Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kauli mbiu ya rais Donald Trump wa Marekani ni kuifanya Marekani kuwa taifa kubwa kwa mara nyengine (Make America Great Again). Huu ni ukweli aliouona Trump tangu mwaka 2020 alipogombea na Joe Biden na ambao sasa ndio umezidi kudhihirika.
Kwa ujumla wake hiyo ni kauli ya kutapata kwa wazalendo wa Marekani na ambayo si rahisi tena kuitekeleza kutokana na mambo yalivyobadilika.
Mnamo mwezi Novemba mwaka jana mchambuzi mmoja wa masuala ya kivita alisema Uiengereza kwa muda huo ilikuwa na silaha na makombora ya masafa marefu ya kupigana na Urusi kwa muda wa chini ya mwezi mmoja tu. Ufaransa ilikuwa ni wiki mmoja tu na Ujerumani ni mchana mmoja kwisha tu.
Japo misaada mingi kwa Ukraine kutoka Marekani muda huo ilianza kusua sua ikitajwa kutokana na upungufu wa silaha pia lakini haikutolewa makisisia nchi hiyo ingeweza kumudu kuendelea kwa vita vya mfululizo na Urusi kwa muda gani.
Kauli anazozitoa Trump kutaka wapalestina wa Gaza wapelekwe Jordan na Misri ni fikra inayotoka moyoni mwake kuonesha ni jinsi gani asivyokuwa na huruma na wapalestina na kwa upande mwengine anavyoipendelea Israel ambayo kila kiongozi na tajiri mkubwa wa Ulaya hupenda kujinasibisha kwamba ana asili ya huko.
Ni ukweli usiopingika pia kuwa ni yeye huyo Donalda Trump aliyesisitiza kufikiwa muafaka wa kusitisha vita Gaza kabla hajaingia madarakani jambo ambalo limetekelezwa na Israel. Hiyo kiundani ni kutokana na kuwa Marekani haijioni na uwezo tena wa kuipatia Israel silaha kali za kuripua na majengo na kugeuza miji kuwa kifusi kama ilivyofanya kwa muda wa mwaka mmoja na zaidi tena bila kupata mafanikio yaliyokuwa yakitarajiwa.
Vita vya Gaza vilivyokwenda sambamba na vita vya Ukraine vimeifanya Marekani kuwa taifa dhaifu sana kiasi kwamba rais Trump anafanya mipango ya kujifufua kama ile ifanywayo na nchi za ulimwengu wa tatu.
Trump katika kuchanganyikiwa kwake kutokana na athari za vita amekuwa akianza kutengeneza serikali yenye watumishi wachache ambapo makampuni mengi ya kiserikali yametakiwa yawalipe wafanyakazi wao wengi pesa za miezi kadhaa kama kivutio cha kujiondoa kazini kwa hiyari.
Raisi Trump pia amewaona wahamiaji kama ni mzigo kwa taifa kinyume na mawazo ya matajiri wenye viwanda vikubwa. Kwa amri hiyo mitaa ya Marekani imekuwa ya mshike mshike watu kufukuzana na nguo kuchanika kama ilivyo kwenye miji ya nchi nyengine za kiamaskini duniani.