Issa Michuzi na vekesheni

Status
Not open for further replies.
Kwani Michuzi amelipiwa pesa na mwajiri wake kwenda kufanya shughuli zake binafsi?

Nani kamlipia nauli?

Na inakuwaje video clip ya habari hiyo hiyo inatokea kote DAILY NEWS na Michuzi? Who owns it?

Mfano, video ya mabomu Mbagala ilitokea DAILY NEWS na MICHUZI.

Video ya Kassim Dewji ilitokea DAILY NEWS, ikawa ukibonyeza haichezi. Kesho yake ikahamishiwa MICHUZI, ikawa inacheza. Mpiga picha huyo huyo mmoja. Sasa zile video ni copyright ya serikali au ni mali ya MICHUZI?

Halafu, just because kuna watu wengi wanachomoka muda wa kazi kwenda kwenye miradi yao, that doesn't make it appropriate.
 


Hujaelewa point, and the point is, badala ya Michuzi kudeclare kwa wananchi kwamba ametumwa kazi na muajiri wake, yeye anasema anaenda vekesheni. Tena alivyo na kiburi, asiyejali pesa za serikali, asiye naheshima kwa mwajiri wake, anathubutu kusema kwamba ataendelea vekesheni Ujerumani na Australia.

Michuzi katudharau walipa kodi, anaona tunamshambulia. Yeye sio wa kwanza, anashambuliwa Salva ije kuwa yeye?

Kikwete naye aanzishe blog kuzuia mashambulizi toka kwa wananchi?
 
Ila mkuu Uwiano
hiyo quote hapo juu naona inakataa kubalansi
 

Hapa Bluray,

Ukweli mtupu! Umepigilia msumari wa nguvu. Kuna matumizi mabaya ya hela za umma katika hizi safari. Na Michuzi anasaidia sana kuleta ufafanunuzi ki-usanii-pengine hata yeye mwenyewe kujua.

Kama kawaida kwenye safari ya kuwakoma wala jasho la walipakodi, lazima wasindikizaji wawepo. Kwa makusudi kabisa wanashindwa kuelewa kuwa hapa ishu si wivu wa "kike" (ambao mi ni naona anayesema hivyo ni mbaguzi na mnyanyasaji wa kijinsia). Ila ni kutokuelewa.
 
Wewe UM katafute kazi ya kufanya..sasa ni madudu gani haya unatuletea jamvini?

Usimlaumu sana UM kwa sababu yeye kama memba wa jamvi kaleta mada ijadiliwe. Na nadhani majibu keshapata. Kama kaka Michuzi atakuwapo jamvini anaweza kumfafanulia vizuri.
 

UM,
Nilikuwa sijakuelewa sasa nimekulewa vizuri. Kumbe mnatafuta nafasi nyingine kwa mtu wenu wa Habari Corporation! Mmeona nafasi ya Michuzi ni nyeti mnataka mmtoe mweke mtu wenu kama mlivyomweka Salva Ikulu. Haya ujumbe wako umefika na binafsi nimekulewa vizuri. Haya endelea na kampeni yako.
 


Yaelekea wewe mtu wa visasi sana, hupendi kukosolewa na umezoea kupigiwa mapande. Kwa taarifa yako siko habari corporation. Hiyo ilikuwa katika kukupa mifano tu ya watumishi wa serikali.

Hapa ni kumkosoa Michuzi, aache kwenda vekesheni kwa kutumia pesa za serikali, au aache hiyo kazi aendelee na vekesheni.

Nyie ndio wale wale ambao mkipenda mnaita kengeza, na kwa vile mmezoa kupea kazi not on merit bali on kujuanakujuana, basi unadhani wote wanatabia hiyo.

Kwa tabia kama yako, ya kujifanya kipofu, kujifanya huoni kosa hapo, ndio kosa hilo hilo linatucost wananchi kushindwa kuoiondoa CCM madarakani. Eti kutaka kuiondoa CCM madarakani ni kutaka kuiweka CHADEMA, na kuifukia dhana halisi ya kuiondoa CCM madarakani ni kutaka mabadiliko.

Kama wewe ndio Michuzi, ni vyema unatumia nafasi hii kuelezea kwa nini unakwenda vekesheni kwa kutumia pesa za walipa kodi na sio kuanza kuspin na kupoteza muelekeo wa mada.


Kwa taarifa yako tu JF iko kumulika na kuexpose uozo wote wa nchi hii, sio wa RA&CO only, sababu iliyokufanya uingize mambo ya habari corporation humu.
 
Usimlaumu sana UM kwa sababu yeye kama memba wa jamvi kaleta mada ijadiliwe. Na nadhani majibu keshapata. Kama kaka Michuzi atakuwapo jamvini anaweza kumfafanulia vizuri.

Nashukuru umeliona hili. Baada ya UM kuleta mada yake na mimi nimejadili..au kuna la ziada?
 
Wanapokuwa wanakata ticket huwa waajia ratiba inaisha lini, kwa nini wasirdi nyumbani soonest possible kuokoa pesa za walipa kodi?

Hatujui ratiba inaisha lini. Lakini ni kweli si vema kuendelea kukaa nje kama ratiba imeisha ili tu kuendelea kupata masurufu!


What so special with a photo by Michuzi? cant a photo be taken by anybody from the Tanzanian Embassy in the United states?

Hapa unaanza kuharibu argument yako yote. Kwanza jifunze kuheshimu taaluma za watu wengine. Kupiga picha ni taaluma, si kila mtu anaweza kupiga picha katika standard inayotakiwa kuwekwa kwenye magazeti na record nyingine za serikali. Itafika mahali utaanza kuhoji ni kwa nini wanatembea na makamera makubwa wakati wangeweza kutumia kamera ya kwenye simu tu!

Kwa mfano, kwa nini isiwe lazima kwa secretary wa Ubalozi kujua kupiga picha ndipo aaajiriwe ili aweze kufanya kazi kama hizo inapobidi? Huu ni ufujaji wa pesa za walipa kodi usio wa lazima.

Hili linawezekana lakini kwa matumizi ya balozi husika. Lakini Bw Michuzi ameajiriwa na Daily News (kama sijakosea!), na ninaamini ndo waliomtuma. Hao wanabalozi watakuwa wanawajibika kwa magazeti pia?

Hoja yako ya msingi nadhani ni kwa serikali kujaribu kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwenye misafara ya Rais. Lakini katika kujenga hoja hiyo, uamuzi wa kupitia kwa uwepo wa Michuzi kwenye msafara huo nadhani umekuvurugia hoja nzima na kufanya ionekane kama wivu tu!
 
Last edited:
Inaonekana huyu jamaa aliyeleta habari hii jamvini ana mawivu, kila siku tunasema wabongo tuwe wabunifu wa mambo ambayo si ya kifisadi lakini Michuzi amekuwa akifanya kazi nzuri; na kumbuka ana vodacom, tigo na makampuni kibao yanadhamini Blog yake. Fanyakazi acha majungu.
 
Hii discussion ni ya kimasikini sana na nahisi aliyeitoa jamvini hajawahi toka kikazi japo kwa masaa.

Kw ataarifa yako unaposafiri kikazi ndio unapata nafasi ya kipekee kufanya au kuwaona watu ambao ingekuwa gharama sana kuwatembelea kwa gharama zako.

Huu ni wivu usiokuwa wa kimaendeleo. Michuzi kaza buti achana na waliokata tamaa na maisha.

Kama serikali imekulipia nauli na malazi utashindwaje kujilipia nauli ya daladala kwenda kuwasalimia jamaa zako? Nani asingefanya hivyo? au haujui kama ukiwasafarini kikazi unalipwa padiem?
 
hahahaha mkuu Msanii alicho shika misupu ni nini hicho cheusi?
 
karibu MtindiowaUbongo


Asenti..tuanze hapa:

  1. Nilishawahi kumkuta zaidi ya mara moja akitumia credit card yake kuetembelea website za ngono na kufanya bookings. Yaani badala ya kuijengea mazingia bora familia yake yeye anatumia jasho lake kutafuta machangudoa online....Ukweli lazima usemwe.
Huyu anayesema amemuona Michu anafanya sagulasagula kutembelea website za ngono..ok fine enough...eeer lets say ni kweli...I have newz for this stalker..LIVE YOUR LIFE! ukiwa nchi za watu utafungwa kwa u-stalker!
 
Karibu sana AbbyBonge
Kwa hiyo kwa nauli ya serikali unadiriki kuudanganya umma kuwa umeenda vekesheni??? hii inatilia shaka hata hizo nyuzi anazoripoti kama hajaongezea chumvi ili kusaka uhalali.

Enewei natoa hoja tu
 
Ah mkuu jamaa ameshika mguu wa mtoto huyo. we acha tu hahaha

hehehe sasa huo mguu anautumia mwenyewe au zawadi kwa nanihii? awe anautumia yeye anapo kuwa vekesheni.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…