Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,972
Wakuu,
Tangu mchakato wa Katiba Mpya uanze kumrkuwa na maswali mengi kuliko majibu! Kwanza Ilani ya Uchaguzi ya CCM, 2005 haikuwa na kipengele cha Katiba Mpya bali ilikuwa na suala la MAHAKAMA YA KADHI ambalo lilileta mtafaruku mkubwa sana! Nahisi Wakristo walikosa imani na JK. Mwaka 2010 suala la KADHI liliondolewa na JK katika Hotuba yake katika Baraza la Iddi alisema kuwa suala la MAHAKAMA YA KADHI ni Ibada ya Waislamu na wanatakiwa waianzishe na kuigharamia wenyewe!
Cha kushangaza hatukuona reaction kubwa sana toka kwa Waislamu baada ya kauli hiyo ya JK! Ukiona kobe kainama ujue anatunga Sheria!
Mara ikafika tarehe 31 Oktoba 2010 tukamsikia JK ananguruma akilitangazia taifa juu ya Katiba Mpya!
Kabla ya hapo Mwanasheria Mkuu, Jaji Werema na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani walishatuhakikishia kuwa "Katiba Mpya - NO!"
Kwa lugha nyingine ni kwamba, suala la Katiba Mpya halikujadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri, otherwise wajumbe 2 wa Baraza hilo yaani Celina Kombani na Jaji Werema wasingejitokeza hadharani kutoa kauli za kupinga uwepo wa mchakato wa kutunga Katiba Mpya! Kumbuka kuwa kwa mujibu wa "Doctrine of Collective Responsibility" wajumbe wa Cabinet hawaruhusiwi kwenda kinyume na yale yaliyokubaliwa kwenye Cabinet, otherwise walitakiwa wajiuzulu!
Wengi walijiuliza kuwa wazo la kutunga Katiba Mpya nani alimpatia JK maana hata kwenye Chama halikujadiliwa!
Kiu ya baadhi ya wanasiasa ya kuona kuwa Tz inakuwa na Katiba Mpya ilifunika mashaka yote hayo! Wanasema kuwa ukweli ni ukweli tu hata kama umetoka kwa Shetani! Madam ni kweli baadhi ya wanasiasa walitaka Katiba Mpya haidhuru wazo lilitoka wapi, ni sawa tu kwao!
Sheria ilitungwa, Tume iliundwa. Ikakusanya maoni. Waislamu waliapa kuwa bila suala la KADHI kuingizwa kwenye Katiba Mpya hawatakubali!
Composition ya Tume nayo ilitia mashaka kuwa watu wa Dini fulani walikuwa wa "Kuitetea MAHAKAMA YA KADHI" kuliko kuipinga!
Hata hivyo Tume ya Warioba ilifunika kombe ili mwanaharamu apite! Walipiga chini mambo ya KADHI na surprisingly hatukuona reaction yoyote ya watu wa "DINI ILE!"
Sasa hivi tumeshuhudia mjadala mkali kwenye Kamati za Bunge Maalum la Katiba juu ya suala la KADHI! Waislamu nao kwa sasa wamekuja juu wakidai kuwa "BILA MAHAKAMA YA KADHI HAKUNA KATIBA MPYA!"
Cha kujiuliza ni je, huu mchakato ambao ulianza katika mazingira ya kutatanisha kumbe lengo lake ndio lilikuwa hili? JK mwenyewe wakati wa kulizindua Bunge Maalum la Katiba alisisitizia juu ya Makakama ya Kadhi kwenye Hotuba yake!
Watz wenye mapenzi mema na nchi yetu hawawezi kukubali masuala ya Dini kuchanganywa na yale ya Serikali!
Dunia ya sasa haikaliki kwa sababu ya Serikali za Nchi mbalimbali kukumbatia Imani za kidini!
Wewe fikiria huko Iraq na Syria zenye Waislamu wengi eti wanataka kuwa na Islamic state! Hayo mambo yalilelewa muda mrefu ndio tunaona matokeo yake. Hivyo hivyo huko Nigeria na kwingineko!
Huko Kenya nako watapata majanga makubwa hata kuliko ya Al Shaabab!
Waislamu ni ndugu zetu na tunawatakia mema katika Dini yao lakini wafanye mambo yao badala ya kutaka wasio Waislamu wachangie kueneza imani yao!
Otherwise, kama JK lengo lake lilikuwa ni kuwaridhisha watu wa Dini yake ambao kwa sasa wanadai kuwa "BILA MAHAKAMA YA KADHI HAKUNA KATIBA MPYA" basi hiyo Katiba na hiyo Mahakama visiwepo maana ni afadhali Katiba ya sasa imetuweka katika hali ya amani muda wa nusu karne kuliko hii itakayoiangamiza nchi muda wa miaka 2 tu!