Israeli ni Wakristo waliozaliwa mara ya pili, sio wale jamaa pale Middle East

Asante kwa fafanuzi.
Turudi kwa nini Ibrahim, Kwa nini Israel. Msingi ulikuwa ni utimilivu wa unabii wa Mungu sio waisrael kama kikundi cha watu maana haa hivyo Mungu hakuwachagua kwa sababu yoyote ile waliokuwa nayo yenye ubora zaidi ya jamii nyingine. Bali kwa sababu ya kiapo ambacho aliapa na mababu kupitia Ibrahim dunia nzima ibarikiwe.
Kumbukumbu la Torati 7:8
bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.

Mwanzo 22:18
na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.


Mzao hapo sio kila myahudi. Bali alichagua Yesu azaliwe kupitia wao ili baada ya hapo wote watakaompokea Yesu wanafanyika warithi wa ahadi hiyo. Hata wayahudi wakikataa wamejitoa kwa makusudi katika kineage ya Uzao wa ibrahim.

Na haianzii kwa Ibrahim, inaanzia kwa Adam kabisa kuwa mzao wa adam atamponda nyoka kichwa. Maana yake alikuwa ni Adam wa pili Yesu sio kikundi cha watu.

Yesu anakuwa kama mzabibu wayahudi ndugu zake wanakuwa nj matawi, sisi sio wamataifa bali ni mizabibu pori amboo tumekuja kuunganishwa na Yesu kupitia Artificial gratification. Na warumi imeweka vizuri Yesu. Hivyo kiini ni Yesu Ibrahim nq sio mtu mwingine yoyote mkuu.

Warumi 11:17
Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,

Warumi 11:18
usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe.
Warumi 11:19
Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi.
Warumi 11:20
Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.


Mkuu huo ndio msingi wa maandiko. Hayajaja kwa ajili ya kuwapa uspecial kikindi cha watu bila kujali kama kinamtii au la. Bali walikiwa njia ili kupitia wao azaliw mkombozi ambaye kwa yeye kila amwaminiye awe mrithi wa ahadi za ibrahimu yaani Uzima wa milele.

Kuhusu tamaduni ni kweli zimeelezwa, ila pia sio zao Mungu aliwapa makusudi ili hizo tamaduni (images) zituelekeze kwa Yesu (object). Hivyo kila tamaduni inafunzo la kiroho ambalo ndio sababu ya uwepo wake. Wao wamekomalia vivuli na wameacha object kwa makusudi.

Ndio mqana Paulo anaungana na ninachokisema anawaadress ywakorintho akiwaunganisha na wayahudi kana kwamba wakina Musa na haruni na wao walikuwa ni mamababa zao.

1 Wakorintho 10:1
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;

1 Wakorintho 10:6
Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.



Tuendelee kuchimba maana maarifa ya Mungu hatana mwisho.

Barikiwa sana.
Tuko pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…