La kujifunza lipo, nalo ni kwamba njaa ni mbaya! Inahamia kichwani kama ilivyohamia ya huyu Dr. MihogoMie kwa mtazamo wngu lipo la kujifunza kupitia andiko lake nakushauri jaribu kulisoma narudia tna ukiacha kkubari hongo ya nafasi ya ubalozi na kumpiga Kampeni Mh Magufuli lipo pia la kujifunza ndani yke...
Sent using Jamii Forums mobile app
La kujifunza lipo, nalo ni kwamba njaa ni mbaya! Inahamia kichwani kama ilivyohamia ya huyu Dr. Mihogo
Nimekuelewa mkuu,Hakuna mpambano wa vyama kwa sababu vyama havina tena itikadi zinazoeleweka. CCM haijulikani inasimamia na kuongozwa na itikadi gani kama ilivyo kwa baadhi ya vyama vya upinzani
CCM inachotaka inachukua! Inachukua iwe ni "wanachama" iwe ni ushindi nk, inachukua kwa sababu CCM sio kwamba ni Chama Dola bali CCM ndio DOLA yenyewe(tafakari hata usajili wake). Hao kina Balozi Dr Slaa, Dr Mashinji, Mwanakijiji na weengi wengine ambao bado wapo vyama vya upinzani ni watumishi wa DOLA wakitumikia mfumo kwa kadri wanavyoelekezwa
Ajabu ni kwamba weledi ni kama unapungua/ umepungua katika kuyaendesha mambo haya kiasi cha watu wa kawaida kugundua na kuhisi uwepo wa nguvu hii ambayo kikawaida inatakiwa ijifiche sana. Tangia enzi za awamu ya kwanza kwa mfano kulikua na Majaji ambao ni wa kwenye "mfumo" lakini kulikua na weledi wa hali ya juu kutokuwa expose tofauti ilivyo sasa ambapo you can easily spot them
Mwalimu Nyerere alipotoa hoja na shinikizo kwa CCM(dola) kukubali mfumo wa vyama vingi alisema ni muhimu CCM(DOLA) isimamie kuanzishwa kwa siasa hizo ili "iuratibu" mfumo huo yenyewe kabda watu hawajaudai. Mwalimu alikua ni bingwa wa siasa na ndie aliyeusuka 'mfumo" na wengi hawakumuelewa alikua na maana gani aliposema CCM (dola) "iratibu" ujio na uwepo wa vyama vingi
Ushauri wa Mwalimu ulifuatwa ila kwa sasa kinachokosekana ni weledi. Angekuwepo nadhani CCM(dola) ingeshameguka kama "alivyotamani" na kungekua na vyama viwili vikubwa vyenye nguvu sawa vikiachiana madaraka kwa maelekezo kutoka "mahala" na huku kukiwa na stability ya kisiasa na kiusalama nchini. Ni wachache walimuelewa. Mwenyewe aliwahi kusema kua Marekani kuna chama kimoja tu hayo mengine mbwembwe tu
Alimaanisha uwepo wa Republican na Democrat ni uratibu wa Dola na hivyo vyama ndio Dola la Marekani. Ndio maana misingi ya kitaifa ya nchi ile ikiwa ni pamoja na ubabe na ubeberu kwa mataifa mengine uko palepale miaka yote, watawale Democrats au Republicans. Natamani watu waelewe
Mkuu labda hujaijua organisation ya CCM. Hata kama unatamani lakini kuitoa CCM madarakani futa kabisa akilini mwako
Nimekuelewa mkuu,
Kwamba hata mwalimu aliporuhusu upinzani nchini hakuwa anamaanisha upinzani per-say. Ila upinzani aliokusudia ni wa CCM kuweza kujikinga na upinzani! kwamba CCM ndio dola na ndio upinzani at the same time. kwamba mwalimu alituchezea akili watanzania!
Absolutely. Wakati Mwalimu Nyerere anawaambia CCM wakubali na kisha wasimamie ujio wa vyama vingi wengi hawakumuelewa wakidhani anataka kuleta upinzani ambao pengine unaweza kuchukua nchi. Hakua na maana hiyo na "wahusoka" walimuelewa alipokaa nao nyuma ya pazia na kuwaingiza darasaniNimekuelewa mkuu,
Kwamba hata mwalimu aliporuhusu upinzani nchini hakuwa anamaanisha upinzani per-say. Ila upinzani aliokusudia ni wa CCM kuweza kujikinga na upinzani! kwamba CCM ndio dola na ndio upinzani at the same time. kwamba mwalimu alituchezea akili watanzania!
Kwani hao uliowataja wapo Chama gani kwa sasa? Na kama ni wabaya mbona wamepokewa ndani ya CCM kwa vifijo?Hiyo kali ndio maana CCM itaendelea kuwagawa ili itawale milele tuache ushabiki yani hkn la kujifunza mtaendelea kupokea makapi kutoka CCM km kweli unaitakia mema Chadema yko lazima lazima ukubari chama kilifanya makosa kumpokea Mh Lowasa na Mh Sumaye ilo lipo wazi kbs... View attachment 1365112
Sent using Jamii Forums mobile app
CHADEMA ingekuwa katika hali mbaya sana, kama wote waliojitoa ndani ya chama hicho, huku wakielekeza tuhuma zao kwa viongozi wa chama, wangekomaa tu, angalau kwa muda bila kujiunga CCM, watu wengi wangeelewa kwamba ndani ya CHADEMA pana matatizo makubwa.
Lakini hizi juhudi za kukidhoofisha CHADEMA kwa njia hii inayotumika sasa hivi, badala yake inaweza ikawa inawaongezea CHADEMA nguvu.
Kwa hali hiyo basi, juhudi za CCM kukidhoofisha CHADEMA zinafifishwa (diluted) kwa kutokuwa na kutoelewa mbinu sahihi kwa upande wa CCM.
Hao wanaolipwa na CCM humu mtandaoni kuwalaumu Mbowe, 'specifically', nao wanakosa weledi wa kujua kwamba historia ya mabandiko yao humu JF siku zote yanaelekezwa kwenye kumkatisha tamaa Mbowe ili CHADEMA isambaratike.
Sasa hii "Misimamo Rasmi" ndiyo itakayowaaminisha wasiokubali hadaa hizo?
Watu wenye kufikiri watajiuliza, leo itakuwaje huyo anayeiua CHADEMA ashutumiwe kwa vile anatimiza lengo lao?
N.B. Sina 'interest' yoyote na CHADEMA au Mbowe, mbali ya kutetea haki ndani ya nchi yetu Tanzania, na kutamani uwepo wa mabadiliko. CCM sasa basi, inatosha.
Kwani hao uliowataja wapo Chama gani kwa sasa? Na kama ni wabaya mbona wamepokewa ndani ya CCM kwa vifijo?
Kwani hao uliowataja wapo Chama gani kwa sasa? Na kama ni wabaya mbona wamepokewa ndani ya CCM kwa vifijo?
Mkuu unajadili mada ki shabiki sana mpaka unapoteza point za maana; mara unapost kitabu cha Daktari kama ndo mwarobaini ya siasa za Tanzania.Lazima mkubari hkn jambo mzuri kwenye maisha km kufanya kosa na kkubari kosa kujipanga usirudie tna Chadema mlifanya makosa makubwa kupokea wezi wale...
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu labda hujaijua organisation ya CCM. Hata kama unatamani lakini kuitoa CCM madarakani futa kabisa akilini mwako
Mkuu unajadili mada ki shabiki sana mpaka unapoteza point za maana; mara unapost kitabu cha Daktari kama ndo mwarobaini ya siasa za Tanzania.
Kila wakati huwa tunasikia CCM imekufa na baadae wanaosema imekufa wanahamia kwenye Chama hichohicho inachosemekana kimekufa.
CCM naiona ikishinda uchaguzi mkuu wa 2020 iwe kwa halali au kwahila. Tuambieni CDM mtatumia mbinu Gani Mpya kuitoa CCM? Mtawatumia USA na nchi zingine za magharibi? Kwani nchi hizo zinataka kuitoa CCM au zinataka rasilimali? Je CCM wakiamua kuwapa watakacho huo huko mnakosemelea hizo rasilimali za nchi Kama madini n. K mtakimbilia wapi kusemelea?
Rudi kwetu wananchi mtupange mpaka tuwaelewe njooni vijijini Huku maana Hatutumii hata social media Huku.
Sent using Jamii Forums mobile app