Issue ya Fei Toto ni siasa za mpira

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Siasa za mpira bongo zimerudi tena kwa kasi Sana

Contract termination ni Kati ya mchezaji na club je imefanyika hivyo?

Mchezaji hawezi kuongea na club nyingine mpaka mkataba wake uwe umebakiza miezi 6 je ipo hivyo kwa fei toto.?

Vipengele vya kuvunja mkataba vipo 3 ikiwa hauchezi kama mlivyokubaliana kwenye mkataba kama ilivyokuwa issue ya Onyango na simba je fei toto achezi yanga?

Ikiwa haujalipwa mshahara wa miezi 3 iliyopita kama ilivyokuwa kwa Msuva na Waydad casablanca ya Morocco.

Je haya masharti yanga wameyakiuka kwenye mkataba?

Azam wanamshawishi kwa mshahara wa milioni 10 je ameongea na yanga milioni 10 wamegoma jumpatia?

Azam wamemwahidi jumba la kifahari tufanye kama milioni 200 je yanga wanashindwa?

Je Azam wamekaa mezani na Yanga kuomba kumnunua fei toto!!!?jibu hapana..

Ukifatilia yote hayo utagundua ni mchezo ni siasa either imechezwa na Yanga au azam wenyewe .

Azzam wanajua ubora wa yanga wanaweza kucheza hii mchezo ili yanga waache ku focus kwenye game yao ya kesho

Hakuna mchezaji mwenye mkataba wa miaka zaidi ya 2 anayeweza kuondoka kienyeji hivi kwenye timu yeyote duniani.

Labda kama Fei hakuwa na mkataba na Yanga sawa yanaweza kutokea mauza uza kama haya!!!
 
Kwasasa Yanga Wana Focus kwenye Mechi dhidi ya Azam na ilo ndilo linalo hitajika kwasasa. Mitandaoni wawaaache watu waandike wanavyoweza kikubwa ni point tatu.
 
Huu uzi umezungumza ukweli sema mashabiki wa simba hawatauchangia coz wanataka kusikia Deal done kaenda Azam ila hawaelewi inatakiwa iweje ili aende huko.
 
Hapa tunazungumza tu lakini wangapi wameona mkataba kati ya feisal na yanga pia usikariri kuwa kuvunja mkataba Kuna vipengele vitatu kila mkataba una vipengele vyake.
 
Unakosea unapozungumzia mambo ya mikataba ya wachezaji wengine kwenye issue ya kimkataba kati ya Fei Toto na Yanga SC, tambua vipengele vya mikataba tofauti sio lazima kufanana.

Na unapoorodhesha hayo mambo yaliyopo kwenye mkataba wa Fei Toto kama ndio yanamzuia kwenda Azam, kwani suala la kuvunja mkataba kwa kununua sehemu iliyobaki halipo kwenye mkataba kati ya Fei Toto na Yanga?

Kama lipo, basi hapo hakuna kosa kisheria, naona Yanga wanaanza kulia lia tu mitandaoni Fei haondoki, lakini wajue kama akiamua kuondoka kwa kununua sehemu ya mkataba iliyobaki hakuna wa kumzuia, nyie ombeni Mungu tu awahurumie kwa hivi vilio vyenu.
 
Mi ninachojua mwanasheria wa yanga ni kilaza hajawahi kushinda hata mechi moja kama huamini utaona subiria kwenye hili sakata yule jamaa anawatia hasara lakini bado wanamng'ang'ania
 
wewe nawe acha kukariri unafikiri Mkataba wa Nkane na wa Morisson unaweza kuwa sawa katika kuvunja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…