Isiye waterfalls: Sehemu mpya ya kitalii Moshi

Isiye waterfalls: Sehemu mpya ya kitalii Moshi

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Katika mkoa wenye vivutio vingi vya kitalii basi ni mkoa wa Kilimanjaro.

Hii inatokana na uwepo wa mlima,ukiachilia mbali mlima huu kuwa kivutio,kuna mito inayotoka mlimani inayoteremka na baadae kuwa mto mmoja yani mto Pangani ambao unamwaga maji yake kwenye bahari ya Hindi.

Uwepo wa mito hiyo umetokeza maporomoko mengi sana ya maji (waterfalls) hasa Marangu.

Kwa sasa naomba kuitangazia dunia na serikali yetu eneo jipya kabisa la kitalii. Isiye waterfalls.

IMG_20201231_151040_3.jpg

Maporomoko hayo yanapatikana kwenye mto Isiye amabayo yapo karibu na kijiji cha Uri kata ya Kibosho wilaya ya Moshi vijijini.

Sehemu hii bado ni mpya inahitaji maboresho mbalimbali ili watalii watapofika waweze kujionea,kupiga picha, kupumzika na kuoga pia.

Bonyeza hapa kuona kwenye ramani moja kwa moja Isiye Waterfall

Serikali kushirikiana na wananchi ni muhimu sana kuboresha ili kuweza kuliingizia taifa pesa na kwa wananchi watajenga migahawa, guest za wageni na maduka n.k ili kutoa huduma kwa watalii

kwa mdau wa maendeleo fanyeni kuingia Google map mkadirie(rate) na kucomment pamoja na kuongeza picha.
 
Vipi hatuwezi kuzalisha umeme hapo?

Ova
 
Mto umbwe una waterfalls Ila geographical yake ni ngumu sana mtu kuzifikia
Mkuu kwa wanadamu kigumu ni roho tu,umeona utalii wa China? Wanatengeneza madaraja ambayo kwa macho huwez kuamini, kutokana na ubunifu huo madaraja mengine yamekuwa kivutio bila wao kutarajia
 
Mkuu kwa wanadamu kigumu ni roho tu,umeona utalii wa China? Wanatengeneza madaraja ambayo kwa macho huwez kuamini, kutokana na ubunifu huo madaraja mengine yamekuwa kivutio bila wao kutarajia
Kweli aisee
 
Kwahiyo hii waterfalls ndiyo imetokea Jan 202⁉️⁉️⁉️😤
Tanganyika ilipata uhuru 1961 kabla yake haikuepo? Au muungano uliofanyika 1964 kabla yake hazikuepo hizo ncho?Swali la kipuuzi sana hili
 
Tanganyika ilipata uhuru 1961 kabla yake haikuepo? Au muungano uliofanyika 1964 kabla yake hazikuepo hizo ncho?Swali la kipuuzi sana hili
Haya kabla ya utambulisho hapo kwenye waterfalls palikuaje mwaka mmoja uliopita?
 
Haya kabla ya utambulisho hapo kwenye waterfalls palikuaje mwaka mmoja uliopita?
Ilikuepo tu sema kugundua sasa,kwani hata Materuni haikuepo miaka ya 1700?? Shida kujua kama hii kitu ni fursa
 
"Maporomoko hayo yanapatikana kwenye mto Isiye amabayo yapo karibu na kijiji cha Uri kata ya Kibosho wilaya ya Moshi vijijini."

"Kibosho" ni Tarafa. Miongoni mwa kata zake ni pamoja na Kibosho Magharibi, Kibosho Mashariki na Kibosho Kati.

Hakuna kata ya "Kibosho".
 
Jambo la kushangaza pamoja na Marangu kuwa na maporomoko mengi ya maji lakini kwenye mitandao inajulikana 1 tu. Materuni waterfalls sio mitandao ya kizalendo wala ya kibeberu(wikipedia)

Watanzania tunafeli wapi tunapishana na pesa hizi?
 
Back
Top Bottom