Ishu ya kung'atwa na paka, Ray C kufa ndani ya siku 97.

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Staa anayetamba na ngoma mpya ya ‘ Nshumu
Nshumu ’ , Rehema Chalamila ‘ Ray C ’ amevamiwa na
kung ’ atwa mguuni na paka anayesadikiwa kuwa na
kichaa hivyo kuibua mjadala kuwa endapo hatazingatia
chanjo (Vaccination) anahofiwa kufa ndani ya siku 97
tangu alipokutwa na kisanga hicho wiki mbili zilizopita .
Kwa mujibu wa shuhuda wetu , Ray C aling ’ atwa na
paka huyo eneo la kutolea dawa za Methadone , ndani
ya Hospitali ya Mwananyamala , Dar ambapo alikwenda
kunywa dawa ya kuachana na matumizi ya madawa ya
kulevya .
“Ray C alikuwa anakatiza kwa miguu , ghafla akarukiwa
na paka na kumng ’ ang’ ania mguu kwa meno .
“Ray C alijaribu kumzuia lakini hakufanikiwa hivyo
alisababisha bonge la tafrani. Kama siyo watu
kumsaidia yule paka asingetoka mguuni kwake , ”
alisema shuhuda huyo akisisitiza si bure paka huyo
alikuwa na kichaa (rabies ) .
Ilifahamika kwamba baada ya paka huyo kumvamia ,
alikimbilia chumba cha matibabu hospitalini hapo
ambapo alipata huduma ya kwanza lakini baada ya
hapo mguu wake ulianza kuvimba . Baada ya
kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa lilimtafuta Ray C
ambaye alikiri kuvamiwa na kung ’ atwa na paka huyo
huku akipinga madai kwamba labda alitumiwa kichawi .
“Kiukweli naendelea vizuri na jeraha limepona baada ya
kupatiwa matibabu . Watu wanasema sana lakini mimi
sina imani za kichawi , ” alisema Ray C . Maelezo ya
kitaalam yalionesha kwamba endapo Ray C aling ’ atwa
na paka mwenye kichaa , muda wa kupata virusi vya
ugonjwa huo hadi kuanza kwa dalili , kwa kawaida
unaweza kuwa kati ya wiki 3 hadi 12 .
‘ Ray C ’ .
Maelezo hayo ya kitaalam yalieleza kwamba , mara
baada ya kung ’ atwa , Ray C alipaswa kupata chanjo ya
kwanza siku hiyohiyo, chanjo ya pili ilitakiwa iwe
baada ya siku tatu , chanjo ya tatu iwe baada ya siku
saba na chanjo ya mwisho iwe baada ya siku kumi na
nne kama alikuwa hajapata chanjo hiyo kabla .
Kama Ray C aliwahi kuchanjwa dhidi ya ugonjwa huo,
alipaswa apewe chanjo mbili, moja palepale (kinga ) na
nyingine siku ya tatu. Kitaalam ilielezwa kwamba kama
Ray C hatafuata utaratibu huo wa chanjo , atakaa kati ya
siku 21 hadi 90 ambapo dalili za ugonjwa wa kichaa
cha mbwa zitakuwa zimeanza kuonekana , ukijumlisha
na siku saba za kuumwa basi atakiona kifo ndani ya
siku 97 hivyo cha msingi ni kuzingatia chanjo .
Dalili za mtu mwenye ugonjwa huo ambao kiwango cha
kuua ni asilimia 100, ni pamoja na homa kali , kuumwa
kichwa , kuvimba na kuwashwa koo .
Nyingine ni kuwa mwoga , kuchanganyikiwa, kuwa na
tabia zisizo za kawaida , maumivu , kuona vitu ambavyo
havipo (maruweruwe ) , kujifichaficha kwenye kona au
kukimbia , kuogopa maji (hydrophobia ) , mwili kupooza
na kushindwa kula. Nyingine ni mgonjwa kushtushwa
na mwanga na kelele , kupoteza fahamu na mwisho
hupatwa na mauti .
Kwa mujibu wa wataalam hao, muongozo
unaojitosheleza wa kupambana na ugonjwa huo ni
pamoja na kutoa taarifa ya mnyama ( mbwa au paka )
anayehisiwa kuwa na kichaa na kumuangamiza haraka
iwezekanavyo kabla hajasababisha madhara zaidi .
Pia watu wanashauriwa kuwachanja mbwa au paka
wote kwa wakati mmoja na kuendelea kuwachanja
watakaozaliwa huku wakidhibiti mbwa
wanaotangatanga na kuwaua mbwa wote ambao
hawajachanjwa .
 

Attachments

  • 1419784570332.jpg
    45.4 KB · Views: 1,808
Labda Dr Mzizi mkavu na Riwa watusaidie ukweli kwenye hili swala!
 
Last edited by a moderator:
picha yake apo chini ray c anaonekana mshangazii sanaa... duhu naka umri kamesha sogea na majuzi alikua mkasi analalamika anatamani kupata mtoto naona ndo basi tena.. nitole iyo.
 
Mi nilidhani kafa tuanze kukusanya rambirambii
 
Babake rais kwa hiyo atapelekwa bartmore kupasuliwa mguu kutoa tezi la mguu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…