#COVID19 Israel yaanza kutoa dozi ya nyongeza dhidi ya COVID-19

#COVID19 Israel yaanza kutoa dozi ya nyongeza dhidi ya COVID-19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Israel imekuwa taifa la kwanza ulimwenguni kuanza kutoa dozi ya nyongeza ya chanjo ya COVID-19 kwa watu wenye umri mkubwa, huku waziri mkuu Naftali Bennet akitoa mwito kwa watu maarufu mitandaoni kusaidia kuhamasisha vijana kupata chanjo.

Hatua hiyo imechukuliwa wakati idadi ya Waisrael wanaopata chanjo ikipungua ikilinganishwa na maambukizi yanayozidi kuongezeka.

Afisa mwandamizi wa wizara ya afya Nachman Ash amesema hueda kukaanzishwa kizuizi cha kufunga shughuli mwishoni mwa mwzi iwapo idadi ya maambukizi a hasa yanayosababishwa a kirusi cha Delta itazidi kuongezeka.

Ujerumani na Ufaransa nazo zimehidi kutoa dozi hiyo huku shirika la kimataifa la afya WHO likitoa wito wa kusitishwa kwa utoaji wa chanjo hiyo katika nchi zenye watu wachache waliopewa dozi ya kwanza.
 
Back
Top Bottom