Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Katika kuthamini mchango wa kiongozi mkuu wa Hamas aliyefariki, Ismael Haniyeh tunaweza kuchukua mafunzo machache katika uongozi wake.
Kutokana na huzuni ya kumpoteza kiongozi huyo sitokwenda mbali kuangalia historia yote ya maisha yake.Machache ninayoweza kuyataja ni kama ifuatavyo.
Alizaliwa mwaka 1962 na mpaka anauliwa alikuwa na miaka 62. Alizaliwa kwenye kambi ya wakimbizi huko Gaza kutokana na wazee waliohamishwa na Israel kutoka mji wa Ashkelon mwaka 1948.
Alisoma shule za msingi na sekondari huko huko Gaza na hatimae kujiunga na chuo kikuu cha kiislamu huko huko Gaza ambako alifaulu kwa kiwango cha juu katika faisihi ya lugha ya kiarabu.
Baadae alikuwa muhadhiri katika chuo kikuu hicho na kuwa karibu na muasisi wa kundi hilo,sheikh Ahmed Yasin
Akiwa na miara 25 akiwa sekondari aliwahi kuwekwa gerezani na Israel kutokana na harakati zake za kupinga uvamizi wa ardhi za Palestina unaofanywa na Israel.Aliwekwa gerezani kwa mara nyengine mbili ikiwemo kukaaa kwa miaka mitatu kabla ya kuachiwa huru akaishi Lebanon.
Alirudi Gaza mwaka 1993 na kujiunga na vuguvugu la siasa ambapo hatimae aliwahi kuwa waziri mkuu wa Palestina chini ya Fatah.Baadae mwaka 2006 Fatah ilikataa kufanya kazi na Hamas na akaondoka madarakani kurudi Gaza ambapo chama cha Hamas katika uchaguzi wa mwaka 2007 kilishinda dhidi ya fatah na kuanzisha serikali yao.
Mwaka 2019 kwa hekima za uongozi alikubaliana na makundi yanayofanya kazi Gaza kuachia uongozi na kuondoka Gaza ili kuongoza kisiasa akiwa nje ya nchi hiyo.Mpango huo ulileleta faida kubwa sana kwani walifanikiwa kuiimarisha Gaza kijeshi na kisiasa.
Katika maisha yake amenusurika mara kadhaa na majaribio ya kumuua kabla ya shambulio la juzi huko Teheran ambapo alliuliwa kutoka na shambuliwa ambaklo kwa mujibu wa Iran na Hamas yenyewe lililofanywa kwa ushirikiano wa Israel na Marekani.
Katikati ya vita vya Gaza Israel iliwauwa kwa makusudi mke,watoto na wajukuu zake wengi na baadae dada na watu kadhaa wa familia yake.Kitu cha kushangaza kwa watu wengi ni kwamba mauwaji hayo hayakumbadilisha chochote Ismail Haniye na hakufa kwa ugonjwa wa moyo wala kuacha harakati za kuitetea Palestina na wala hakulegeza misimamo dhidi ya Israel.
Pamoja na kuuliwa kwa idadi kubwa ya wapalestina na wapiganaji wake huko Gaza lakini kiongozi huyo kwa nguvu kubwa ya kiimani ya kiislamu hakuamrisha kusalimu amri kwa harakati zao za mapigano dhidi ya Israel.
Masaa machache kabla ya kuuliwa kwa shambulio la ndege huko Iran bado Ismael Haniye alionekana akiwa na afya nzuri na mcheshi japo alipatwa na misiba mingi sana katika maisha yake.