A SAD LOVE LETTER
Najua hautamani kusikia lolote kutoka kwangu kwa kuwa sina thamani tena kwako, thamani niliyokuwanayo kabla hujanipatia ujauzito mara mbili zote ukanisihi nitoe. Kwa sababu ninakupenda nilifanya yote unayotaka. Ulipodai kuwa ukitumia kondom hujisikii raha sikuogopa kuibeba mimba ya tatu nilikuambia fanya unavyotaka.
Nilifanya haya nikiamini kuwa nalinda penzi langu kwako!!!
Naumia sana leo unaponiita mkimi Malaya!!! Mjinga tena mshamba!! Hakika hujakosea maana nilikuwa Malaya katika chumba chako, chumba ulichonifanya utakavyo tena kila siku, huku jukumu la kukisafisha ukiniachia mimi, kweli nilikuwa mjinga sana kwa kukulilia hata pale ulipokuwa umenikosea waziwazi na nilikuwa mshamba kwa kuwa ni wewe uliyenifundisha kufanya mapenzi kwa kutumia kila kiungo cha mwili wangu.