikua mnoko flani mtata..Nilipojifunza kusamehe..Huenda nika nawiri..Japo sio kazi rahisi na mungu ana ku-reward..nimepata favors za kutosha tu nashukuru Mungu nimeanza 2022 kwa furaha tofauti na miaka yooote tangu nijitambue! Kisasi sio issue..Unaposamehe unapata peace of mind 100% aliyekutendea anabaki kuteseka yeye!
 
Wapiii. Kuna ex wangu flani alisukumwa kwenye ngazi akavunjika miguu yote yuko kwenye wheelchair toka October last year. Wamejaribu kuficha wapi nikaja kutokuwa mwaka kana mwishoni. Nilinyamazaga ila Lila nikipiga magoti na muombea mabaya na kifo.

Yani nilikaribisha 2022 in style. Na ni katiyeye sana Sana anafanyaga niingie jamvini kuwin wadau kisaikolojia


Kwanini unamuombea mabaya na kifo?

Uliwekeza sana kwake ? [emoji3][emoji851]

Ni kweli inaumaga lakini Mungu atuhurumie na atupe wepesi wa kuachilia na kumwachia Mungu mwenyewe awafanyie visasi.
 
📖LK 17:3-4
▪Samehe uendelee na maisha yako.

▪Samehe uruhusu baraka za Mungu zitende kazi kwako.

▪Samehe utue mzigo mzito ndani yako.

▪Samehe umruhusu Mungu ashughulike naye/nao

▪Samehe urejeshe afya yako iliyoharibika.

▪Samehe urejeshe mahusiano yako mazuri na Mungu.

Soma neno ukue kiroho
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom