Israel kabla ilikuwa inajulikanaje?

jonathan2018

Member
Joined
Oct 21, 2018
Posts
11
Reaction score
10
ki biblia, Israel ni nchi ya ahadi waliopewa waisrail. hivyo ni nchi ambayo haikuwa yao apo mwanzo..
je, kabla ya kuwa utumwani nchini misri. hawa waisrael walikuwa wanaishi nchi gani.. na je, wamisri waliwatekaje hawa jamaa adi kuwafanya wawe watumwa wao.. na hiyo nchi yao ya zamani kabla ya utumwa kwa sasa inakaliwa na watu gani....
Naomba kujuzwa na wanaofahamu hili..
 
soma bibilia mkuu utaelewa kila kitu, ukiwa na swali au kitu ambacho hutaelewa niuliza nitakupa majibu pls
 
Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.
3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema,
4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,
5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.
6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.
7 Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
 
Mkuu nitasummarise tu.... Abraham alikuwa anaishi huko Ur katika nchi ya mesopotamia ila baada ya vuta nkuvute na mfalme Nimrod /Amraphel mwisho wa akahamia nchi inaitwa canaan (Israel ya sasa) ambayo iliitwa canaana sababu ndipo waliishi mjukuu wa Nuhu aliyeitwa canaan na vikapita vizazi na mjukuu wake aliitwa Yakobo nickname yake akaitwa Israel na ndipo nchi walioishi ikachukua hilo jina. Baadae hao waisrael walienda utumwani huko misri kwa miaka 400 hivyo watoto wa Canaan sasa kina Amori,Hivi,Hiti,yebusi,amaleki,Rapha n.k waliishi huko hivyo waisrael waliporudi walikuta tayari sehemu kubwa ya hiyo ardhi ya canaan inakaliwa na hayo makabila ya watoto wa canaan.

Hivyo vita ikapiganwa kwa miaka kadhaa kati ya hao waisrael vs canaanites na mwisho wa siku canaan wakaporwa ardhi yao na wakakimbilia ilipo gaza ya sasa huko palestina hivyo kubadilisha jina la nchi hiyo kutoka kuitwa CANAAN hadi kuitwa ISRAEL/JUDEA and the rest is history.

NB: Israel sio nchi ya ahadi kwa Israel pekee bali ni nchi aliyoahidiwa Abraham na Mungu wake na wote tunafahamu Abraham alikuwa baba wa mataifa mengi ila kama kawaida ujanja ujanja wa Yakobo akaiba uzao wa kwanza na kujipa umiliki huo na hata baraka za Abraham akajimilikisha hivyo tusiseme nchi yao ya ahadi bali nchi aliyoahidiwa ABRAHAM.

Ni hayo tu
 
zitto junior jibu lako ni muafaka na funga kazi
anayetafuta Palestina au Israel au eti kuna Taifa teule lililoandaliwa na sisi ni wasindikizaji
asipoelewa pointi yako asilaumu mtu
 
Judea = Jodan
 
kwa mujibu wa biblia hao wanaitwa waisraeli walikuwa utumwani misri
lakini kihistoria hakuna rekodi yoyte ya wao kuwa misri utumwani,HAIPO
 
Hasa kilichowatoa kaanani kuja Misri ni njaa, kwa kweli usifanye mchezo na njaa , haina baunsa mkuu, kuna ndugu yao mmoja alikuwa na fursa misri ndio aliwavuta ndugu zake wote kuja kustiri matumbo misri, lakini kama unavyojua uongozi ni kupokezana vijiti, sasa mda ukaenda akaja kiongozi mwengine mithili ya jiwe huyo aelewi aliwafanya kama vijakazi mkuu walikuwa dhariri kweli kweli
 
Kabla ya taifa la Israel kuwa na kuitwa Israel, lilikuwa linakaliwa na makabila ya uzao wa nduguye Esau, Mungu akaagiza popote watakapokuwa wanapita wawaangamize na wajitwalie wao ardhi iwe yao maana amewaruhusu
 
MSINICHOKE WAUNGWANA..
NAENDELEA KUULIZA ILI NINOE ZAIDI UJUZI..
ETI NI KWELI KWAMBA CHEMBE CHEMBE ZA HAWA NEPHILS BADO ZIPO DUNIAN? KWENYE DUNIA YA LEO! KWASABABU HAWA JAMAA NDIO WALIKUWA MABINGWA WA UCHAWI NA UWEZO WA KISHETANI.. NA KAMA WALITEKETEZWA WOTE, MBONA MAMBO YA KICHAWI NDO YANASHAMILI SANA.. NA WATU NI WACHAWI SANA?. .. NA MAWAKALA WENGI WA UGANGA NA UCHAWI, WANGA, NK. + HAO FREEMASONS AND ILLUMINATS.. . JE! KUNA UWEZEKANO WA CHEMBE CHEMBE ZA DNA KU SURVIVE KWA WATU DUNIANI? NAWASILISHA NDUGUZE
 
😀😀 dah nmecheka sana hii comment.... Mkuu u've made my night
 
Mkuu hebu fafanua hapo. Kama sijapaelewa
story ya wayahudi kuwepo utumwani ni fabricated story
hakuna rekodi yoyote misri inayoonyesha waliwahi kuwepo kule utumwani
hata hiyo wanayoita exodus haina ushahidi wowote
haiwezekani watu milioni 3 au zaidi wasafiri kwamiaka 40 kutoka misri hadi israel halafu wasiache ushahidi wowote mahala walipopita!!!!
kwa ufupi hiyo stori ipo kwenye biblia tu na sio kwenye kitabu chochote cha historia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…