Israel yashutumiwa kwa shambulizi Syria

Israel yashutumiwa kwa shambulizi Syria

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imelalamikia shambulizi la anga linaloshukiwa kufanywa na Israel, ambalo limepiga jengo la ghorofa katika kitongoji cha Mezzeh mjini Damascus na kusababisha vifo vya raia saba, wakiwemo wanawake na watoto.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza BBC, shambulio hilo lilitokea Jumanne jioni, kwenye eneo ambalo lina ubalozi wa Iran na vituo vya kidiplomasia. Hadi sasa, jeshi la Israel halijatoa taarifa yoyote juu ya tukio hilo.

Hata hivyo, Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria, lenye makao yake Uingereza, limeripoti idadi ya vifo kuwa watu 13, wakiwemo raia tisa na wanachama wawili wa kundi la Hezbollah la Lebanon, linalounga mkono Iran na serikali ya Syria.

Shirika hilo lilisema shambulio hilo lililenga nyumba inayotumiwa na viongozi wa kundi la "Axis of Resistance" la Iran.

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Syria, Sana, chanzo cha kijeshi kimesema kuwa ndege za Israel zilirusha makombora matatu kutoka upande wa Milima ya Golan inayokaliwa na Israel, yakilenga jengo hilo.

Picha kutoka eneo la tukio zilionesha uharibifu mkubwa kwenye vyumba vya ghorofa ya kwanza, ya pili, na ya tatu, huku wafanyakazi wa huduma za dharura wakikagua uharibifu huo.

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu liliwataja waliouawa kuwa ni daktari wa Yemen, mke wake, watoto wao watatu, mwanamke mwingine na mtoto wake, pamoja na mwanamume. Ubalozi wa Iran uliripoti kuwa hakuna raia wake aliyeuawa katika shambulio hilo.

Hata hivyo, siku iliyofuata, shambulio jingine la Israel karibu na mji wa Quneitra, kusini-magharibi mwa Syria, lilisababisha kifo cha afisa wa polisi wa Syria.
 
Asubiri kidogo tu russia wanahamisha raia wao walioko israel wapato 1.5 million baada ya hapo myahudi watakiona
 
Asubiri kidogo tu russia wanahamisha raia wao walioko israel wapato 1.5 million baada ya hapo myahudi watakiona
Kashindwa vita ya ukraine aje amweze muisraiel ,ni maoni yako usiidhanie Israeil kirahisi
 
Kashindwa vita ya ukraine aje amweze muisraiel ,ni maoni yako usiidhanie Israeil kirahisi
Ukraine mrusi anapigana na mataifa 30, kwa israel ni mayahudi na hao US tu
 
Tutajie hayo mataifa 30.
sina muda wa kuandika utitiri mataifa hapa, elewa ni nchi za jumuiya ya NATO ulaya karibu zote na US, na sasa zimeongezeka Finland na Sweden karibuni
 
Back
Top Bottom