Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SMAIL BAYUMI MUASISI WA TANU CLUB MOMBASA 1950s
Nimemjua Ismail Bayumi Moshi mimi nikiwa mtoto mdogo wa darasa la pili au la tatu miaka ya mwanzoni 1960s.
Naukumbuka utanashati wake na gari yake nzuri aliyokuwa akiendesha.
Wakati huo nadhani alikuwa akija Moshi akitokea Mombasa kuja kuwatembelea wazee wake Mzee Likenji na Mama Koko.
Namkumbuka pia na dada yake Sophia Bayumi.
Hawa wote nitakuja kukutananao mimi nikiwa kijana na haikuwa tabu kwao kumkumbuka mama yangu maarufu kwa jina la Mama Mohamed muuguzi katika hospitali ya Dr. Georgiadis Nursing Home.
Mama yangu alikuwa mpangaji wa nyumba yao na kimbilio la kwanza kama mtoto wa jirani ataumwa usiku.
Hizi ndiyo kumbukumbu zangu za siku hizo.
Siku moja rafiki yangu toka utotoni Yusuf Mzee sasa sote tuko Dar es Salaam na wakati huo kamaliza shahada ya uhandisi Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam tumekutana mjini akaniambia Mzee Likenji kaja Dar-es-Salaam anaumwa yuko Muhimbili na yeye anaelekea huko.
Yusuf Mzee tumesoma sote darasa moja Lutheran Primary School Moshi baadae ikawa Stanley Primary na tulikuwa marafiki wakubwa pamoja na Yusuf Kibwana na kaka yake Shikeli Kibwana.
Shikeli alikwenda kusoma uganga Poland. Yusuf Kibwana na Yusuf Mzee nyumba zao zilikuwa jirani.
Yusuf Kibwana tulikuja kukutana Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam baada ya kupoteana karibu miaka 20.
Yusuf alikuja kusoma sheria. Nikaungana na Yusuf Mzee kwenda kumjulia hali Mzee Likenji Muhimbili.
Nilipigwa na butwaa kwani alinitambua mara moja na akaniita kwa jina langu, "Mohamed umekuwa mkubwa."
Lakini pale nilishangaa zaidi kumkuta rafiki yangu mwingine wa utotoni Moshi, Mangi na dada zake wamekuja kumuona Mzee Likenji.
Mangi ni mtoto wa Shariff Mundhari katika viongozi wakubwa wa Waislam Moshi mjini na Imam Mkuu wa Msikiti wa Riadha miaka ile sisi tukiwa wadogo.
Mzee Likenji akawa ananitania ananiambia nikae karibu na yeye nisimuogope hawezi kuniambukiza ugonjwa wake.
Kuna usemi wa Kiswahili unasema, "Milima haikutani lakini binadamu hukutana."
Turudi kwa Ismail Bayumi. Nilikuwa katika mazungumzo na Bibi Titi nyumbani kwake Upanga.
Bibi Titi akamtaja Ismail Bayumi.
Akaniambia niende Arusha kwa Ismail Bayumi anieleze mkutano aliofanya Mombasa Tononoka Hall wakati wa kupigania uhuru.
Nilikwenda Arusha na nikakutana na Ismail Bayumi.
Aliyonieleza nimeyaandika katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).
Bibi Titi alifanya mkutano mkubwa Tononoka Hall uliojaza watu ndani na nje ya ukumbi.
Chanzo cha safari ya Bibi Titi Mombasa ilikuwa Tom Mboya aliyemuomba rafiki yake Ismail Bayumi muasisi wa TANU Club Mombasa afikishe salamu kwa Julius Nyerere amlete Bibi Titi Mombasa afanye kampeni Jomo Kenyatta atolewe kifungoni.
Leo FB wameniwekea picha ya Ismail Bayumi.
Juzi juzi hapa nilikuwa Mombasa na nilikwenda kuutembelea Ukumbi wa Tononoka, mahali ambako Ismail Bayumi aliendesha harakati nyingi za TANU miaka ile ya kupigania uhuru.