Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Pamoja na kwamba mshirika wake,Mmarekani hayuko vizuri kuendelea kumsaidia lakini bado Israel haijachoka kuchokoza majirani zake na bado inajiamini kuwa ina mpango bora wa kupata ushindi dhidi ya hatari ya kuzidiwa nguvu.
Baada ya muda wa kusitisha vita huko Gaza kuisha hapo juzi Israel imelalamikia msimamo wa Hamas kwamba wameonesha dalili za kukataa kuendeleza mapatano kwa hatua ya pili iliyopangwa katika makubaliano ya awali.
Hamas kwa upande wao wameona ni vyema kutoendelea na hatua ya pili kwani kwa hesabu zao Israel imekiuka mkataba wa mwanzo kwa takriban mara 200. Kubwa zaidi wamekataa kuondoka kusini ya Gaza na wamesitisha malori ya misaada kuendelea kuingia Gaza.
Hali wakati ni tete kiasi hicho Benjamin Netanyahu na waziri wake wa ulinzi wameviambia vikosi vya jeshi lao vijitayarishe kushika maeneo ya kusini ya mji mkuu wa Damascus kwa kusingizia cha kwenda kuwalinda waSyria wa jamii ya Druze.
Uchokozi huo wa wazi wa Israel unafuatia baada ya kendelea kuikalia milima ya Golan baada ya kuvunja azimia la UN iliyoka eneo la mpaka wa Syria na Israel kama eneo lisilotakiwa kuwepo majeshi ya upande wowote.
Kwa kujiongezea maadui na kujiamini mno Israel inaamini kupigana na kila mtu basi ndio kuwashinda maadui zake wao hao ijapokuwa hilo lina kila dalili za kuwanoa zaidi maadui hao wanaomzunguka kila upande.