Ni mambo ya ndani ya msumbiji.
Yanahusu wananchi wa Cal Delgado na Frelimo.
Jimbo hili lina waislam wengi wamakonde.
Ni eneo la kaskazini na linapakana na Tanzania.
Baada ya uhuru frelimo walilitupa na kubagua wa eneo hili.
Hawamo serikalini.
Hawamo jeshini
Mji wao hauna huduma zozote zile muhimu.
Ni eneo maskini zaidi msumbiji.
Jimbo hili sasa limepata Gas kwa wingi lakini frelimo haina sera ya angalau kuwadanganya kwa jimbo hilo kufaidika na rasilimali hio.
Kuna kitu kingine Kina Samora na Mondlane walipo anzisha mapambano ya kuwaondoa wareno basi harakati hizo zilianza Tanzania kupitia eneo hili lenye wamakonde na waislam wengi.
Jeshi la frelimo la ukombozi lilikua na hawa jamaa na tuliwafundisha sisi
Kusini ya msumbiji walikuwepo Ranamo.
Kwa ufupi baada ya uhuru Samora na kundi lao lilianza kuwatoa jeshini wamakonde hawa na eneo ziliko anza harakati ya uhuru likatupwa kwenye dimbwi la umasikini
Hivo hizi ni harakati za ndani kudai usawa na haki ya utajiri wa gas.
Huwezi kundoa Uislam wa asili jimbo hili na kuubandika Isis.
Ni kawaida kumbandika mpinzani wako jina baya ili uungwe mkono na dunia.
Na kwa sababu hizi msumbiji wanaungwa mkono na SA na hata sisi.
Lakini hii ni vita ya ndani. Ni vema wakapatanishwa na kufanya suluhu kwani wanaungwa mkono na watu wao.
Tusiwe na double standard mfano Juba Sudan Ilipo taka kujitenga na Khatoum kwasababu walionewa na wakiwatenga kwa sabaabu wao ni wakristo tukawaunga mkono . Na hatikuwaita magaidi hata johnn Garang alikuwepo UDSM
Lakini hawa wa msumbiji ni magaidi kwa sababu ni waislam hivo sawa kuonewa
Sent using
Jamii Forums mobile app