Issa Michuzi kaandika kwenye blog yake kuwa yuko vekesheni, na kweli anatundika picha mbalimbali akiwa anajivinjari sehemu mbalimbali nchini Marekani.
Ninachojiuliza, je ni kweli amejilipia vekesheni hiyo yeye mwenyewe au yuko kwenye msafara wa Rais Kikwete nchini Marekani?
Kama yuko kwenye msafara wa rais, ina maana analipiwa gharama zote na pesa ya walipa kodi. Je ni halali kufanya ziara ya kikazi kuwa vekesheni yake na kufanya shughuli binafsi kama alivyoonyesha kwenye picha mbalimbali kwenye blog yake?
Kwa mshahara wa mfanyakazi wa serikali kama Issa, sio rahisi kufanya vekesheni sehemu mbalimbali za dunia, na kujigharimia mwenyewe. Je Issa Michuzi anapata wapi pesa hizi?
Je, Issa Michuzi ni fisadi au anafadhiliwa na mafisadi kwenye safari zake? Kama mfanyakazi wa serikali, Issa Michuzi anatumia muda kiasi gani ofisini, akilitumikia Taifa kama muda mwingi anakuwa safarini, na kwa nini anatumia muda wake mwingi kwenye shughuli zake binafsi kama safari zake zinalipiwa na walipa kodi?
Naomba kueleweshwa na yeyote mwenye kujua zaidi.
Picha zote zimetoka Michuzi blog.