Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wanachama wa CCM ndiyo ilikuwa silaha ya ushindi kwa chama chao. Mh lakini ukitupia kwa jicho la tatu je ni kweli wanachama pekee yao au kuna namna ilifanyika tangu mwazoni?
==================
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kuwa ushindi wa kishindo ulioupata kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024 umetokana na juhudi za wanachama wa CCM waliokitafutia kura za ushindi, tofauti na baadhi ya taasisi zinavyoeleza.
Katibu wa NEC, Idara ya Organaizesheni CCM Issa Ussi Gavu ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kawaida cha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), kilichofanyika Jijini Tanga leo Desemba 15, 2024.
"Kulikuwa na taasisi nyingi nje ya mfumo wa chama chetu, niwaambie tu kuwa hakuna taasisi, kikundi wala mtu aliyewezesha ushindi wa chama chetu.Tuliopambana kukitafutia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni sisi wana CCM," amesema Gavu