LGE2024 Isihaka Mchinjita: Suluhisho la kudumu la kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji ni kuiondoa CCM madarakani

LGE2024 Isihaka Mchinjita: Suluhisho la kudumu la kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji ni kuiondoa CCM madarakani

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo @ACTwazalendo Bara, Isihaka Mchinjita @MchinjitaIR, amesema kuwa suluhisho la kudumu la kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji ni kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho anadai ndicho chanzo cha matatizo hayo.

Akihutubia wakazi wa kijiji cha Chipome, jimbo la Tunduru Kusini mkoani Ruvuma, Novemba 24, 2024, Mchinjita amesisitiza kuwa mtu aliyeanzisha tatizo hawezi kuwa suluhisho la tatizo hilo.

“CCM lazima waondoke ili tuondokane na migogoro ya wakulima na wafugaji,” amesema.

Amebainisha kuwa ACT Wazalendo inataka mipango yote ya matumizi ya ardhi vijijini kuendeshwa kwa uwazi, kwa kushirikisha mamlaka ya wananchi kupitia mikutano mikuu ya vijiji.

Ameendelea kusisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuamua matumizi ya ardhi yao, ikiwa ni pamoja na kugawa maeneo kwa ajili ya ufugaji, huku wakipanga idadi ya mifugo inayoweza kufugwa katika maeneo husika.

“Hatutaki mambo ya kuletewa wafugaji kutoka nje bila mipango, wakulima na wafugaji kuchanganywa, kisha wanageuka kuwa maadui na kuwindana wao kwa wao,” amengeza.

Aidha Mchinjita amewanadi wagombea wa ACT Wazalendo katika kijiji hicho, akiwataka wananchi kuwapa nafasi ya kuleta mabadiliko kupitia uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
 
Isihaka Mchinjita, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo amesema kuwa ili migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji iishe basi wananchi wakiondoe madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa chama hicho kimeshindwa kumaliza migogoro hiyo.

 
Back
Top Bottom