Kuna rafiki yangu aliwahi kuniambia , kule Urusi walikuwa wakipokea wanafunzi wengi miaka ya 50s na 60s kutoka China. Machina walikuwa hawana girl friend wala birthday celebrations . Kazi yao ni kitabu tu . Hakuna Jumamosi wal Jumapili.
Machina hawa ndio walio-sacrifice starehe zao na ndio waliokuja kuiinua China hii ya leo.
Kinyume na waafrika wao kila weekend lazima wafanye parties. Waaalikwe wasichana ,Pombe ndio ushindwe mwenyewe. Kila mwezi walikuwa na Birthdays kama vile huzaliwa kila mwezi.
Afrika kweli inaweza kupata maendeleo????
Huo ni mtazamo wako tu kwamba ili uendelee lazima usifanye sherehe au ku-relux. Kwa nchi zetu za dunia ya tatu hata ukiamua kutokula na kutokua na hayo uliyo yataja huwezi kuendelea bila kuwa na utawala wenye vision.
Wewe unasema wachina walikuwa wengi russia, umesahau kwamba watanzania nao walikuwa wengi sana miaka ya 70 na 80 huko huko russia na India hata ulaya ya magaribi kidogo. Swali hapa ni je, walivyorudi walikuta nini kimeandaliwa ili watumie ujuzi wao?? jibu ni hakuna.
Mfano ni wale wataalamu wetu pale Nyumbu, walikuwa na uwezo wa ku-design engines za magari na at the first stage waliweza lakini alivyochukua nchi mwinyi akafikiri nchi itaendelea kwa kuwa na wauza mitumba wengi, akaisahau nyumbu, leo wale wataalamu wote wako nje ya TZ wanapiga mzigo.
Kitu kikubwa ili nchi iweze kuendelea ni maandalizi ya muda mrefu kwa wananchi wake. Tanzania kwa mfano hatuna hata national priorities, kila serikali ikiingia inakuja na nyimbo zake kwa mwendo huo hatuwezi kufika.
Kama wanaoendesha nchi ya Rwanda wamesoma na kuishi Tanzania wengi wao, na sasa Rwanda inaonekana kupiga hatua kuliko sisi TZ, hiyo ni ishara kwamba tuna tatizo la uongozi/utawala na wala siyo wataalamu. Tuna endekeza siasa ktk kila kitu hata pale pasipo hitaji siasa.
Katika makosa ambayo Nyerere alifanya ni kuingiza siasa kwenye utendaji wa kitaalamu ili adhibiti migomo. Ndiyo maana unakuta mkurugenzi mkuu wa kiwanda ni mtu amesomea sheria, au siasa badala mtu huyo awe na taaluma inayo husiana na kiwanda kile, mfano mhandisi, n.k.