Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ISMAIL ALI MLAPAKORO AMEFARIKI DUNIA
Familia iliyotoa mchango mkubwa kwa Uhuru wa Tanganyika, Elimu na soka la Tanzania
Na. Mohammed Said
Ndugu zetu wa Morogoro wamepata msiba mkubwa kwa kifo cha Ismail Ali Mlapakoro.
Ismaili Ali Mlapakoro ni Mchezaji kiungo WA timu maarufu .kaka sitini na sabini mjini Morogoro na nchi Jogoo na ni fundi umeme mstaafu wa Shirika la umeme(TANESCO) Tawi la Morogoro.
Baba wa marehemu, marehemu Mzee Ali Mlapakoro alikuwa Liwali wa Morogoro wakati wa ukoloni.
Mzee Ali Mlapakoro ndiye baba yake Hassan Mlapakoro aliyekuwa golikipa wa Sunderland na Simba.
Mzee Ali Mlapakoro alikuwa na ndugu yake akiitwa Salum Mlapakoro.
Salum Mlapakoro ndiye aliyeisimamia TANU Morogoro akisimama bega kwa bega na Mwalimu Nyerere kupigania uhuru wa Tanganyika.
Salum Mlapakoro ndiye baba yake mchezaji mwingine maarufu wa mpira wa Spurs ya Morogoro na timu ya taifa Kassim Manga.
Ukipenda unaweza ukamwita Kassim Manga Khamis Salum Mlapakoro.
Ukoo huu wa Mlapakoro ni maarufu Morogoro kwani umetoa liwali, umepigania uhuru, umetoa eneo lililojengwa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) zamani Agriculture College, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kadhalika familia hiyo imetoa mpigania uhuru, na watoto wao wakawa wachezaji mpira hodari katika wakati wao.
Sikupata kumfahamu Ismail Mlapakoro wala kuijua historia ya Mzee Mlapakoro kama mpigania uhuru ingawa watoto wa ukoo huu tulifahamiana toka ujana wetu.
NIlichukulia taarifa ya msiba wa ndugu yetu Ismail kama taarifa ya msiba lakini mpashaji habari wangu bila shaka alikuwa anajua sikuwa naufahamu ukoo wa Mlapakoro kwa namna uliivyostahili kufahamika.
"Huu ni msiba mkubwa kwa mitaa ya Boma, Mlapakoro, Amani, Karume (zamani Bandamela), Kata ya Mji Mkuu na mji mzima wa Morogoro.
Mzee Salum Mlapakoro ndiye aliyempokea Mwalimu Nyerere na kuipa nguvu TANU Morogoro."
Ndugu yangu akanieleza historia ya Mzee Mlapakoro katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nilisikitika sana.
Nafsi yangu iliumia kuwa nimeandika historia ya wazee wetu wengi jinsi walivyopambana kumwondoa mkoloni Tanganyika lakini sikupata kuijua historia ya Mzee Salum Mlapakoro.
Haya mambo imekuwaje kuwa hivi?
Sisi ni taifa gani lisilowatambua mashujaa wake waliopigania uhuru?
Nikajilaumu kuwa labda na mimi sikujihangaisha zaidi na ndiyo ikawa sababu ya kuikosa historia ya Morogoro na historia ya Mzee Salum Mlapakoro.
Haukuwa wakati wa kulaumiana.
Imenitosha kuwa ndugu yangu angalau kachukua juhudi ya kunitaarifu msiba wa ndugu yetu.
Hassan "Tony British" Mlapakoro yu hai na Allah ampe umri tawil, Manga katutangulia wote hawa wachezaji mpira maarufu wakati wao na Mzee Salum Mlapakoro ni baba mdogo wa Hassan na babu yake Manga kwa hiyo nasi ni baba na babu yetu.
Haukupita muda baada ya mazungumzo haya ndugu yangu akaniletea picha hizo hapo chini ya Ismail na ya Mzee Mlapakoro; na kunifahamisha kuwa wa kwanza kushoto ni Mzee Salum Mlapakoro akiwa na Mwalimu Nyerere mkutano wa Uchaguzi wa Kura Tatu mwaka wa 1958.
Kanikaangia mbuyu.
Nami nina meno ya kutafuna.
Haraka nikaingia Maktaba kutalii kitabu cha Saadan Abdu Kandoro, "Mwito wa Uhuru."
Kitabu hiki kina orodha ya wajumbe wote waliohudhuria mkutano wa Kura Tatu.
Naam naliona jina la Salum Mlapakoro kutoka Wilaya ya Morogoro.
Kisa cha picha hiyo nakifahamu na nimekieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
Kisa hiki alinieleza Mzee Bilal Rehani Waikela nyumbani kwake Tabora.
Picha hiyo imepigwa Igalula stesheni moja kabla ya treni kuingia Tabora.
Treni hii katika picha ilichukua wajumbe kutoka TANU HQ New Street, Dar-es-Salaam, Morogoro ikawachukua wajumbe wengine halikadhalika Dodoma hadi ilipofika Igalula.
DC wa Western Province alitoa amri kwa TANU Tabora kuwa hawana ruhusa kwenda stesheni kumpokea Nyerere na ujumbe wake uliokuwa unakuja kuhudhuria Mkutano Mkuu wa TANU wa mwaka wa 1958.
Wanachama wa TANU wakaenda Igalula kuisubiri treni na ilipofika wakamwamuru Mwalimu na wajumbe wote wateremke wakawaingiza kwenye magari na kuingia mjini Tabora kwa msafara wa magari na maandanano makubwa.
DC alijuta.
Alidhani anaikomoa TANU kumbe anajikomoa mwenyewe.
Hii picha ya Salum Mlapakoro na Julius Nyerere imepigwa Igalula wakati wanateremka kwenye treni.
Msiba wa ndugu yetu Ismail imekuwa sababu ya sisi kurudi nyuma kumkumbuka mzee wetu Salum Mlapakoro.
Mzee Salum hakuuona uhuru alifariki mwaka wa 1961 kabla ya uhuru wa Tanganyika.
Tunamuomba Allah amrehemu ndugu yetu Ismail amsamehe dhambi zake na amtie peponi.
Amin.