RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Tunakukumbusha!
✍️Sisi ni marafiki zako tunaokupenda, lakini ukifilisika kamwe hatutopokea simu yako na hatutopenda kukuona machoni mwetu.
✍️Elewa sisi ni watu wako wa karibu sana, lakini ukifilisika hutoweza tena ku-view status zetu za WhatSapp.
✍️Ni kweli tunakupenda kama rafiki yetu na mdau wetu wa karibu, lakini ukifilisika hatutokunywa tena pombe na wewe.
✍️Amini tunayokwambia wewe ni rafiki yetu tunakupenda sana, lakini ukifilisika mpenzi wako atakuwa mpenzi wetu. Yaani shemeji yetu atakuwa shemeji yako.
✍️Tunaapa viapo vyote kuwa wewe ni rafiki yetu ambaye unatusaidia sana, lakini amini haya tunayokwambia kuwa ukifilisika hatukujui.
✍️Achana na hao ndugu zako twende tukale bata, maisha ni mafupi sana. Lakini hatukufichi ukifilisika rudi kwa hao ndugu zako.
👁️ Naam! Naamini ushaelewa ni kwa nini tunakupenda na kwanini tupo karibu na wewe. Ishi na watu kwa akili binadamu tunasahau wema - usiseme hatukukwambia.
RIGHT MARKER,
DAR ES SALAAM.