Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
POSTA HIZI ZINASEMA NINI KUHUSU ZANZIBAR?
Nimeitazama picha ya Ismail Jussa akipokelewa uwanja wa ndege Zanzibar akitokea Nairobi kwenye matibabu.
Ismail yuko kwenye kiti cha magurudumu.
Yaliyomsibu sote tunayajua.
Unaweza kusema ni mchanganyiko maalum wa Ton Ton Macoute na Gestapo.
Nikimwangalia Jussa akiombewa dua vidole vikawa vinaniwasha niandike kitu kuhusu yeye.
Nikajiwa na fikra ya kiasi ya miaka 10 iliyopita wakati wa SUK na niko Zanzibar wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2010.
Nilipiga picha moja ya posta tatu za kampeni ikiwaonyesha vijana watatu wa Kizanzibari wakigombea nafasi kupitia CCM na CUF.
Katika hawa vijana watatu wawili nikifahamiana nao - Cholo Mughery na Jussa.
Licha ya kuwajua hawa wagombea posta zile zilikuwa zimebeba ujumbe mzito sana katika historia ya Zanzibar.
Hii ndiyo sababu nikapenda kuwa na picha hii.
Msomaji wangu tafadhali angalia posta hizi za uchaguzi wa mwaka wa 2010 kisha uniambie wewe unaona nini katika hizi posta na zinakupa ujumbe gani?
Picha inaongea maneno elfu moja.