Israel Mwenda umekubali kukaa miezi 6 bila timu?

Israel Mwenda umekubali kukaa miezi 6 bila timu?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
We dogo una vielement vya kutojitambua au labda unajichukulia poa kiasi kwamba timu nazo zinakuchukulia poa.

Umeingia anga za usajili wa kimhemko wa Yanga ambao siku hizi wanasajili wachezaji ili kuikomoa Simba.

Huko ulipokwenda umekuta mambo hayaeleweki, timu haiwezi kusajili ina madeni mengi kama ya serikali. Ungekuwa na manager anayejitambua angeuliza hilo kwanza kabla haujatia saini.

Wamekupa mkataba wa miezi 6 ila hakuna mashindano utacheza maana haupo katika usajili rasmi wa NBC wala CAF. Baada ya miezi 6, kiwango chako kitakuwaje?

Soma Pia: Beki wa zamani wa Simba SC, Israel Mwenda atua Yanga kwa Mkopo akitokea Singida Big Stars

Mwisho wa msimu hao Yanga watakutupa maana lengo halikuwa kukusajili bali kukuharibia ili Simba isikurudishe. Picha la Baleke linaenda kukurudia wewe.

Pole sana. Binafsi niliona ulifaa kuwa mbadala sahihi wa Kapombe ila ndiyo hivyo haukuwa na subra.

PS. Kama vipi na wewe unga tela nenda zako FIFA kajikusanyie maokoto.
 
Kwa hiyo atachukua namba ya nani, Yao au Kibwana? Na atacheza wapi bila kusajiliwa?
Mwenda anacheza mbele ya hao wote nadhani uongozi unafanyia kazi hayo mambo kama walimchukua na wanamlipa lazima atacheza
Naangalia hapa marudio ya game ya Jana mwenda anahitajika sana
 
Mwenda anacheza mbele ya hao wote nadhani uongozi unafanyia kazi hayo mambo kama walimchukua na wanamlipa lazima atacheza
Naangalia hapa marudio ya game ya Jana mwenda anahitajika sana
Ila si tulikubaliana hakuna mchezaji wa Simba anaweza pata namba pale Yanga? Zimebaki siku mbili dirisha lifungwe, ngoja tusubiri tuone.
 
Ila si tulikubaliana hakuna mchezaji wa Simba anaweza pata namba pale Yanga? Zimebaki siku mbili dirisha lifungwe, ngoja tusubiri tuone.
Wapo wanaweza kupata number Zimbwe Kapombe Kagoma hata fadlu tunaweza kumpa yanga under 20
Nb:Mwenda ni mchezaji wa Singida
 
Nainjoy kuwavuruga hawa vyura. Hapo nasubiria mwarabu amalize kazi kwa mvurugano mkuu. Robo fainali iz not 4 everibade.
Ule uwanja unapikwaa yani wikii hii ni machinjio ya wanyama...damu lazima imwagike tuu mle..mpk tukicheza jumapili tutaona vumbi...hahaaa chezea robo fainale... 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Ule uwanja unapikwaa yani wikii hii ni machinjio ya wanyama...damu lazima imwagike tuu mle..mpk tukicheza jumapili tutaona vumbi...hahaaa chezea robo fainale... 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
Wanafungika vizuri tu pamoja na makafara yao
 
Back
Top Bottom