Israeli ni Wakristo waliozaliwa mara ya pili, sio wale jamaa pale Middle East

Israeli ni Wakristo waliozaliwa mara ya pili, sio wale jamaa pale Middle East

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Wagalatia 3:28 ,29
Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Ni hayo tu. Mfano mimi sio mmatumbi kimsingi ni mzao wa Ibrahimu mwenye sifa kuliko hao wa middle east. Badala ya mtu kwenda kuwashangaa na kuwashabikia bora unishabikie mimi.

Hivyo vita vya Iran na Israel hiyo ni vita vya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni na kidoogo ni maandalizi ya utawala wa mpinga kristo.

Hata wewe ukitaka unaweza kuwa mtoto wa ibrahim na muisrael kwelikweli. Uizrael wa Biblia sio rangi au taifa bali ni maamuzi.. mtu Yeyote duniani akitaka anaweza kuamua kuwa muisrael popote alipo.

Ni hayo tu...
Mtumishi Matunduizi
 
Sasa kina netanyahau na gallant ni watu gani kama si waisrael wana wa ibrahim?
 
Wale ni waisrael typically acheni watetee taifa lao katikati ya maadui wao. Kuleta siasa ni kufanya upotoshaji wa maandiko matakatifu hata kama kila mtu ni muisrael kwa imani ya ibrahim
 
Waisrael sio wakristo.
Lengo kuu la mwenyezi Mungu kuwaweka Israel Middle east ni ili kutokea hapo katikati ya dunia watu wote wamjue Mungu. Baada ya hilo lengo kufeli na hao jamaa kujitafutia majukumu Mengine wanaopenda wao, yeyote qmbaye alimuamini Yesu ndiye aliyefanyika mtoto wa ibrahimu na muizrael. Kwa hiyo hata pale middle east wayahudi waliomuamini Yesu ndio wanafanya familia ya wayahudi duniani wengine wale ni reject.
 
Sasa kina netanyahau na gallant ni watu gani kama si waisrael wana wa ibrahim?
Ndio Bible inasema hivyo, taifa teule ni wale waliomfuata kristo sio kuwa na vinasaba vya Abraham au Israel ya kimwili ndio kunakufanya taifa teule.
 
Kuleta siasa ni kufanya upotoshaji wa maandiko matakatifu
Hakuna upotoshaji Bible ndio imeandika hivyo, ilisema kabisa clear kuwa warithi wa baraka za Abraham na taifa teule ni watu gani.
1 Petro 2:9
[9]Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

1 Petro 2:9-10
[9]Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

[10]ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.
 
Wakristo sio wa Israeli kwa namna yoyote ile hata kiroho, we are not jews.
Any Christian outside Jews tunafahamika kama Gentiles.

Hakuna namna yoyote ile ambapo wakristo sisi tunachukua nafasi ya jews wala kibiblia Kanisa kuchukua nafas ya Jews.

Hili ni kosa inafanyika kufundisha hivi, na katika circles za theolojia hii tunaiita REPLACEMENT THEOLOGY.
 
Mkuu mimi nakuelewa.
Hizi dini za kutembea na mabendera ya Israel 🇮🇱 ni matokeo ya ukosefu wa maarifa sahihi.
 
Wakristo sio wa Israeli kwa namna yoyote ile hata kiroho, we are not jews.
Any Christian outside Jews tunafahamika kama Gentiles.

Hakuna namna yoyote ile ambapo wakristo sisi tunachukua nafasi ya jews wala kibiblia Kanisa kuchukua nafas ya Jews.

Hili ni kosa inafanyika kufundisha hivi, na katika circles za theolojia hii tunaiita REPLACEMENT THEOLOGY.
Sio kweli.
Jews wamekuwa hivyo kwa sifa ya utoto wa Yakobo, lineage ya urithi kutoka kwa Ibrahim. Wao wanaamini IBRAHIM NI BABA YAO, KUMBE ILI IBRAHIM AWE BABA YAKO INABIDI UMUAMINI YESU SIO MASUALA YA KIBAIOLOJIA. BIBLIA NI KITABU CHA KIROHO SIO CHA KUKUZA UTAMADUNI WA WATU FLANI.
 
Kumbe waGalatia alipotosha aliposema wakristo ni warithi wa ahadi za Abraham? Maana kwenye agano la jipya njia pekee kuingia mbinguni ni YESU na hao wayahudi walimkataa Yesu sasa watarithi vipi baraka au ahadi za Abraham na wamemkataa YESU? Nipe mstari mmoja tu agano jipya unaosema mtu ataingia mbinguni bila kupitia kwa YESU ili tuamini wayahudi ni warithi wa baraka za Abraham bila kumhitaji Yesu.
 
Wale ni waisrael typically acheni watetee taifa lao katikati ya maadui wao.
Uko sahihi. Na kufanya hii hawajaanza leo, ni part of Ibrahimic covenant
Kuleta siasa ni kufanya upotoshaji wa maandiko matakatifu hata kama kila mtu ni muisrael kwa imani ya ibrahim
kuna makosa makubwa sananyanafanyika katika theolojia ya jambo hili.
Hata kwa njia ya imani, sio kila mtu ni muisrael.
Jews are jews. And any christian outside Jews are called Gentiles. No where gentiles can take place for Israelites ..not even a church of christ biblically can identify itself to represent Israel as nation.
This wrong teaching is called REPLACEMWNT THEOLOGY na haipaswi kukubalika.

Mungu has convenants with Israelites,including Ibrahic and Davidic convenants.
Na kuna covenants ambazo ni strictly for Jewish people alone and we as Gentiles though are christians we are not part of them for example Sabath convenats.
 
Wapoland wote hao. Baba wa Netanyahu alikuwa akiitwa Benzion Mileikowsky akabadili jina kuwa Netanyahu ili aonekane Myahudi.

Gallant wazazi wake naye ni wapoland
Hili vuguvugu lilianzia poland vijijini likiongozwa na David Ben Gulion Atheist, ambaye kwetu sisi ndio kama Nyerere wao.
Wanaweza kuwa na vinasaba vya huko lakini hawako pale kwa misingi ya kimaandiko. Ni mapambano ya kisiasa na kimakazi tu kama wanavyofanya M23 kukomalia East Congo kwa sababu wanaamini mamabu zao wa kitutsi walikuwa wanaishi hapo.

Ndio maana hao baba zao wakina Netanyahu walipotaka kuletwa Uganda ili watengenezewe nchi humo walikataa wakitaka pale wanapoamini wanauhusiano napo.
 
Kumbe waGalatia alipotosha aliposema wakristo ni warithi wa ahadi za Abraham? Maana kwenye agano la jipya njia pekee kuingia mbinguni ni YESU na hao wayahudi walimkataa Yesu sasa watarithi vipi baraka au ahadi za Abraham na wamemkataa YESU? Nipe mstari mmoja tu agano jipya unaosema mtu ataingia mbinguni bila kupitia kwa YESU ili tuamini wayahudi ni warithi wa baraka za Abraham bila kumhitaji Yesu.
Swali zuri sana mkuu wangu ,i will be back
 
Sio kweli.
Jews wamekuwa hivyo kwa sifa ya utoto wa Yakobo, lineage ya urithi kutoka kwa Ibrahim. Wao wanaamini IBRAHIM NI BABA YAO, KUMBE ILI IBRAHIM AWE BABA YAKO INABIDI UMUAMINI YESU SIO MASUALA YA KIBAIOLOJIA. BIBLIA NI KITABU CHA KIROHO SIO CHA KUKUZA UTAMADUNI WA WATU FLANI.
Ahsante sana ndugu yangu, nimefurahi kuona mtazamo huu, japo naamini tunapaswa kusaidiana kidogo.

Kwanza ningependa usema ni kipi ambacho si kweli ili tusaidiane vizuri. What exactly hapo ambacho si kwel?

Next;

Naomba nianze kwa ku clarify mambo yafuatayo kama ulivyo yaandika na kuyaibua hapo juu:

IBRAHIM KUWA BABA YAO.
Ibrahim ndio chanzo cha Taifa la Isarel. Katika family tree yeye ndio yuko top pale na Yakobo (israel) ni mjukuu straight wa Ibrahim.
NA hivyo wana kila sababu ya kusema ni baba yao, wala hawahitaji kumuamini Yesu ili ibrahimu awe baba yao, ni baba yao LITERALLY, Quit your spiritulization even kwenye simole stuffs kile these. Hakuna application yoyote ya kiroho hapo kuhusu Ibrahim kuwa baba yao. Ni baba yao even by DNA maana ni blood lineage kama ulivyosema.

This is according to IBRAHIMIC COVENANT [Genesis 17:7,8]

Na hata mahala walipo hata sasa ni matokeo ya AGANO LA MUNGU NA IBRAHIM. Israel (nchi) ni URITHI wao waliopewa na Mungu kupitia Ibrahim.

Mimi na wewe na wengine ambao sio wayahudi sasa(Gentiles), tunafanywa kushiriki baraka za Mungu kwa Ibrahim kupitia kwa Yesu Kristo. Kwakua sis sio wazao wa Ibrahim by blood.

BIBLIA NI KITABU CHA KIROHO SIO CHA UTAMADUNI.
Hapa pia naaomba tuelewane vizuri sawa sawa.

Kwanza nakubali kabisa bible is not like a college textbook. It is not an intellectual mind that need help to help you comprehend and grasp the intended themes unless otherwise you just do it for academic purposes.
Biblia ni kitabu cha kiroho.Hapo sipingani na wewe ndugu kwasababu

1. Bible haikuandikwa kwa mapenzi ya Mtu bali mapenzi ya Mungu kwa uongozi wa Roho mtakatifu aliyewatumia aliowachagua kufanya kazi hiyo
  • [2 Peter 1 : 20 , 21]
  • [2 Timothy 3: 16, 17]

LAKINI usisahau kuwa kwakias kikubwa sana Wayahudi na Utamaduni wao ambao mpaka sasa bado wana practise, ndio hasa maandika yameandikwa yakicheza humo. Kwahiyo huwez tenganisha utamaduni wa kiyahudi na maandiko ya biblia.

Ndio maana unaposoma ili kuelewa ni MUHIMU na lia ni LAZIMA kuzingatia suala zima la utamaduni ili kutochukua kila kichoandikwa na kuki apply kama kilivyoandikwa.
You must read and understa the text out of context and context out of the whole book or several chapters.

Muhimu sana.
Kuna mambo mengi mlee ambayo yameandikwa na ni utamaduni typically wala sio kiroho ndugu.

Ahsante
 
Wagalatia 3:28 ,29
Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Ni hayo tu. Mfano mimi sio mmatumbi kimsingi ni mzao wa Ibrahimu mwenye sifa kuliko hao wa middle east. Badala ya mtu kwenda kuwashangaa na kuwashabikia bora unishabikie mimi.

Hivyo vita vya Iran na Israel hiyo ni vita vya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni na kidoogo ni maandalizi ya utawala wa mpinga kristo.

Hata wewe ukitaka unaweza kuwa mtoto wa ibrahim na muisrael kwelikweli. Uizrael wa Biblia sio rangi au taifa bali ni maamuzi.. mtu Yeyote duniani akitaka anaweza kuamua kuwa muisrael popote alipo.

Ni hayo tu...
Mtumishi Matunduizi
HUO NI URONGO BWANA
 
Kumbe waGalatia alipotosha aliposema wakristo ni warithi wa ahadi za Abraham? Maana kwenye agano la jipya njia pekee kuingia mbinguni ni YESU na hao wayahudi walimkataa Yesu sasa watarithi vipi baraka au ahadi za Abraham na wamemkataa YESU? Nipe mstari mmoja tu agano jipya unaosema mtu ataingia mbinguni bila kupitia kwa YESU ili tuamini wayahudi ni warithi wa baraka za Abraham bila kumhitaji Yesu.
Kuna mambo mawili hapo chief umeyaongelea. Baraka za ibrahim na Kuingia mbinguni.

moja wapo ya baraka za Ibrahim ni urithi wa nchi waliyopewa na Mungu. Hil ni agano la Mungu na Ibrahim la milele ,never ending. ABRAHAMIC COVENANT. unajua content ya agano hii ikoje?
ZABURI 105:9-11

Na hii kila myahudi ameshairithi , maana ndio sababu ya wao kuwepo kwao pale, na ndio sababu Hakuna myahudi atakuja kuelewa kuhusu kuondoka au kuondolewa middle east ever toka 1948 baada ya kutimizwa kwa unabii wa Israeli kukisanywa uoya kama taifa.

Baraka hii sio kwaajili yako wewe mkristo ambaye si myahudi.
Wewe na mimi tuna qualify baraka ya ibrahimu kwa kushiriki haki ya kupata wokovu ambayo nayo tunapata haki hiyo kwa kumuamini Kristo aliye wa uzazo wa Ibrahim ,so kwa kristo tunafanywa warith wa kupokea baraka ya kurith uzima wa milele ambao na wayahudi pia ni haki yao.. lakin baraka hii ya pili, sote sisi Gentiles na wayahud tuna qualify kwa kupitia mchakato mmoja unaofanana, KUMUAMINI NA KUMKUBALI YESU kama Masihi wa Mungu.
Baraka ile ya urithi wa ardhi ,mimi na wewe haituhusu na wayahudi wana qualify straight kwakua ni watoto wa Yakobo mjukuu na uzao wa ibrahimu, haijalishi walimkubali au hamkubali Yesu. Hii ni haki yao na Mungu kawapa.

Suala la pili ka kurith uzima wa milele na mbingu liko wazi.Ni kupitia kumkubali Kristo na hapa hakuna cha myahudi wala myunani wala mmatumbi. Kipimo ni kile kile. Tunaingizwa katika agano la Ibrahim kwa kifo cha Yesu (ukimuamini).

Na kwa wayahudi waliomkataa kristo (maana wapo waliomkubali na wanaomkubali hata sasa na kuokoka), watahukumiwa kama mtu yeyote yule aliyemkataa Kristo.

Na katika ile miaka 7 ya dhiki, hapa ndipo wayahud watafungukiwa macho na kufahamu kuwa waliyemkataa (Yesu) ndiye masihi ,na wala sio yule ambaye mpaka sasa wanamgonjea (mpinga kristo).
Na watakapojua hili watamuombolozea, na wataokolewa kwa tabu ya dhiki kuu)
 
Back
Top Bottom