Isingekuwa ubinafsi na uoga wa viongozi Mkulima huyu Eldoforce Bilohe angechukua fomu ya Urais 2020

Isingekuwa ubinafsi na uoga wa viongozi Mkulima huyu Eldoforce Bilohe angechukua fomu ya Urais 2020

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mnamkumbuka Huyu Mkulima___ ( 800 X 640 ).jpg


Huyu ndiye mgombea Urais wa CCM aliyenivutia kwenye uchaguzi wa 2015 , zipo tetesi kwamba mwaka huu alishajipanga kuchukua tena fomu , lakini amekatishwa tamaa na utaratibu wa CCM.

====

Mkulima wa darasa la saba ataka urais CCM​


KATIKA hali isiyo ya kawaida, mkulima kutoka Kijiji cha Mjimtala Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Eldoforce Bilohe (43) jana alitinga makao makuu ya Chama Cha Mapindizi (CCM) kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kuteuliwa kuwa mgombea urais, bila kuwa na ada huku akiwa amebeba maji ya chupa kwapani.

Bilohe ambaye alisema elimu yake niya darasa la Saba, aliwasili makao makuu ya CCM muda wa saa 5:40 asubuhi na kuelekea Ofisi ya kupokea wagombea ndani ya ofisi baada ya kuwapita waandishi wa habari wakiwemo wapiga picha, waliokuwa wamejipanga kumsubiria,lakini aliwapita waandishi bila kumtambua kuwa ni mgombea.Akiwa amevaa suruali ya kaki na fulani yenye rangi ya kijani na njano, alionekana kuduwaza watu wengi, ambao walikuwa wakiwasuburi wagombea, ambao walikuwa wakichukua fomu jana.

Akiwa kati ya watu waliokuwa kwenye orodha ya kuchukua fomu, Bilohe alikuwa amebeba chupa ya maji kwapani baada ya kufika na kupokelewa na maafisa, ambao walimtambua kuwa ni mgombea na ndipo wapiga picha waligutuka na kuanza kupiga picha.Kisha aliingia ndani ya ofisi ya kuchukua fomu na alitoka baada ya muda mfupi na kuanza kuhojiwa na waandishi wa habari.

Alisema amefika Dodoma kwa ajili yakuchukua fomu ya kuteuliwa kuwa mgombea urais, lakini kwa sababu ambazo hazijafahamika, aliambiwa akachukue fedha.“Nilipigiwa simu wakati niko benki yaCRDB nikiwa kwenye foleni, nikisubiri kuchukua fedha, ndiyo nikakimbia kuja hapa,” alisema.Alisema amekuwa mwanachama haiwa CCM tangu mwaka 2003 na elimuyake ni ya msingi na ana uzoefu kutokana na kuwa katika chama kwa muda mrefu.“Nimekuja kama nilivyo kwa sababu sijawahi kuwa na makundi unayoyaona wewe, mimi ni mwanachama wa kawaida kama wanachama wengine,” alisema.

Mmoja wa maofisa wa chama, ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema Bilohe amerudisha si kwa sababu hana hela, bali kuna vigezo ambavyo havijafikiwa, ikiwemo baruaya utambulisho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya aliyotoka.“Hajakamilisha taratibu za kumwezesha kuhukua fomu,” alisema.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zilisema kuwa tayari mkulima huyo ameshalipia ada ya fomu ya Sh 1,000,000 na atachukua fomu
 
Mwambie mkulima arudi shambani kuwinda tumbili, fomu ilikuwa moja tu. Tunabana matumizi, maana kuchapisha fomu moja ya urais ni sawa na bajeti ya wizara fulani hivi.
 
Utaratibu wa Chadema ukiwa kero Kwa CCM, ni ujinga mkubwa, Nilichokilima Mimi nikiamua kukifyeka, yanini wewe uone kero?

Nguvu ni zangu, gharama nimeitumia mie, ya nini uone kero?

Akaribishwe kwingine, shida iko wapi?
 
Utaratibu wa Chadema ukiwa kero Kwa Ccm, ni ujinga mkubwa, Nilichokilima Mimi nikiamua kukifyeka, yanini wewe uone kero?

Nguvu ni zangu, gharama nimeitumia mie, ya nini uone kero?

Akaribishwe kwingine, shida iko wapi?
Jikite kwenye mada
 
Anaweza kuomba kugombea kupitia Ufipa. Ni demokrasia pia
 
Unajua huyu "Mkulima" anafanya gani tangu JPM aingie madarakani? Kama hujui, basi kaa na hili; CCM ina "hazina" na inajua kuitumia.
 
2015 ulivutiwa na Lowasa kwa pesa zake maana penye pesa wanasiasa huwa kama malaya msemo wa mzee Nyerere
 
Bashiru kafungia fomu ofisini kaondoka na funguo.
Ha ha haaa... unanikumbusha "uchafuzi wa SM" Sitoshagaa kusikia wapinzani wanaogombea urais, ubunge na udiwani JMT "WAKIKOSEA KUJAZA FOMU AU KUTOZIPELEKA PANAPOHUSIKA!!!"
Maana ofisi zaweza fungwa tena!!
 
Mwambie mkulima arudi shambani kuwinda tumbili, fomu ilikuwa moja tu. Tunabana matumizi, maana kuchapisha fomu moja ya urais ni sawa na bajeti ya wizara fulani hivi.

Kwi kwi kwi
.. na ngiri, kwale, dikdik, .... nyama kibao!
 
Back
Top Bottom