Israel Mwenda arudisha pesa zote Simba SC na kusepa klabuni hapo

Israel Mwenda arudisha pesa zote Simba SC na kusepa klabuni hapo

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Klabu ya Simba Sc imethibitisha kuridhia ombi la mchezaji Israel Mwenda kuondoka klabuni hapo baada ya nyota huyo kudai kuwa amepata timu nyingine

Taarifa ya Wekundu hao wa Msimbazi imebainisha kuwa nyota huyo alisaini mkataba mpya wa miaka miwili lakini kabla ya kuanza kuutumikia, aliandika barua ya kuondoka kwa madai ya kuwa amepata timu sehemu nyingine.

Snapinsta.app_455316974_18435176086071034_5300896429804545919_n_1080.jpg

“Simba kwa kujali na kuheshimu maslahi ya mchezaji ilimpa sharti la kurejesha fedha zote na tayari amerejesha. Simba ina thamini mchango wa Israel katika miaka yote mitatu aliyodumu nasi.

“Uongozi wa klabu unamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya ya soka.” imesema Simba Sc
 
Aende anakimbia sio level ya Simba kabisaaaaa, yaani mchezaji baba esta akiwa njia tu mnashikana tama
 
Back
Top Bottom